Nabii Frank Julius Kilawah mnamsoma?!

Nabii Frank Julius Kilawah mnamsoma?!

Sasa hii ndio HOJA YA MSINGI. Kama ni kweli kua wanao mfata chemba(private) anawalipisha pesa, hapo pana tatizo.Kama kuna mtu anaushahidi usio tia shaka, tunaomba atujuze lakini Ole wako kama unamzushia, laana itakua juu yako na juu ya uzao wako(Mungu aliahidi kuwalaani wale wote watakao wasema manabii wake vibaya).Yesu aliwaambia wanafunzi wake na hata sasa anaendelea kuwakumbusha kuwa "mmepewa BURE, toeni BURE". Ila msisahau maandiko yasemavyo ya kua "msiende nyumbani mwa Bwana mikono mitupu."
 
Jamani hawa Watumishi wa Mungu haitakiwi kuwasema vibaya, Kuhusu uponyaji hata Yesu Kristo hakuponya wote ila ni wachache tu.
 
Mtoa mada akili huna, hujui hadi leo tu jinsi WACHUNGAJI HAWA WANAIGIZA KUPONYA WATU, hata hujui kidogo tu wanaigiza vipi..? Kaa na ujinga wako, uliwe vizuri, hao watu wanatengenezwa ww, acha ujinga, na wako kibiashara 10000%, ujinga kazi sana..
 
Kwahiyo watumishi wanao ombea watu afu hawaponi hao ndo watumishi wa kweli, ila wale wanao waombea watu uponyaji na wanapona hao ndo matapeli? Kama kweli Frank anafanya kazi za shetan basi Shetan ananguvu kumzidi Mungu. Eliya alisimama hadharani akasema naijulikane leo, sasa mbona nyie mnamponda huku mmefichama? Jitokezeni hadharani nanyie ili tijue uwezo wa Mungu wenu!
Mti wenye matunda ndio unaopondwa mawe
 
Huyo jamaa mbwaaaa mkubwa sana mimi nashangaa watu kama hawa serikali inawatazama tu. Stupid
 
Hii hoja ya kusema kama Frenk anaponya kweli basi aende maospitalini waliko wagonjwa, siiungi mkono hata kidogo kwasababu hata Yesu mwenyewe hakuwafata wagonjwa majumbani wala mahospitalin Bali wote walio letwa kwake walipona. Tena wengine waliulizwa maswali ambayo kama ungeulizwa wewe ungesema Yesu anadharau, lakin walijibu kwa imani na wakapokea uponyaji. Nakama wanao ponywa hamuwajui, basi tafuteni wagonjwa mnao wafahamu then muwapeleke ila msisahau kutupa mrejesho.
Nimehudhuria ibada kwa nabii Frank Julius Killawah Tanga na DSM. Kwa macho yangu nimeshuhudia vilema wakitembea, mtu aliletwa kapooza kwa kuvunjika uti wa mgongo aliiinuka mbele yetu, na mengine mengi. Jirani yangu kaponywa ukimwi. A
 
"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" Kama wana uwezo wa kutoa mapepo, pia wana uwezo wa kuyaweka. Hivyo wanafanya kiini macho cha kuwatia mapepo na baadaye anayatoa tena kwa kiini macho. Tunajua kwamba wote hawa ni matapeli tu. Wachuma wasipopanda. Kutwa kuhubiri magari nyumba na pesa pumbavu wakubwa. Mungu amewawekea zawadi zenu kwa mahubiri yenu. Ona hili jingine juzi limeanza kushushwa ht halijitambui tena. Mungu alisema" ataejikweza atashushwa" wauza unga, walevi na wazinzi ndio hao hao kwenye madhabahu wanahubiri bila aibu. Jamani muogopeni Mungu!! Mwingira, Lusekelo, Davvie, Ngurumo nk hizo fedha mnakusanya kila siku kwa nn msiwasaidie wale wahitaji wanaolia kila siku milangoni mwenu? Aibu zenu.
 
Kwamba "wewe ulilogwa na fulani,mahali fulani,kwa sababu fulani". Anatoa mfano wa kukausha kidonda cha mtu ndani ya dakika 3.Jamani mnamsomaje huyu jamaa

huyo hana tofauti na mganga wa kienyeji,

hana cha unabii wala utume

ni kati ya wapiga dili wa kitanzania wanotumia jina Mungu kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu
 
Proud to be RC....huko kwingine kunipite tu

Sio mkatoliki na sijawahi, ila nina imani na Kanisa Katoliki kwa sababu ni kanisa lenyemfumo mzuri wa uongozi duniani, zaka na sadaka zitolewazo na waumini wake, hutumika kwa faida ya waumini wake na jamii nzima,

Kanisa hujenga shule, hospitali na huduma nyingine za kijamii, huduma ambazo hupunguza makali ya maisha ya waumini na jamii,

tofauti na dini nyingine ambazo zaka na sadaka huwa mali ya mtu au kikundi cha watu kwa manufaa ya viongozi,

wengine hujenga majumba, hununua magari ya kifahari, wengine huutumia zaka na sadaka zitolewazo na waumini wao kugharamia maisha ya vimada wao.
 
Ramli chonganishi, lakini pia yawezekana anamtaja mtu wala hayupo na na kwa kuwa yule mgonjwa ametajiwa fasta hana mda wa kuuliza, kukubali au kukataa. " YAKO IMEKUPONYA" shika sana imani yako...
ukifika pale siku ya kwanza utakutana na watu watakao kupa darasa kidogo.
watakwambia kila atakacho ongea huruhusiwi kukataa ukikataa hakusaidii tatizo lako
 
Huyu jamaa yupo pale Majestik sinema Tanga ambapo ni karibu sana na hospitali ya Bombo. Kwanini asiende Bombo akawaamsha wale wagonjwa ?? au yeye ni mganga anatibu waliorogwa tu.

Hao aliotibu hata mmoja hafamiki. ni watu tu alio arrange nao before tukio.
Kama nabii kweli aje ocean road atibu watu asituibie wake zetu tu maana asilimia kubwa ya waumini wake ni wanawake
Sawa kabisa wanawake wao waneendeshwa na hisia,sisi wanaume tunaendeshwa na kufikiri
 
"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" Kama wana uwezo wa kutoa mapepo, pia wana uwezo wa kuyaweka. Hivyo wanafanya kiini macho cha kuwatia mapepo na baadaye anayatoa tena kwa kiini macho. Tunajua kwamba wote hawa ni matapeli tu. Wachuma wasipopanda. Kutwa kuhubiri magari nyumba na pesa pumbavu wakubwa. Mungu amewawekea zawadi zenu kwa mahubiri yenu. Ona hili jingine juzi limeanza kushushwa ht halijitambui tena. Mungu alisema" ataejikweza atashushwa" wauza unga, walevi na wazinzi ndio hao hao kwenye madhabahu wanahubiri bila aibu. Jamani muogopeni Mungu!! Mwingira, Lusekelo, Davvie, Ngurumo nk hizo fedha mnakusanya kila siku kwa nn msiwasaidie wale wahitaji wanaolia kila siku milangoni mwenu? Aibu zenu.
Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote. Ila tunacho paswa kujiuliza ni kwamba, nani ni NABII wa kweli hapa Tanzania? Maana Bwana asema akiwepo NABII kati yenu mim Mungu nitasema nae si kwa mafumbo bali ni waziwazi! Na kama Taifa halina NABII basi kuna mahali tumemuasi Mungu kama Taifa na TOBA ya kitaifa ndio salama yetu.
 
ukifika pale siku ya kwanza utakutana na watu watakao kupa darasa kidogo.
watakwambia kila atakacho ongea huruhusiwi kukataa ukikataa hakusaidii tatizo lako
Brave .3, ulikutana na hiyi situation au umehadisiwa? Fafanua ili tujue ukweli halisi wa huyu NABII!
 
hawana tofauti na waganga wa kienyeji wote wanatumia majini ya utambuzi
 
Mungu nisaidie kuamini kama kweli umewapa watu wako uwezo wa kufanya mambo makubwa kiasi hiki. Nimeshuhudia semina za Prophet Frank kupitia Chanel 10 na Star TV.

Daah jamaa ana upako wa kutisha,anaponya within a minute.Kina bibi wanatupa magongo within a minute.Kama Yesu karudi vile kinachovutia zaidi ni kutoa historia ya matatizo ya watu katika namna ya kipekee.

Kwamba "wewe ulilogwa na fulani,mahali fulani,kwa sababu fulani". Anatoa mfano wa kukausha kidonda cha mtu ndani ya dakika 3.Jamani mnamsomaje huyu jamaa
Nilichoka pale nilipomsikia akisema Heeeel Jesus sijui ni kwa kusahau au kwa kukusudia tena kwa kufichaficha kama vile kusema Heal Jesus
 
Nilichoka pale nilipomsikia akisema Heeeel Jesus sijui ni kwa kusahau au kwa kukusudia tena kwa kufichaficha kama vile kusema Heal Jesus
Waweza nielekeza kwako ili liwezekane lile ulilotia shaka?au umesahau Ahadi yake Yesu?kwanini mnamashaka mioyoni mwenu? Je haikuandikwa kwamba waweza zijaribu Roho?Umefanya hivyo?Msiumize mioyo yenu kutafakari kazi za Mungu kwa akili za kawaida

Kubali kukaa ktk Roho nawe utajuzwa kwamba haya yanafanyika kwa Mamlaka gani!
 
