Naamini kuna watu wamepitia haya maisha, Kama umepitia haya maisha sema chochote

Kwa mara ya kwanza navaa kiatu mwaka 1978 Darasa la sita huku nyuma ilikuwa ni kupekuwa tu
watoto wa siku hizi wana raha sana ukiwaambiwa tulikuwa tunapekuwa shuleni wanakuona wa ajabu sana ili hali ndiyo ilikuwa hivyo
 
kuna kuchoma matairi yale majivu yake unapiga kwenye kiatu burudanii.
tunatoka mbali na tunaelekea mbali.
umesahau mkuu unga wa tairi lililoungua vizuri (tairi ya general tyre) unachanganya na mafuta ya taa unga wa kidogo wa moshi unaolala kwenye dari la jiko
Nilikuwa natoa Kiwi Grade 0ne kabisa kazi inabaki kung'arisha pamoja na kupigilia pensi na kishati changu cha kibabe
Nikiwa naondoka nyumbani mama ananiambia umaridadi huficha umaskini na uwe mwaminifu ndiyo msingi wako kufanikiwa
(Mama mungu akutunze)
shuleni naahika namba moja basi mambo barabara kabisa
 
M nakumbuk kipnd cha mvua tulikuw tunapak mafuta mazito bdl ya kiwi
 
umesahau mkuu unga wa tairi lililoungua vizuri (tairi ya general tyre) unachanganya na mafuta ya taa unga wa kidogo wa moshi unaolala kwenye dari la jiko
Nilikuwa natoa Kiwi Grade 0ne kabisa kazi inabaki kung'arisha pamoja na kupigilia pensi na kishati changu cha kibabe
Nikiwa naondoka nyumbani mama ananiambia umaridadi huficha umaskini na uwe mwaminifu ndiyo msingi wako kufanikiwa
(Mama mungu akutunze)
shuleni naahika namba moja basi mambo barabara kabisa

teh teh teh asubui vipi ulikuwa unapiga kiporo gani?
 
Dogo yuko vizuri,
Hapo nilinunuliwa Raba made in Tanzania kutoka BORA,
Hapo nilikuwa natumia unga wa betri ule mweusi. Ile betri inaitwa National(Neshno) enzi hizo nabisha nasema ni (Nationali sio neshno kwa sababu hakuna S) kiingeleza tatizo la taifa. Tatizo ule unga mweusi kiatu ndani ya wiki kinaanza kupukutika na kidole gumba kinatokeza.
Huyo dogo atakuwa anaakili zaidi....
 
Huu Uzi umenikumbusha mvali sana,mm nili danganwa ukifa tz unazaliwa ulaya na unakuwa mzungu,kuna Siku nilisaga betri na kuikoroga na baadae nikainywa nikajifunika blanketi ili nife kwa haraka,nilikaa Siku nzima bila kula mpaka walipo niamsha na kuniuliza kwanini nilikuwa nimelala ndipo nika waambia nimekunywa sumi kwakuwa nataka nife nikazaliwe ulaya,kichapo nilicho kipata cwezi kukisahau ever
 
Miye nilikuwa napaka chaki raba zangu safi na shuleni ilikuwa road ya Ikulu ndogo fuuulu lami basi WK mzima smart
 
Dogo yuko vizuri,
Hapo nilinunuliwa Raba made in Tanzania kutoka BORA,
Hapo nilikuwa natumia unga wa betri ule mweusi. Ile betri inaitwa National(Neshno) enzi hizo nabisha nasema ni (Nationali sio neshno kwa sababu hakuna S) kiingeleza tatizo la taifa. Tatizo ule unga mweusi kiatu ndani ya wiki kinaanza kupukutika na kidole gumba kinatokeza.
Huyo dogo atakuwa anaakili zaidi....
Ilitamkwa nationali
 
Mwendo wa kukimbilia nyumbani kuwahi kiporo cha jana.Siku hizi kengere ya kutoka ikilia wanafunzi hawapigi kelele na kugombania mlango.Ice cream za chelewa siku hizi zinaitwa rambaramba,visheti na kababu.Mwendo wa kuunguzana na tunda za ubuyu.Darasa limejaa tunda za ubuyu bila kusahau machata chooni na kwenye kuta za madarasa.Mara AKUMBUKWE CRAZY D,AKUMBUKWE DICK 7 nk.
 
Tatoo ya korosho na njiti ya kiberiti.Mchezo wa vikaratasi unaofanana na bingo/bahati nasibu.
 
Baba ana Kiwi lakini hiyo ni maalumu kwa ajili ya viatu vyake vya kazini na hata kama ningeweza kuitumia unatumiaje kiwi kwenye D.H?

Mara ya kwanza kutumia Kiwi ilikua nimetoka kwenye kipaimara hivyo vile viatu vya Kipaimara vikapangiwa matumizi mengine ya kuendea shule.

Nikajikuta nimepiga kiwi mpaka soli, na sikujiuliza kama baadaye ningekanyagia.
Dah mkuu umenikumbusha DH tulikuwa tunaziita dingi Hana uwezo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom