Nabii asiekubalika nyumbani

Nabii asiekubalika nyumbani

mucho886

Senior Member
Joined
Dec 1, 2013
Posts
169
Reaction score
41
Zitto Kabwe; Nabii asiyekubalika nyumbani?

Ezekiel Kamwaga

JANA, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Kamati za Bunge za Hesabu Barani Afrika (AFROPAC) katika mkutano uliofanyika jijini Lusaka, Zambia.

Huu ni umoja mchanga kabisa ambao ndiyo uko katika mwaka wake wa kwanza. Kimsingi, uteuzi huu wa Zitto unamaanisha kwamba yeye ndiye atakuwa msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku za umoja huu mpya.

Atakuwa kiongozi wa Sekretarieti ya AFROPAC na hivyo atakuwa anasimamia waajiriwa wote wa umoja huo kwa sasa. Hii maana yake ni kwamba Watanzania watapata nafasi zaidi za kuajiriwa.

Ndiyo maana, nafasi hii ilikuwa ikiwaniwa na wabunge wengi kutoka katika mabunge mengine barani Afrika. Kwenye umoja kama AFROPAC, nafasi ya Mkuu wa Sekretarieti huwa na faida kwa wananchi wa nchi anayotoka Katibu Mkuu.

Huu si uteuzi wa kwanza wa Zitto ambao unaonyesha heshima anayopewa nje ya nchi. Ni Zitto huyuhuyu ambaye miaka michache iliyopita aliteuliwa na aliyekuwa Rais wa Ujerumani, Horst Kohler, kuwa mmoja wa viongozi vijana wanaochipukia barani Afrika chini ya mpango uliofahamika kwa jina la Africa Initiative.

Katika bara zima la Afrika, serikali ya Ujerumani iliteua vijana takribani 40 tu ambao walionekana kuwa tumaini la bara hili katika miaka ijayo.

Katika kitabu cha Global Corruption, Mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Masuala ya Rushwa ya Transparency International (TI), Laurence Cockcroft, alimueleza Zitto kama kiongozi “makini, mwenye uelewa mpana na mpambanaji wa rushwa.”

Ni Zitto ambaye amechochea vijana wengi kujiunga na siasa katika miaka ya karibuni. Miaka kumi iliyopita, Bunge lilikuwa ni taasisi ya wastaafu na wateule wachache waliodumu kwa miaka mingi.

Ni Zitto ambaye uwepo wake na ujengaji wake wa hoja ulifichua nguvu na upya ambao taasisi hiyo ilikuwa inatakiwa kuwa nao. Kama utaongea na wabunge vijana walioingia bungeni katika Uchaguz uliopita, nusu watakwambia kwamba Mbunge huyu wa Kigoma Kaskazini ndiye aliyewashawishi kufuata njia hiyo ya uanasiasa.

Mwanasiasa huyu ni mtoto wa familia isiyo ya kitajiri wala yenye historia yoyote na Tanzania. Ni Zitto Kabwe ndiye aliyewaonyesha watu kwamba unaweza kuwa mtoto wa masikini na usiye na uhusiano wowote wa damu au uswahiba na familia tajiri na bado ukawa na fursa.

Na tangu ameingia bungeni, Mbunge huyu amekuwa nyuma ya karibu matukio yote makubwa ambayo yametokea bungeni katika miaka ya karibuni.

Yeye ndiye aliyeibua suala la Buzwagi ambalo leo limetupa Sheria Mpya ya Madini ambayo walau ina manufaa kwa wananchi kuliko sheria iliyokuwepo kabla hajaingia bungeni.

Zitto Kabwe ndiye aliyependekeza kwa serikali Waziri Sospeter Muhongo Mabadiliko ya Sheria katika Nishati ya Gesi ambayo leo yataiingizia serikali mabilioni ya fedha kila makampuni ya gesi yatakapokuwa yanauziana hisa yenyewe kwa yenyewe.

Kabla Zitto hajaingia bungeni, makampuni haya yalikuwa yakibadilisha majina au kuuziana hisa pasipo Tanzania kufaidika na lolote. Nchi hii imepoteza mabilioni ya shilingi kwa mtindo huu.

Leo hii, Mbunge huyu anafuatilia Ufisadi katika Ulipaji wa Kodi unaofanywa na Makampuni Makubwa si Tanzania pekee bali barani Afrika kwa ujumla.

Makampuni haya yanakwepa kulipa kodi au kulipa kodi kidogo kwa serikali kwa kutumia njia ambazo zilikuwa hazijabainika huko nyuma. Kama serikali itaanza kukusanya kodi yake stahili na kuzuia ukwepaji huo wa kodi, Zitto atakuwa amesaidia katika hilo.

Kodi hii ndiyo ambayo itasaidia kununua dawa katika hospitali zetu, madawati katika shule zetu, kuzuia vifo vya akinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kujenga barabara na miundombinu mingine.

Mara zote, Zitto amefanya haya pasipo kutukana wala kugombana na watu. Siku zote amekuwa ni mtu wa kujenga hoja na amekuwa na marafiki karibu katika vyama vyote ambavyo viko hapa nchini.

Ni vigumu, vigumu sana kumlinganisha Zitto na Mbunge yeyote kijana katika Bunge la sasa… Binafsi, naamini kwamba huyu ndiye Mbunge wa muhimu zaidi kuliko wabunge wengine wote waliopo katika Bunge la Tanzania.

Na hii ni kwa sababu ya rekodi zake nilizotaja hapo juu. Badala ya kubishana kuhusu umuhimu wake, ni vema watu wakakumbushana na kueleza ni mbunge yupi amekuwa na mchango mkubwa bungeni kuliko huyu wa CHADEMA.

Kuna wabunge ambao wanazungumza mara kwa mara bungeni lakini baada ya siku tatu hakuna watu wanachokumbuka kuhusu hoja zao. Kuna wabunge ambao watakumbukwa zaidi kwa kupigwa na askari, kutoka nje ya Bunge, kutukana watu kwenye mitandao ya kijamii na kutoa maneno ya kashfa bungeni.

Kuna wabunge ambao watakumbukwa pia kwa kuwa mstari wa mbele kumkashifu na kumponda Zitto Kabwe. Tatizo ni kwamba, hakuna mwanasiasa atakayefanikiwa kwa siasa za namna hii ambazo hazisaidii Taifa.

MTU WA KITAIFA NA KIMATAIFA

Hakuna mwanasiasa wa upinzani hapa Tanzania ambaye ana uhusiano mzuri kimataifa na pia ana heshima miongoni mwa taasisi za dola pamoja na waasisi wa Taifa kuliko Zitto.

Kuna mwanasiasa gani hapa nchini ambaye ana uhusiano wa karibu na Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Dk. Mahathir Mohamed, kuliko Zitto?

Mahathir ni mwanasiasa muhimu kwa vile ndiye aliyeibadilisha nchi yake kutoka kuwa masikini na kuwa na uchumi wa kati. Zitto alimtafuta huyu kwa vile anatafuta namna ya kuikwamua Tanzania kutoka hapa ilipo sasa.

Zitto ni rafiki wa Raila Odinga. Zitto ni rafiki wa familia ya Mwanamapinduzi wa Msumbiji, Hayati Eduardo Chivambo Mondlane. Zitto ni mtu wa karibu na familia ya Mzee Keneth Kaunda kiasi kwamba majuzi alikwenda kumtembelea nyumbani kwake wakati Rais huyo wa zamani wa Zambia alipokuwa akiugua.

Inawezekanaje kwa mwanasiasa wa kawaida na mbinafsi (kama ambavyo Watanzania wanaaminishwa na baadhi ya wanasiasa), awe na ushawishi wa namna hii ambao hakuna mwingine wa umri wake anao?

Kama kijana, nafikiri ni muhimu kwa vijana wenzangu kuanza kumtazama Zitto kama mmoja wa wanasiasa muhimu katika kizazi chetu.

Ni rahisi sana kuingia katika mkumbo wa kusikiliza propaganda za watu ambao kwa sababu zao binafsi hawataki kukubaliana na ukweli huu au wameamua kupambana na ukweli huu kwa gharama yoyote.

Kama Afrika nzima inaona kwamba Zitto anafaa kuwa kiongozi mwandamizi wa taasisi inayoshikilia kupambana na ufisadi katika matumizi ya fedha za umma, iweje leo aonekane mbaya na mbovu kabisa hapa kwetu?

Anachohitaji Zitto Zuberi Kabwe (ZZK) ni kitu kimoja; Heshima.

Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kukubali kwamba katika safari yake ya kisiasa, ZZK amefanya makosa mengi humo njiani.

Lakini, binadamu wanahitaji kuongozwa na mmoja wao. Anayekosea kama wao, anayeumia kama wao, anayecheka kama wao na anayejua mahitaji na matakwa yao.

Mimi ni Mkristo na katika kitabu cha Samweli nakumbuka Wana wa Israel walimwambia Mungu kwamba wamechoka kuongozwa na Mitume na wanataka kuongozwa na mmoja wao.

Hapo ndipo Mwenyezi Mungu alipomteua Sauli….na baadaye Daudi na kasha Suleiman. Na wote walifanya makosa yao katika uongozi wao.

Zitto Kabwe alikosea na atazidi kukosea katika miaka inayokuja. Si kwa sababu anataka lakini kwa sababu ni mwanadamu kama sisi na sote tu wakosaji.

Lakini, kwangu atazidi kuwa mwanasiasa wa kipekee katika kizazi chetu. Nitachukia kama mwisho wake utakuwa sawa na kisa cha Nabii asiyekubalika kwao.

Zitto Kabwe ni wetu. Tumsaidie kwa vile kwa kizazi chetu cha vijana wa sasa, yeye ni maalumu…. Wa kipekee, Zitto.

Zitto Kabwe. Zahoro Muhaji Vicent Kassala Joseph Peter Joseph Peter Kibatala Lutengano Mwalwiba Zitto Z Kabwe
 
Mkono atoboa siri za Zitto
Posted Jumanne,Januari7 2014 saa 24:0 AM
. Nissan Patrol, Mkono alisema lilikodishwa kwa Zitto na mpaka sasa bado analipa gharama za kulikodisha...
“Hata nyaraka za umiliki wa gari hili ninazo mimi mwenyewe kama mmiliki halali. Ninamiliki magari mengi tu hata wewe mwandishi ukitaka Vogue (aina ya gari) nitakukodisha tu,” alisema Mkono.
Zitto, mchana anamtuhumu Mkono kuwa fisadi, jioni anaenda kukodi gari kwake!
>> Hivi tangu 2008 mpaka sasa 2014, huyu "MZALENDO wenu ZITTO" kalipa kodi ya kukodi gari kwa NIMRODI MKONO kiasi gani?
 
Wazalendo wa Kitanzania tunamkubali sana Zitto Kabwe! Akina Mbowe na wafuasi wake ndio wanampiga vita!

Sura ya Zitto ndani ya Chama!
Tangu mwaka 2008 mwenendo wa kisiasa wa Zitto Zuber Kabwe ulianza kutiliwa shaka na wanachama wa CHADEMA ndani na nje ya chama, Hili lilipelekea kuibuka maneno ya chini kwa chini kuwa anakisaliti chama.
Uchunguzi umezidi kubaini kuwa kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2011, kutoka kuugwa mkono na wanachadema kama mwanasiasa makini, Zitto aliamua kuunda kundi la uasi ndani ya chama.
Baada ya kujiridhisha kuwa Zitto Zuber Kabwe Mbunge wa Chadema na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, ameasi Chama na ameunda kundi ndani ya chama linaloendesha vuguvugu la mapinduzi kwa viongozi halali wa chama kwa ufadhiri wa chama tawala ccm, ikiwa ni kinyume cha katiba na itifaki za chama
 
Zitto Kabwe; Nabii asiyekubalika nyumbani?
Ezekiel Kamwaga
Katika kitabu cha Global Corruption, Mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Masuala ya Rushwa ya Transparency International (TI), Laurence Cockcroft, alimueleza Zitto kama kiongozi "makini, mwenye uelewa mpana na mpambanaji wa rushwa."
Tangu lini kawa mpambanaji? Hana mabilioni USWISI? Ujerumani je?
 
Mabilioni ujerumani? Uswiss au ulimuwekea. Zitto ni genious ni mwanasiasa hodari, anakubarika kama wew hujamuelewa hutakuja kamwe kumuelewa
 
Kama kijana, nafikiri ni muhimu kwa vijana wenzangu kuanza kumtazama Zitto kama mmoja wa wanasiasa muhimu katika kizazi chetu.
Zitto Kabwe ni wetu. Tumsaidie kwa vile kwa kizazi chetu cha vijana wa sasa, yeye ni maalumu…. Wa kipekee, Zitto.
Ezekiel Kamwaga, hivi wewe bado ni kijana? Hivi Zitto bado ni kijana!..
 
