Kuna upotoshaji hapa.. Wote wanaoumwa kisukari ni sababu ya pombe? Umefikiria kwamba inawezekana ndugu zako wanaumwa kisukari kwasababu ya suala la vinasaba? Kitu gani utakachokitumia leo ambacho hakina madhara au sumu? Sukari ni tamu, wajua madhara yake?
Ni kwa vip pombe inakufanya masikini? Unajua kuna umri fulani, unabidi uongeze mapato na sio kufikiria nini usifanye ili usiwe maskini. Pia kuhusu ukimwi tunaisingizia pombe kama vile tunavyomsingizia shetani kwa kila kitu. Kitu unachokifanya ukiwa umelewa ndicho unachokuwa unakifikiri wakati wote, labda huwa hatufanyi kwasababu tunaona aibu na uoga. Nimesikia watu wengi wanakorofishana na wenzao na kusema "ngoja nikamnywee pombe atanikoma!". Kama unaacha pombe, acha tu, lakini usilete visingizio na usijisingizie, hakuna atakayekuuliza kwanini unaacha maana hapa duniani kuna vinywaji vingi (soda, chai, maziwa, juisi, bia,n.k) na vyakula mbalimbali (hadi chura na nyoka) na hauwezi kunywa au kula kila kitu.