Waweza nielekeza kwako ili liwezekane lile ulilotia shaka?au umesahau Ahadi yake Yesu?kwanini mnamashaka mioyoni mwenu? Je haikuandikwa kwamba waweza zijaribu Roho?Umefanya hivyo?Msiumize mioyo yenu kutafakari kazi za Mungu kwa akili za kawaida

Kubali kukaa ktk Roho nawe utajuzwa kwamba haya yanafanyika kwa Mamlaka gani!
Za kipepo? Nini maana ya hell na kutaja majina ya walozi hata maandiko yamesema nyakati za mwisho watatokea watu kama hawa na akatahadharisha kuweni waangalifu
 
Biblia inasema zipimeni roho kama zatoka kwa Bwana au la Maana hata wajumbe wa shetani hufanya miujiza pia , lakini pia niwashauri kuwa kuna ulimwengu wa roho ulimwengu wa roho una pande mbili , upande wa Mungu aliyeumba Mbingu na nchi na upande wa shetani hapa lazima uwe mwanachama katika upande mmoja tu. Walioko upande wa shetani hupenda kuigiza kwamba ni watumishi wa Mungu ukitaka kujua kwamba mtumishi aliyepo mbele yako ni wa upande gani 1. Mtumishi wa Mungu aliyehai kumuona ni bure kabisa hakuna fedha yoyote utakayotakiwa kutoa 2. Mtumishi wa Mungu yoyote Shauku yake kubwa ni kuona watu wanaokolewa kila baada ya kufanya mkutano ataita watu waokoke. 3 Mtumishi wa Mungu yoyote haelezei mambo ya kichawi awapo madhabahuni bali humtukuza Mungu
4. Mungu hazoeleki kama anataka kukuponya hawezi kutumia njia moja wengi manabii wanatumia mafuta Mafuta mengi hutoka kuzimu , ikumbukwe kuwa Mafuta kwa mfalme Daudi yalitumika kwa sababu aliandaliwa kuwa mtawala , inashangaza kuona siku hizi kwenye maombi ya manabii hutumia mafuta, hata kama kusoma hujui itoshe tu ujue Watumishi wengi sio wa Mungu ni kutoka kuzimu.

5 . pia ukimuona mtumishi yoyote wa Mungu hana msaidizi katika huduma yake hamuachii mtumishi wa Mungu yoyote kanisa akisafiri anaweka kanda au hataki kusafiri , wandugu hayupo Mungu wa hivyo kumbuka Elisha na eliya, Musa na Joshua walikabidhiana kazi za utumishi kwa kufundishana na kuwa karibu , hii inaitwa on job training hata wanadam wanafanya hivyo sembuse Mungu wa miungu .
6. Pia suala la upako ambao unatoka kwa Mungu aliumba vyote ni kwamba unaongezeka kuanzia mwanzo mpaka mwisho unakua mwingi Mungu humuonyesha mwanadamu huduma yake akitonyesha mwisho akitokea mwanzo hii ndio tabia ya Mungu aliyeumba wanadamu kwa hiyo huwezi kukuta mtu from know where akawa na upako mwingi na hauongezeki , na staili yake ya kuombea lazima awawekee mkono kila siku pana shida , anaChokiongea huwa hafikirii anaropoka tu ujue pana shida kwa mtu huyo .
Nimeamua niwaandikie mabo machache yatayowapa picha ya kujua mtumishi gani ni wa Mungu na yupi sio wa Mungu sitaji mtu ila pimeni wenyewe , "Wanadamu yafuateni haya kwa umakini mkubwa maana wajumbe wa shetani wapo wachungaji wanamapepo ambayohufanya kama vile Mungu aponyavyo , Msiwe wabishi kwakuwa mliwahi kwenda mkaponywa Shida zenu , ila kumbukeni Mtaikosa Mbingu pia Mtakosa kutembea na Mungu huku Duniani , mtapata na Laana kwa Mungu yote hufunguliwa kwa pamoja . Nimalizie kwa kusema Mungu yupo mtafuteni kwa Bidii hakika mtamuona mwaka 2017 ni mwaka wa kuwatambua watumishi waongo na wakimbieni maana Mungu anawaumbua watu hao mwaka huu. Mungu awabariki katika kristo Yesu
 
Back
Top Bottom