Naamini kuna watu wamepitia haya maisha, Kama umepitia haya maisha sema chochote

yajutu

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
951
1,206
07b03ab0cbf7aa7366a73df283c1f467.jpg
 
Dogo yuko vizuri,
Hapo nilinunuliwa Raba made in Tanzania kutoka BORA,
Hapo nilikuwa natumia unga wa betri ule mweusi. Ile betri inaitwa National(Neshno) enzi hizo nabisha nasema ni (Nationali sio neshno kwa sababu hakuna S) kiingeleza tatizo la taifa. Tatizo ule unga mweusi kiatu ndani ya wiki kinaanza kupukutika na kidole gumba kinatokeza.
Huyo dogo atakuwa anaakili zaidi....
 
Dogo yuko vizuri,
Hapo nilinunuliwa Raba made in Tanzania kutoka BORA,
Hapo nilikuwa natumia unga wa betri ule mweusi. Ile betri inatitwa National(Neshno) enzi hizo nabisha nasema ni (Nationali sio neshno kwa sababu hakuna S). Tatizo ule unga mweusi kiatu ndani ya wiki kinaanza kupukutika na kidole gumba kinatokeza.
Huyo dogo atakuwa anaakili zaidi....
Sisi tuliambiwa ule unga mweusi ni sumu, na unaua. Ktk michezo tusithubutu kuonja ule unga!
 
Sisi tuliambiwa ule unga mweusi ni sumu, na unaua. Ktk michezo tusithubutu kuonja ule unga!
Tulikuwa tunajua ni sumu, ila zile zilizoisha kabisa ambazo ganda la bati limekaribia kutoka tulijiaminisha huwa imepungua japo zoezi lilifanyika kwa umakini hadi tulipogundua ule unga unamaliza kiatu.
 
Baba ana Kiwi lakini hiyo ni maalumu kwa ajili ya viatu vyake vya kazini na hata kama ningeweza kuitumia unatumiaje kiwi kwenye D.H?

Mara ya kwanza kutumia Kiwi ilikua nimetoka kwenye kipaimara hivyo vile viatu vya Kipaimara vikapangiwa matumizi mengine ya kuendea shule.

Nikajikuta nimepiga kiwi mpaka soli, na sikujiuliza kama baadaye ningekanyagia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom