Na Hii Ndio Maana Ya Kuzomewa Kwa Zuma na Dr. Slaa Kigoma

Status
Not open for further replies.
- Wote wawili hawajui Demokrasia ndio maana wamezomewa, Sheria ya Demokrasia toka ilipozaliwa Greece ni kwamba ikibanwa huwa inatafuta njia ya kusema kubanwa kwake na huwa ina tabia ya kusema kwa kutumia njia nyingi sana ila tatizo ni kama walengwa wamesikia. Tatizo la Zuma ni lile lile la Chadema na Dr. Slaa, uwazi wa mahesabu ya matumizi ya chama, wote wamejibu kwa kukurupuka Zuma alimfukuza Malema na huku wenzetu wamemfukuza Zitto lakini wote wawili hakuna aliyegusa hoja za Malema na Zitto, ndio maana watazomewa mpaka watakapojifunza kusikiliza sauti ya Demokrasia iliyobanwa.

- Majuzii Katibu Mkuu wa CCM Kinana, katika ziara zake Mikoani aidha Mawaziri wamezomewa au kulaumiwa sana na wananchi mbele ya Kiongozi huyo mkuu wa chama, matokeo jana mawaziri wote wahusika wameitwa na Kamati Kuu ya CCM kujibu mashitaka yao na sababu za kuzomewa kwao, that is Democracy na ndio maana CCM itaendelea kutawala kwa muda mrefu sana kama kilivyo sasa Chama kikongwe cha siasa kwenye madaraka kwa mudaa mrefu kuliko vyote Afrika.

Habari Inaendelea kwenye gazeti la kesho na kila Jumapili la Jambo Leo Uchambuzi wangu.

Le Mutuz Big Shoow
Afadhali uvue hilo kofia la wasomi... maana unajitangaza msomi.. wakati mawazo ya chekechea... lini utapata akili ya mwanafunzi wa sekondari walau? Achilia mbali makofia ya chuo unachojitwika.
 
Hivi Wilium, mnadhani maandiko yenu huwa yanawaongezea wanachama!!!! nawahurumieni sana,
endeleeni kujifariji.
 
Na bado slaa atazomewa sana hadi ajiuzulu
Ni njaa tu zinawasumbua. Hivi hii ajira yenu huwa mnalipa kodi kweli? Kwa hiyo na wewe hapa unatarajia elfu saba? Kazi kweli kweli!!!

attachment.php
 
- Wote wawili hawajui Demokrasia ndio maana wamezomewa, Sheria ya Demokrasia toka ilipozaliwa Greece ni kwamba ikibanwa huwa inatafuta njia ya kusema kubanwa kwake na huwa ina tabia ya kusema kwa kutumia njia nyingi sana ila tatizo ni kama walengwa wamesikia. Tatizo la Zuma ni lile lile la Chadema na Dr. Slaa, uwazi wa mahesabu ya matumizi ya chama, wote wamejibu kwa kukurupuka Zuma alimfukuza Malema na huku wenzetu wamemfukuza Zitto lakini wote wawili hakuna aliyegusa hoja za Malema na Zitto, ndio maana watazomewa mpaka watakapojifunza kusikiliza sauti ya Demokrasia iliyobanwa.

- Majuzii Katibu Mkuu wa CCM Kinana, katika ziara zake Mikoani aidha Mawaziri wamezomewa au kulaumiwa sana na wananchi mbele ya Kiongozi huyo mkuu wa chama, matokeo jana mawaziri wote wahusika wameitwa na Kamati Kuu ya CCM kujibu mashitaka yao na sababu za kuzomewa kwao, that is Democracy na ndio maana CCM itaendelea kutawala kwa muda mrefu sana kama kilivyo sasa Chama kikongwe cha siasa kwenye madaraka kwa mudaa mrefu kuliko vyote Afrika.

Habari Inaendelea kwenye gazeti la kesho na kila Jumapili la Jambo Leo Uchambuzi wangu.

Le Mutuz Big Shoow

Umeabikaje.......thread haijapata. Mwitikio ulioutaka.......jaman mzomeen huyo huyo!!!!!!!!
 
- ha! ha! ha! majibu rahisi kwa maswali magumu au na mimi mtanifukuza Chadema? ha1 ha! ha!

Le Mutuz
Lazima kuna tatizo kichwani kwako watu hawajalifahamu ndio maana wanakujibu na kupoteza muda wao. Hauko sawa kiakili ila unabahati kuwa Chama ulicho hakiwezi kutambua tofauti.
 
Tatizo la watanzania wa aina hii ni kufikiri ki F4F, hawajui kuwa hayo magazeti ya walalahoi ndio yanasomwa na wengi.
wewe na huyo mchumba wako le mutuz mnafikiri ki div 5 ndio maana mnatulazimisha tusome huo utumbo, hebu nipe takwimu za hao watanzania wengi wanaosoma jambo leo kama si lumumba family peke yake. Yaani nipoteze muda wangu kusoma huo utumbo, hebu niambie cha maana alichoandika huyo kubwa jinga
 
- Bado nasubiri mwenye uwezo wa kuzigusa hoja u know!!

Le Mutuz
@Le Mutuz ingawa mara nyingi sikubaliani na wewe kuhusu misimamo yako kisiasa, nikupongeze kwa jinsi unavyowasilisha hoja zako.Uko mstaarabu bro,huna matusi.Kuna id nyingine unayotumia jf?Labda uko makini kwa hili lenye jina lako.
 
Mbona na wewe hujadili hoja wanazotuhumiwa nazo tuone balance ya article yako kama mchambuzi makini bali umefanya comparative analysis ya watu,mahali na nature tofauti.
Vip Tz Magamba yatatawala milele coz CDM wamemfukuza Zitto vp na South ANC ndo watajifia kwa kumfukuza Malema?
Malema amekwenda kuanzisha EFF vp umemshauri Zitto kuanzisha chake?
Malema anapigania maslahi ya wana SA wazi bila uoga na wazi na anasema kina flani waachie migodi na anaaminika kwa misimamo yake vipi hapa tz?
 
Mmoja ya watu ambao wamezomewa ni Kinana hasa karika suala lake la kusafirisha meno ya tembo nje! Kuhojiwa katika vikao vya chama ni suala linghine na kuwajibishwa ni suala lingine! Hebu tuone matokeo yatakavyokuwa! Kinachozomewa na wananchi ni serikali yote ya CCM!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom