Wakuu,
JANA, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Kamati za Bunge za Hesabu Barani Afrika (AFROPAC) katika mkutano uliofanyika jijini Lusaka, Zambia.
Huu ni umoja mchanga kabisa ambao ndiyo uko katika mwaka wake wa kwanza. Kimsingi, uteuzi huu wa Zitto unamaanisha kwamba yeye ndiye atakuwa msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku za umoja huu mpya.
Atakuwa kiongozi wa Sekretarieti ya AFROPAC na hivyo atakuwa anasimamia waajiriwa wote wa umoja huo kwa sasa. Hii maana yake ni kwamba Watanzania watapata nafasi zaidi za kuajiriwa.
Ndiyo maana, nafasi hii ilikuwa ikiwaniwa na wabunge wengi kutoka katika mabunge mengine barani Afrika. Kwenye umoja kama AFROPAC, nafasi ya Mkuu wa Sekretarieti huwa na faida kwa wananchi wa nchi anayotoka Katibu Mkuu.
Huu si uteuzi wa kwanza wa Zitto ambao unaonyesha heshima anayopewa nje ya nchi. Ni Zitto huyuhuyu ambaye miaka michache iliyopita aliteuliwa na aliyekuwa Rais wa Ujerumani, Horst Kohler, kuwa mmoja wa viongozi vijana wanaochipukia barani Afrika chini ya mpango uliofahamika kwa jina la Africa Initiative.
Katika bara zima la Afrika, serikali ya Ujerumani iliteua vijana takribani 40 tu ambao walionekana kuwa tumaini la bara hili katika miaka ijayo.
Katika kitabu cha Global Corruption, Mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Masuala ya Rushwa ya Transparency International (TI), Laurence Cockcroft, alimueleza Zitto kama kiongozi "makini, mwenye uelewa mpana na mpambanaji wa rushwa."
Ni Zitto ambaye amechochea vijana wengi kujiunga na siasa katika miaka ya karibuni. Miaka kumi iliyopita, Bunge lilikuwa ni taasisi ya wastaafu na wateule wachache waliodumu kwa miaka mingi.
Ni Zitto ambaye uwepo wake na ujengaji wake wa hoja ulifichua nguvu na upya ambao taasisi hiyo ilikuwa inatakiwa kuwa nao. Kama utaongea na wabunge vijana walioingia bungeni katika Uchaguz uliopita, nusu watakwambia kwamba Mbunge huyu wa Kigoma Kaskazini ndiye aliyewashawishikufuata njia hiyo ya uanasiasa.
[03:40, 14/05/2014] ZITTO KABWE: Mwanasiasa huyu ni mtoto wa familia isiyo ya kitajiri wala yenye historia yoyote na Tanzania. Ni Zitto Kabwe ndiye aliyewaonyesha watu kwamba unaweza kuwa mtoto wa masikini na usiye na uhusiano wowote wa damu au uswahiba na familia tajiri na bado ukawa na fursa.
Na tangu ameingia bungeni, Mbunge huyu amekuwa nyuma ya karibu matukio yote makubwa ambayo yametokea bungeni katika miaka ya karibuni.
Yeye ndiye aliyeibua suala la Buzwagi ambalo leo limetupa Sheria Mpya ya Madini ambayo walau ina manufaa kwa wananchi kuliko sheria iliyokuwepo kabla hajaingia bungeni.
Zitto Kabwe ndiye aliyependekeza kwa serikali Waziri Sospeter Muhongo Mabadiliko ya Sheria katika Nishati ya Gesi ambayo leo yataiingizia serikali mabilioni ya fedha kila makampuni ya gesi yatakapokuwa yanauziana hisa yenyewe kwa yenyewe.
Kabla Zitto hajaingia bungeni, makampuni haya yalikuwa yakibadilisha majina au kuuziana hisa pasipo Tanzania kufaidika na lolote. Nchi hii imepoteza mabilioni ya shilingi kwa mtindo huu.
Leo hii, Mbunge huyu anafuatilia Ufisadi katika Ulipaji wa Kodi unaofanywa na Makampuni Makubwa si Tanzania pekee bali barani Afrika kwa ujumla.
Makampuni haya yanakwepa kulipa kodi au kulipa kodi kidogo kwa serikali kwa kutumia njia ambazo zilikuwa hazijabainika huko nyuma. Kama serikali itaanza kukusanya kodi yake stahili na kuzuia ukwepaji huo wa kodi, Zitto atakuwa amesaidia katika hilo.
Kodi hii ndiyo ambayo itasaidia kununua dawa katika hospitali zetu, madawati katika shule zetu, kuzuia vifo vya akinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kujenga barabara na miundombinu mingine.
Mara zote, Zitto amefanya haya pasipo kutukana wala kugombana na watu. Siku zote amekuwa ni mtu wa kujenga hoja na amekuwa na marafiki karibu katika vyama vyote ambavyo viko hapa nchini.
Ni vigumu, vigumu sana kumlinganisha Zitto na Mbunge yeyote kijana katika Bunge la sasa… Binafsi, naamini kwamba huyu ndiye Mbunge wa muhimu zaidi kuliko wabunge wengine wote waliopo katika Bunge la Tanzania.
Na hii ni kwa sababu ya rekodi zake nilizotaja hapo juu. Badala ya kubishana kuhusu umuhimu wake, ni vema watu wakakumbushana na kueleza ni mbunge yupi amekuwa na mchango mkubwa bungeni kuliko huyu wa CHADEMA.