makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Nimekuwa nafuatilia vikao vya bunge kwa kipindi sana hasa katika bunge hili lililoanza mwaka 2010 ambalo limekuwa linakaribiana na changamoto kubwa nadhani kuliko mabunge yote yaliyowahi kutokea. Katika hali hii uongozi imara ni jambo kubwa kabisa lilikuwa linahitajika ambapo wote mtakuwa mashahidi kwamba ulionekana kutokuwepo katika vikao vya mwanzo vya bunge hili.
Hali naona kama imeanza kurekebika kidogo hasa kwa Naibu Spika ambaye naona kadri siku zinavyokwenda amekuwa akibadilika kwa mtazamo chanya kiasi cha kuanza kuaminiwa kwa uongozi wake. Napenda nikiri kwamba kwa Spika mwenyewe bado hajaonyesha hivyo na pia kwa wenyeviti (Hasa yule mwenyekiti ambaye mara zote akiongoza anaondoka na balaa)
Kwa ufupi napenda niseme kwamba naanza kumuamini naibu spika na nakuwa na imani ya kikao kwenda salama pale anapokuwa anaongoza bunge
Ni mtazamo wangu tu................
Mtazamo wako ni hasi+++++!
Hivi wewe unategemea mwanamme mzima anayeongozwa na mwanamke anaweza kuwa na maamuzi sahihi kweli???
Ndugai hana lolote wala chochote nim mbambaishaji mmoja tu kutoka Chama Cha Magamba aliyeukwa ulaji wa Uspika.
Jiulize ni kwanini swala la Posho linawatesa Wabunge wa CCM kwa sasa. Ndugai na Bibi yake Makinda walikubaliana kuwadanganya Wabunge kuwa Rais alikuwa amesha saini kibali cha kuruhusu ongezeko la Posho, kitu ambacho hakikuwa kweli!
Ndugai huyu huyu alienda kuropoka mbele ya vyombo vya habari kwamba NYONGEZA WATAKAYOLIPWA WABUNGE ilikuwa eti ni fedha kidogo sana ukilinganisha na malipo ya mihimili na taasisi zingine!
Hapa ndipo unaweza kugundua ukihiyo wa Ndugai kwa kutaka kutumia kigezo cha ofisi za watu wengine kama kigezo cha kuongezewa posho!!!
Narudia tena Ndugai na Bibi Anna Mikanda wameshindwa kuongoza Bunge.