Na Iwe Marufuku Wanajeshi Wanaoteuliwa Kazi za Kiraia au Kisiasa Kuvaa Nguo za Kijeshi

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Tanzania kuna sheria inayopiga marufuku shughuli za kisiasa kufanyika katika shule, vyuo, sehemu za kazi, jeshini (JWTZ, JKT, Polisi, Magereza, Fire etc).

Sasa cha ajabu ni kwamba kuna wanajeshi ambao wanateuliwa kuingia kazi za uraiani au hata zinazohusu mambo ya chama tawala CCM, na wanaendelea kuvaa nguo za kijeshi. Tunatoa picha gani kwa mwananchi wa kawaida?

Tujiulize, ni picha gani inayoingia kichwani mwa Mtanzania wa kawaida anapomwona mkuu wa mkoa au wlaya aliyevalia nguo za JWTZ anaongea mambo ya kui-promote CCM, wakati tunasema hatutaki siasa ndan ya JWTZ? Je, raia huyo anamowna huyo mkuu wa wilaya au mkoa aliyevalia kijeshi kama nani kwanza - mwanajeshi au mkuu wa wilaya/mkoa? Na kama anamwona kama mwanajeshi kwanza, utamshawishije raia huyo kwamba hakuna siasa ndani ya JWTZ?

Suluhisho hapa ni raisi. Askari yeyote anaeteuliwa kushika wadhifa wa kiraia au kisiasa iwe marufuku kuvaa kijeshi. Kama anaona hawezi kuacha kuvaa nguo zake za kijeshi basi akatae uteuzi abaki jeshini.
 
Back
Top Bottom