republicoftabora
Member
- May 9, 2012
- 59
- 15
nani alisema shida zetu zinatokana na mtu mmoja [rostam]. shida zetu zinatokana na system [ccm] iliyopo madarakani tangu uhuru. lakini mambo yakawa mabaya zaidi kwanzia kipindi cha mwinyi [1985 - 1995]. kwasababu hapa ndipo tabaka la walionacho na wasionacho lilizidi zaidi.
Kujiuzuru kwao ni kulilenga kukiokoa chama na kukisafisha chama sasa pengine tuwaulize wana CCM kama chama kimeokolewa ama kimesafishika vipi..Tafadhali naomba jibu la kichwa cha habari hapo juu.
Kwa takriban humu JF tuliaminishwa kuwa shida zetu zote sisi watu milioni 45 zinatokana na mtu mmoja kwa jina la ROSTAM AZIZ
sasa nashangaa toka aondoke kwenye ulingo wa siasa watu bado wanakufa muhimbili, barabara mbovu, malaria kwa wingi, njaa iko pale pale, maji machafu, watu wanakufa kila kukicha
sasa cha kujiuliza imekuwaje?
au tuliaminishwa visivyo na wachambuzi wa JF?
kwa asilimia 90 yamekwisha maana bado tuna rasilimali zetu ambazo kama wangeendelea kuwepo hapa sasa zingekuwa ni urithi wa wanafamilia zao!
nilikua nataka nikujibu lakini nimeona napoteza mda tuu. muulize baba na babu yako atakwambia kipindi cha nyerere kilivyokua. labda nikupe mfano mmoja wa kipindi cha nyerere, bibi yangu aliwapeleka mama yangu mzazi na kaka zake kusoma kenya kwa kulima tumbaku. sasa hivi tumbaku hiyo hiyo anashidwa kuishi vizuri mpaka mama na kaka zake wamsaidie. sasa jiulize kwasababu gani imekua hivyo. nitakupa neno moja tu kama unaakili nzuri utaelewa "wawekezaji". wewe utakua ujui vizuri historia hayo mambo yote uliotaja hapo juu yalitokea baada ya vita vya idi amini [1978-79] nchi yeyote ikiingia kwenye vita lazima uchumi utashuka.naam kipindi cha Mwinyi?
Sukari kwa foleni
Mafuta ya taa kwa foleni
TV ikulu kwa 'nabii'
Sabuni kwa majani ya povu
Njaa wimbo wa taifa
Hongera 'baba wa Taifa'
Tatizo la Richmond limeisha.Tafadhali naomba jibu la kichwa cha habari hapo juu.
Roma haikujengwa kwa siku moja, una protocol zake ktk ujenzi wowote.Tafadhali naomba jibu la kichwa cha habari hapo juu.