Zitto Kabwe; Nabii asiyekubalika nyumbani?

Ezekiel Kamwaga

JANA, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Kamati za Bunge za Hesabu Barani Afrika (AFROPAC) katika mkutano uliofanyika jijini Lusaka, Zambia.

Huu ni umoja mchanga kabisa ambao ndiyo uko katika mwaka wake wa kwanza. Kimsingi, uteuzi huu wa Zitto unamaanisha kwamba yeye ndiye atakuwa msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku za umoja huu mpya.

Atakuwa kiongozi wa Sekretarieti ya AFROPAC na hivyo atakuwa anasimamia waajiriwa wote wa umoja huo kwa sasa. Hii maana yake ni kwamba Watanzania watapata nafasi zaidi za kuajiriwa.

Ndiyo maana, nafasi hii ilikuwa ikiwaniwa na wabunge wengi kutoka katika mabunge mengine barani Afrika. Kwenye umoja kama AFROPAC, nafasi ya Mkuu wa Sekretarieti huwa na faida kwa wananchi wa nchi anayotoka Katibu Mkuu.

Huu si uteuzi wa kwanza wa Zitto ambao unaonyesha heshima anayopewa nje ya nchi. Ni Zitto huyuhuyu ambaye miaka michache iliyopita aliteuliwa na aliyekuwa Rais wa Ujerumani, Horst Kohler, kuwa mmoja wa viongozi vijana wanaochipukia barani Afrika chini ya mpango uliofahamika kwa jina la Africa Initiative.

Katika bara zima la Afrika, serikali ya Ujerumani iliteua vijana takribani 40 tu ambao walionekana kuwa tumaini la bara hili katika miaka ijayo.

Katika kitabu cha Global Corruption, Mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Masuala ya Rushwa ya Transparency International (TI), Laurence Cockcroft, alimueleza Zitto kama kiongozi “makini, mwenye uelewa mpana na mpambanaji wa rushwa.”

Ni Zitto ambaye amechochea vijana wengi kujiunga na siasa katika miaka ya karibuni. Miaka kumi iliyopita, Bunge lilikuwa ni taasisi ya wastaafu na wateule wachache waliodumu kwa miaka mingi.

Ni Zitto ambaye uwepo wake na ujengaji wake wa hoja ulifichua nguvu na upya ambao taasisi hiyo ilikuwa inatakiwa kuwa nao. Kama utaongea na wabunge vijana walioingia bungeni katika Uchaguz uliopita, nusu watakwambia kwamba Mbunge huyu wa Kigoma Kaskazini ndiye aliyewashawishi kufuata njia hiyo ya uanasiasa.

Mwanasiasa huyu ni mtoto wa familia isiyo ya kitajiri wala yenye historia yoyote na Tanzania. Ni Zitto Kabwe ndiye aliyewaonyesha watu kwamba unaweza kuwa mtoto wa masikini na usiye na uhusiano wowote wa damu au uswahiba na familia tajiri na bado ukawa na fursa.

Na tangu ameingia bungeni, Mbunge huyu amekuwa nyuma ya karibu matukio yote makubwa ambayo yametokea bungeni katika miaka ya karibuni.

Yeye ndiye aliyeibua suala la Buzwagi ambalo leo limetupa Sheria Mpya ya Madini ambayo walau ina manufaa kwa wananchi kuliko sheria iliyokuwepo kabla hajaingia bungeni.

Zitto Kabwe ndiye aliyependekeza kwa serikali Waziri Sospeter Muhongo Mabadiliko ya Sheria katika Nishati ya Gesi ambayo leo yataiingizia serikali mabilioni ya fedha kila makampuni ya gesi yatakapokuwa yanauziana hisa yenyewe kwa yenyewe.

Kabla Zitto hajaingia bungeni, makampuni haya yalikuwa yakibadilisha majina au kuuziana hisa pasipo Tanzania kufaidika na lolote. Nchi hii imepoteza mabilioni ya shilingi kwa mtindo huu.

Leo hii, Mbunge huyu anafuatilia Ufisadi katika Ulipaji wa Kodi unaofanywa na Makampuni Makubwa si Tanzania pekee bali barani Afrika kwa ujumla.

Makampuni haya yanakwepa kulipa kodi au kulipa kodi kidogo kwa serikali kwa kutumia njia ambazo zilikuwa hazijabainika huko nyuma. Kama serikali itaanza kukusanya kodi yake stahili na kuzuia ukwepaji huo wa kodi, Zitto atakuwa amesaidia katika hilo.

Kodi hii ndiyo ambayo itasaidia kununua dawa katika hospitali zetu, madawati katika shule zetu, kuzuia vifo vya akinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kujenga barabara na miundombinu mingine.

Mara zote, Zitto amefanya haya pasipo kutukana wala kugombana na watu. Siku zote amekuwa ni mtu wa kujenga hoja na amekuwa na marafiki karibu katika vyama vyote ambavyo viko hapa nchini.

Ni vigumu, vigumu sana kumlinganisha Zitto na Mbunge yeyote kijana katika Bunge la sasa… Binafsi, naamini kwamba huyu ndiye Mbunge wa muhimu zaidi kuliko wabunge wengine wote waliopo katika Bunge la Tanzania.

Na hii ni kwa sababu ya rekodi zake nilizotaja hapo juu. Badala ya kubishana kuhusu umuhimu wake, ni vema watu wakakumbushana na kueleza ni mbunge yupi amekuwa na mchango mkubwa bungeni kuliko huyu wa CHADEMA.

Kuna wabunge ambao wanazungumza mara kwa mara bungeni lakini baada ya siku tatu hakuna watu wanachokumbuka kuhusu hoja zao. Kuna wabunge ambao watakumbukwa zaidi kwa kupigwa na askari, kutoka nje ya Bunge, kutukana watu kwenye mitandao ya kijamii na kutoa maneno ya kashfa bungeni.

Kuna wabunge ambao watakumbukwa pia kwa kuwa mstari wa mbele kumkashifu na kumponda Zitto Kabwe. Tatizo ni kwamba, hakuna mwanasiasa atakayefanikiwa kwa siasa za namna hii ambazo hazisaidii Taifa.

MTU WA KITAIFA NA KIMATAIFA

Hakuna mwanasiasa wa upinzani hapa Tanzania ambaye ana uhusiano mzuri kimataifa na pia ana heshima miongoni mwa taasisi za dola pamoja na waasisi wa Taifa kuliko Zitto.

Kuna mwanasiasa gani hapa nchini ambaye ana uhusiano wa karibu na Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Dk. Mahathir Mohamed, kuliko Zitto?

Mahathir ni mwanasiasa muhimu kwa vile ndiye aliyeibadilisha nchi yake kutoka kuwa masikini na kuwa na uchumi wa kati. Zitto alimtafuta huyu kwa vile anatafuta namna ya kuikwamua Tanzania kutoka hapa ilipo sasa.

Zitto ni rafiki wa Raila Odinga. Zitto ni rafiki wa familia ya Mwanamapinduzi wa Msumbiji, Hayati Eduardo Chivambo Mondlane. Zitto ni mtu wa karibu na familia ya Mzee Keneth Kaunda kiasi kwamba majuzi alikwenda kumtembelea nyumbani kwake wakati Rais huyo wa zamani wa Zambia alipokuwa akiugua.

Inawezekanaje kwa mwanasiasa wa kawaida na mbinafsi (kama ambavyo Watanzania wanaaminishwa na baadhi ya wanasiasa), awe na ushawishi wa namna hii ambao hakuna mwingine wa umri wake anao?

Kama kijana, nafikiri ni muhimu kwa vijana wenzangu kuanza kumtazama Zitto kama mmoja wa wanasiasa muhimu katika kizazi chetu.

Ni rahisi sana kuingia katika mkumbo wa kusikiliza propaganda za watu ambao kwa sababu zao binafsi hawataki kukubaliana na ukweli huu au wameamua kupambana na ukweli huu kwa gharama yoyote.

Kama Afrika nzima inaona kwamba Zitto anafaa kuwa kiongozi mwandamizi wa taasisi inayoshikilia kupambana na ufisadi katika matumizi ya fedha za umma, iweje leo aonekane mbaya na mbovu kabisa hapa kwetu?

Anachohitaji Zitto Zuberi Kabwe (ZZK) ni kitu kimoja; Heshima.

Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kukubali kwamba katika safari yake ya kisiasa, ZZK amefanya makosa mengi humo njiani.

Lakini, binadamu wanahitaji kuongozwa na mmoja wao. Anayekosea kama wao, anayeumia kama wao, anayecheka kama wao na anayejua mahitaji na matakwa yao.

Mimi ni Mkristo na katika kitabu cha Samweli nakumbuka Wana wa Israel walimwambia Mungu kwamba wamechoka kuongozwa na Mitume na wanataka kuongozwa na mmoja wao.

Hapo ndipo Mwenyezi Mungu alipomteua Sauli….na baadaye Daudi na kasha Suleiman. Na wote walifanya makosa yao katika uongozi wao.

Zitto Kabwe alikosea na atazidi kukosea katika miaka inayokuja. Si kwa sababu anataka lakini kwa sababu ni mwanadamu kama sisi na sote tu wakosaji.

Lakini, kwangu atazidi kuwa mwanasiasa wa kipekee katika kizazi chetu. Nitachukia kama mwisho wake utakuwa sawa na kisa cha Nabii asiyekubalika kwao.

Zitto Kabwe ni wetu. Tumsaidie kwa vile kwa kizazi chetu cha vijana wa sasa, yeye ni maalumu…. Wa kipekee, Zitto.

Zitto Kabwe. Zahoro Muhaji Vicent Kassala Joseph Peter Joseph Peter Kibatala Lutengano Mwalwiba Zitto Z Kabwe

Kuchaguliwa na vi organization vya Afrika wala usione unabii.

Mama Getrude Mongella alichaguliwa kuwa rais wa bunge la Africa akaenda kututia aibu huko kwa kujionyesha hana integrity kwa matumizi mabaya ya fedha za AU.

Wanasiasa wa uhakika hawasifiwi kwa wingi ama ufahari wa marafiki, bali kwa kazi walizozifanya. Huyo Zitto mikwala yake ya kuwataja walioficha fedha Uswizi imeishia wapi?

Sema jingine.
 
Mabilioni ujerumani? Uswiss au ulimuwekea. Zitto ni genious ni mwanasiasa hodari, anakubarika kama wew hujamuelewa hutakuja kamwe kumuelewa
Mkakati wa Zitto, kitila na Mwigamba ni huu!
....tutahakikisha kila post ya kumchafua inapatiwa majibu bila kutumia ID yake inayojulikana. Ni vema aidha akatupatia majibu na sisi kuyapost ama afungue ID mpya kabisa ambazo hazijawahi kuwepo kwenye mitandao halafu ndo awe anazitumia kujibu lakini kwa kuzingatia tuliyokwishayazungumza hapo juu yaani kutofanya kwa emotion na kuepuka jazba lakini pia kushauriana na watu wa karibu kabla ya kutoa majibu kwa jambo lolote linalomhusu.

Hivyo hapa tunajibizana na Zitto na timu yake!.
 
ZITTO KUITWA NA KAMATI MAALUMU YA UCHUNGUZI WA MABILIONI YA NJE.
TAREHE KAMATI MAELEZO YA ZITTO
28/02/2013 Aliitwa na kamati ya kufuatilia fedha za Uswiss katika ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali Dodoma. Alitoa taarifa kuwa anazo nyaraka zote zenye taarifa za walioficha fedha Uswis kwa majina na namba za account zao.
Pia alitoa masharti ya yeye kutoa ushahidi huo mbele ya kamati.
1. Kwanza asibugudhiwena mtu kwani taarifa alizonazo ni za siri.
2. Ahakikishiwe usalama wake kwa kuwa taarifa hizo ni nyeti sana.
20/03/2013 Kamati ilimwita Dar Es Salaam Alitoa udhuru kuwa yupo jeshini hivyo hawezi kufika mbele ya kamati kwa wakati huo.
22/03/2013 Kamati ilimfuata katika kambi ya jeshi Tanga kwa mahojiano nae. Katika majadiliano hakuweza kutoa majibu na kutaka wamwache hadi atakapo maliza mafunzo ya jeshi na kurejea ndipo atatoa huo ushahidi.
12/04/2013 Kamati ilimwita tena Dodoma kwa mahojiano. Alitoa udhuru kwa kusema anasafari ya kwenda Afrika Kusini.
14/05/2013 Kamati ilimwita tena Dodoma kwa mahojiano nae kupta ushahidi na majina aliyodai anayo. Hakufika mbele ya kamati na akasema,
1. Ana hoja yenye maslahi kwa taifa.
2. Kamati iliwasiliana naye akadai anajiandaa na mdahalo wa kigoda cha mwalimu Dar Es Salaam.
18/06/2013 Kamati ilimwita tena bila kuchoka Alitoa udhuru kuwa anafanya maandalizi ya timu ya Taifa kwenda AFCON kwa kuwa yeye yupo katika kamati ya maandalizi ya timu ya Taifa.
Kamati baada ya usumbufu wote huo ikaona ni vema kutumia njia mbadala ya kupata taarifa alizonazo ili kuiwezesha serikali kuchukua hatua.
Kamati ilimpa Mh Zitto Zuberi Kabwe hati ya kuitwa mbele ya kamati. Zitto kwa kuapa mbele ya kamati alisema,
Sina jina lelote wala akaunti ya mtu yeyote anaemiliki fedha Uswis.
12/12/2013 Zitto katika mchango wake alidai kwa nini hoja yake haisikilizwi na serikali ipo kimya huku yeye nayo majina
 
alisema hana majina yoyote ya wenye mabilioni ya uswisi - werema .

Kijana amekaa vizur katka ulingo huu,hongera sana ztto songa mbele,tumia kivuli cha taifa katka kufanya kaz
Kuhusu mapambano ya kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii:
Katika hili sisi hatukuona haja ya kufanya hivyo kwa sababu mbili:
Imani yetu kwamba taasisi yetu ni kubwa kuliko watu kwa hiyo ni muhimu kuzingatia kwamba hatuiui taasisi katika mapambano haya. Tukiendekeza mashambulizi kwa njia ya mitandao ya kijamii hatutakuwa na ngao ya kuwakinga watu wa kawaida (wanataasisi na wasio wanataasisi) dhidi ya kujikuta wakiamini kwamba taasisi hii nayo haina jipya ni sawa tu na ile tunayotaka kuitoa.
Tutakuwa tumeiua taasisi na mkakati huu hautakuwa na maana sana kama lengo ni kufanya mabadiliko ya uongozi wa taasisi tu lakini malengo ya taasisi ya mwaka 2015 yasitimie!
Kujikita kwenye mashambulizi kupitia mitandao ni kuzidi kuwashtua wakuu waliopo kwamba bado tuko serious na mkakati wa kuwatoa na kuwafanya wafanye kazi zaidi huku wakiendelea kumpaka matope MM kwamba ndiye anayerusha makombora hayo kwenye mitandao kwa kusudi la kuhujumu taasisi maana hiyo ndo lugha yao.
Hatukatai kwamba wakuu wanajua kabisa kwamba bado MM ana nia ya kumvaa mkuu aliyepo lakini tunajua kwamba kwa sasa wanaamini wamemdhoofisha na hana madhara tena. Ndiyo maana tunataka kutekeleza mkakati wetu kwa siri sana ili wafikiri MM amekata tamaa kumbe ndo anakuja na mkakati mzito zaidi.
Hata hivyo, ni muhimu kukumbushana kwamba wenzetu hawatanyamaza kwa sababu eti sisi tumeacha kuwashambulia kwenye mitandao ya kijamii. Lazima wataendelea! Wataendelea kumchafua MM kwa kupitia wapuuzi kama yule kichaa wa ‘ars' na kundi lake. Nini tutakuwa tunakifanya sasa? Tutahakikisha tuko busy kupost mambo mema na mazuri yatakayokuwa yakifanywa na MM kila wakati na kuzidi kusambaza sifa zake njema kila inapotokea nafasi. Atakayefanya kazi hiyo ni sisi wengine wala si yeye!
Pia tutahakikisha kila post ya kumchafua inapatiwa majibu bila kutumia ID yake inayojulikana. Ni vema aidha akatupatia majibu na sisi kuyapost ama afungue ID mpya kabisa ambazo hazijawahi kuwepo kwenye mitandao halafu ndo awe anazitumia kujibu lakini kwa kuzingatia tuliyokwishayazungumza hapo juu yaani kutofanya kwa emotion na kuepuka jazba lakini pia kushauriana na watu wa karibu kabla ya kutoa majibu kwa jambo lolote linalomhusu.
 
Back
Top Bottom