Nabii Frank Julius Kilawah mnamsoma?!

Nabii Frank Julius Kilawah mnamsoma?!

Hata mimi nimemshuhudia channel ten ila hana tofauti na wengine kama akina Gwajima,Dr Geo Davie nabii mkuu,Kakobe,Mwingira,mzee wa Upako n.k
Imani yako ndio itakuponya na sio kufuata mkumbo
Amini ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu baaasi na anaishi daima nasi,tuwe na imani naye.
Siku hizi hata wachawi wanafanya miujiza hivyo bila kuwa na imani dhabiti hutaweza kumtofautisha nabii wa kweli na nabii wa uwongo.
Omba neema ya Mwenyenzi Mungu ili uweze kuwatofautisha.
geordavie ni tatizo.
 
Kwahiyo watumishi wanao ombea watu afu hawaponi hao ndo watumishi wa kweli, ila wale wanao waombea watu uponyaji na wanapona hao ndo matapeli? Kama kweli Frank anafanya kazi za shetan basi Shetan ananguvu kumzidi Mungu. Eliya alisimama hadharani akasema naijulikane leo, sasa mbona nyie mnamponda huku mmefichama? Jitokezeni hadharani nanyie ili tijue uwezo wa Mungu wenu!
 
Usanii tu kama wa babu wa kikombe. Mimi mpaka leo nahangaika kutafuta mtu anayee ishi ambaye alifufuliwa na mzee wa ufufuko na uzima sijampata
 
Ndio wapiga DILI hao...Mr Magu anapiga nao kelele kila kukicha...
Na hawaishi leo wala kesho kwani Dar ndio KICHAKA cha Wajinga....

Hao watu WANAIGIZA TU.....hakuna swala la UPONYAJI hapo....elewa wajinga ndio waliwao....

Kama unaamini hayo tafuta mtu yeyote unaemjua wewe ana ULEMAVU na anatembelea Magongo mpeleke huko uone kama atarudi anatembea....

Kama vipi NABII Frank angekwenda kwenye Mahospitali huko ndio kwenye watu wanao hitaji kuponywa....

MJINI HAPAA....AKILI KUMKICHWA....
 
Hii hoja ya kusema kama Frenk anaponya kweli basi aende maospitalini waliko wagonjwa, siiungi mkono hata kidogo kwasababu hata Yesu mwenyewe hakuwafata wagonjwa majumbani wala mahospitalin Bali wote walio letwa kwake walipona. Tena wengine waliulizwa maswali ambayo kama ungeulizwa wewe ungesema Yesu anadharau, lakin walijibu kwa imani na wakapokea uponyaji. Nakama wanao ponywa hamuwajui, basi tafuteni wagonjwa mnao wafahamu then muwapeleke ila msisahau kutupa mrejesho.
 
Kwahiyo watumishi wanao ombea watu afu hawaponi hao ndo watumishi wa kweli, ila wale wanao waombea watu uponyaji na wanapona hao ndo matapeli? Kama kweli Frank anafanya kazi za shetan basi Shetan ananguvu kumzidi Mungu. Eliya alisimama hadharani akasema naijulikane leo, sasa mbona nyie mnamponda huku mmefichama? Jitokezeni hadharani nanyie ili tijue uwezo wa Mungu wenu!

Watumishi kitu gani . Kuna watumishi sikuizi. Nani kawateua kupitia wapi kwa ishara gani. Au mtu anaamka tuu asubuhi kakariri mistari kadhaa tayari mtumishi. Hao anaowaponya mbona hawajulikani wametoka wapi wa wapi hawajulikani. Hakuna address hata ya mmoja tuka cross check tujiridhishe
Watu wanatoka kwa waganga wa kienyeji wanaamua kubadili mbinu ya kupiga ramli wanatumia mfumo mwingine halafu mnaenda kujaa huko kisa mnataka Mungu wa muujiza. Lakini hampendi kuambiwa acheni dhambi hamtaki mnataka muambiwe kesho unapata ajira kaesho unapata mume kesho unapata kununua hari kesho biashara yako inainuka nk.
Hamtaki injili inayochoma hamtaki maelekezo mnatamani muujiza kila ibada.
Hebu niambie Daudi au Suleyman walimponya nani mgonjwa. Je hapakuwa na wagonjwa ??
 
Daudi na mwanae yaani Solomon hawakua na upako wa ki-nabii. Hawa wote walikua ni wafalme. Ila ktk hizo nyakati biblia inamtambulisha SAMWELI kama NABII. Sasa kwakua tuna mjadili Frank kama NABII basi tumlinganishe na NABII mwenzake SAMWELI. Sasa ukifatilia mambo aliyo yafanya Mungu kwa mkono wa SAMWELI, yangetokea leo hii, watu wangesema SAMWELI ni mganga wa kienyeji au Freemason.Habari hizi zinapatikana ktk kitabu cha 1samw.Kitu cha msingi tunacho paswa kujiuliza ni kwamba, Kama Nabii Frank ni nabii wa uongo, ni nani basi ambae ni NABII wa kweli? Maana Bwana asema, "akiwepo NABII kati yenu, Mimi Mungu nitasema nae."Yuko wapi huyo? mtaje ili nae tumchunguze.
 
Mungu nisaidie kuamini kama kweli umewapa watu wako uwezo wa kufanya mambo makubwa kiasi hiki. Nimeshuhudia semina za Prophet Frank kupitia Chanel 10 na Star TV.Daah jamaa ana upako wa kutisha,anaponya within a minute.Kina bibi wanatupa magongo within a minute.Kama Yesu karudi vile.Kinachovutia zaidi ni kutoa historia ya matatizo ya watu katika namna ya kipekee.Kwamba "wewe ulilogwa na fulani,mahali fulani,kwa sababu fulani". Anatoa mfano wa kukausha kidonda cha mtu ndani ya dakika 3.Jamani mnamsomaje huyu jamaa
na wewe umeamini?unadhani nani hajui kua yale na maigizo angekwenda nani hospital akalipe mahela kibao wakati pale ni bure na unapona saa hiyohiyo
 
Ananisikitisha sana anachonganisha hadi ndugu, alimwambia mama mmoja kwenye mkutano mbeya, Eti tatizo linalomsumbua mwanae mume wake ndio kafanya ushirikina loh!!! mama akamwambia mume wangu alishakufa siku nyingi sana, aliona aibu akaanza kujibalaguza eti oohh!! alifanya hivo kabla hajafa, mweee!!! wakati ukiangalia mtoto ana mtindio wa ubongo.
 
Back
Top Bottom