Naam, Lowassa si Waziri Mkuu, Rostam sio active politician sasa, Je matatizo yenu yameisha?

Kwa takriban humu JF tuliaminishwa kuwa shida zetu zote sisi watu milioni 45 zinatokana na mtu mmoja kwa jina la ROSTAM AZIZ

sasa nashangaa toka aondoke kwenye ulingo wa siasa watu bado wanakufa muhimbili, barabara mbovu, malaria kwa wingi, njaa iko pale pale, maji machafu, watu wanakufa kila kukicha

sasa cha kujiuliza imekuwaje?

au tuliaminishwa visivyo na wachambuzi wa JF?
 
nani alisema shida zetu zinatokana na mtu mmoja [rostam]. shida zetu zinatokana na system [ccm] iliyopo madarakani tangu uhuru. lakini mambo yakawa mabaya zaidi kwanzia kipindi cha mwinyi [1985 - 1995]. kwasababu hapa ndipo tabaka la walionacho na wasionacho lilizidi zaidi.
 
kwa hiyo wasingewajibika sababu matatizo hayawezi kuisha kwa wao kuondoka??

No wonder kuna watu wanataka kuwarudisha 2015.
 
nani alisema shida zetu zinatokana na mtu mmoja [rostam]. shida zetu zinatokana na system [ccm] iliyopo madarakani tangu uhuru. lakini mambo yakawa mabaya zaidi kwanzia kipindi cha mwinyi [1985 - 1995]. kwasababu hapa ndipo tabaka la walionacho na wasionacho lilizidi zaidi.

naam kipindi cha Mwinyi?
Sukari kwa foleni
Mafuta ya taa kwa foleni
TV ikulu kwa 'nabii'
Sabuni kwa majani ya povu
Njaa wimbo wa taifa

Hongera 'baba wa Taifa'
 
kwa staili ya dawa ya moto ni moto na siyo maji basi jibu la swali lako ni swali lifuatalo:

Alipokuwa Waziri Mkuu na mwenzake Acive Politician wakati huo , je matatizo yako yalikwisha?

Yangu hayakuisha na ndio maana nasema tujaribu wengine sasa maana kuwepo kwao na kutokuwepo kwao hakuna tofauti!!!
 
Kwa takriban humu JF tuliaminishwa kuwa shida zetu zote sisi watu milioni 45 zinatokana na mtu mmoja kwa jina la ROSTAM AZIZ

sasa nashangaa toka aondoke kwenye ulingo wa siasa watu bado wanakufa muhimbili, barabara mbovu, malaria kwa wingi, njaa iko pale pale, maji machafu, watu wanakufa kila kukicha

sasa cha kujiuliza imekuwaje?

au tuliaminishwa visivyo na wachambuzi wa JF?

Inaonekana unataka kumtetea ROSTAM WAKO kwa mlango wa nyuma. Hamna wakati hapa Tz tumekua na mjadala wa kitaifa kuhusu kwamba jamaa yako Rostam ni kikwazo cha maendeleo yetu kama taifa, japokua ROstam ni poster boy mzuri wa tatizo letu kuu la Ufisadi na kukosa uzalendo kwa viongozi wetu wengi, ila Rostam ni tatizo la ndani la JK, serikali yake na CCM na siyo Tanganyika yetu....Rostam amejenga loyalty ya TAKRIMA ambayo siyo aminifu sana kama loyalty ya KIITIKADI ambayo bado ina chembe chembe ndani ya CCM na inahitaji kufufuliwa na wana miaka miwili ya kufanya hivi la sivyo wanakuja watawala wengine na wao kujaribu jaribu. Huyu Rostam wako atakua hana maana in either scenario.
 
I really wish hawa nguruwe wangeondoka wote!Kwamba kuna mijitu ya ajabu isiyoona umuhimu wa hao kuondoka mi sijui. Nnachojua ni kuwa hii serikali yote, nikimaanisha washirika wao na hao walioondoka nao waondoke ili nchi ibaki salama.
 
Waliofitiana na kuwaondoa akina RA na EL ni wana CCM wenyewe. Mimi naamini kabisa mpaka sasa kufitiniwa na kuangushwa kwa EL kumesababisha ombwe kubwa la uongozi ktk utawala wa sasa na kufungulia njia wanamageuzi kuchukua nchi hii.
 
naam kipindi cha Mwinyi?
Sukari kwa foleni
Mafuta ya taa kwa foleni
TV ikulu kwa 'nabii'
Sabuni kwa majani ya povu
Njaa wimbo wa taifa

Hongera 'baba wa Taifa'
nilikua nataka nikujibu lakini nimeona napoteza mda tuu. muulize baba na babu yako atakwambia kipindi cha nyerere kilivyokua. labda nikupe mfano mmoja wa kipindi cha nyerere, bibi yangu aliwapeleka mama yangu mzazi na kaka zake kusoma kenya kwa kulima tumbaku. sasa hivi tumbaku hiyo hiyo anashidwa kuishi vizuri mpaka mama na kaka zake wamsaidie. sasa jiulize kwasababu gani imekua hivyo. nitakupa neno moja tu kama unaakili nzuri utaelewa "wawekezaji". wewe utakua ujui vizuri historia hayo mambo yote uliotaja hapo juu yalitokea baada ya vita vya idi amini [1978-79] nchi yeyote ikiingia kwenye vita lazima uchumi utashuka.
 
Tumewasingizia akina Lowasa weeee. Sasa kaja jizi lenyewe linaiba matrilion bila aibu na huruma na matusi juu. Hata rambirambi analamba
 
Tafadhali naomba jibu la kichwa cha habari hapo juu.
Roma haikujengwa kwa siku moja, una protocol zake ktk ujenzi wowote.
Au wewe ulikuwa unafikiria EL akiwa Raisi na Rostam akiwa active kisiasa nchi itatatua Matatizo yake papo papo.
By the way kindergarten unasomea wapi. tukulete maziwa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom