Naamini ipo siku tutafika hapa,nina ndoto hii na ninaamini itakuwa hata kama wengine tutakuwa tushatangulia mbele za haki.

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Nina tamani sana tufike mahali nchini Tanzania,mtu akitoka CCM aseme "nimeamua kuondoka CCM kwani sikubaliani kabisa na itikadi ya Ujamaa na kujitegemea,nimeona niende kwenye chama ambacho hakiamini katika ujamaa".

Mwingine akitoka Chadema,aseme kwa hoja,,"siwezi kaa chadema kwani siamini kama falsafa ya mlengo wa kati kama inaweza kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye nguvu kiuchumi,binafsi nimeona niende chama cha kijamaa"

Atakayeondoka CUF,aseme "sikubaliani kabisa na Uliberali,nimeshauri kwenye vikao vya ndani tubadili itikadi yetu ila wamegoma,binafsi sikubaliani na falsafa hii,sasa natoka"

Au mwingine aseme naondoka NCCR Mageuzi kwani falsafa ya UTU,haiwezi kutufikisha popote na imeshindwa duniani,nimeamua kutoka na kwenda chama kingine"

Mwingine aseme sikubaliani na falsafa ya ACT,mimi ni muumini wa ubepari,nimeusoma mpaka ngazi ya PHD,sasa nimegundua sikuwa katika chama kinachoendana na falsafa yangu,naachia ngazi nafasi zote za uongozi na ninajivua uanachama"

Hivi ndivyo akina Oscar Kambona,walivyoondoka TANU,hawakuamini katika Ujamaa na waliishi hivyo mpaka umauti ulivyowakuta,hivi ndiyo Mzee Edwin Mtei alivyotofautiana na Mwalimu Nyerere na akaondoka CCM.

Ni ngumu sana mtu ambaye alisoma sawasawa na akasoma vizuri kuhusu masuala ya falsafa za maendeleo na akauelewa vizuri ujamaa eti akaenda chama cha kibepari,pia ni vigumu sana mtu aliyesoma vizuri ubepari akawa mwanachama wa chama cha mlengo wa kijamaa,ngumu sana.

Kinachoitesa siasa ya Tanzania kwa sasa,vijana wengi wapo kwenye vyama vya siasa,kwa sababu wamevutiwa na watu,ama wanasaka fursa za maisha na wengine wanasaka fursa za kutimiza ndoto.

Taifa letu,lina changamoto ya kukosa falsafa yake,tangu tuuzike ujamaa kivitendo mwaka 1992 na kuucha kinadharia,hii imeathiri mpaka uimara wa siasa za Tanzania.

Naamini ipo siku tutafika hapa,nina ndoto hii na ninaamini itakuwa hata kama wengine tutakuwa tushatangulia mbele za haki.

Maana sababu ambazo unazisikia kutoka kwa wanasiasa wanaohama kutoka chama kimoja kwenda kingine nyingi ni magomvi yao ndani ya vyama,huyu haelewani na huyu,huyu anasema nimeambiwa nisiongee na huyu,huyu anasema nimekataliwa kuzungumza na fulani.
 
Mwanahabari Huru sikiliza video hiyo! Salary Slip
 
Attachments

  • KUHAMA VYAMA.mp4
    2.2 MB · Views: 15
Last edited:
Tunagawana pesa hapa za kikao Leo jumapili kama 500,000 nikimaliza nitakujibu mambo ya siasa, Khaa wengine weekend tupo ofisi wewe unapiga poroja weekend,
 
Mkuu siasa za sasa tofauti sana na siasa za akina kambona na nyerere japo hao ni walimu wetu kwenye siasa
 
Back
Top Bottom