Na haya ndio maisha yetu

Nakapanya

JF-Expert Member
May 22, 2012
2,096
708
Nianze kwa kusema;kuujua udhaifu wa adui yako ni hatua moja mbele ya kukusaidia kumshinda huyo adui yako.Watanzania tumekuwa tukikabiliwa na matatizo mengi toka miaka mingi iliyopita hadi sasa,Mwalimu Nyerere alituambia maadui zetu wakubwa ni ujinga,maradhi na umaskini,baadaye wakaongezeka maadui wengine;adui mkubwa alyeongezeka ni ufisadi.Binafsi naomba niongeze maadui wengine wafuatao:
.uoga
.chuki
.ubinafsi
.upuaaziaji.
.kutojitambua
hao ndio ,aadui ambao kwa kiasi kikubwa wanalishambulia taifa letu la Tanzania ambalo tangu kuzaliwa kwake lenyewe linatambaa tuu haliwez hata kuinuka.Watanzania tumekuwa watu wa kwenda na matukio;linapotokea tukio huwa ni wepesi sana kulizungumzia na kuonyesha hisia zetu,pindi linapotokea tukio jingine basi hulisahau tukio la kwanza kabisaa hata kama lilikuwa lina uzito na maslahi ya umma.Ni kwasababu hiyo ndio maana serikali imekuwa ikicheza na akili zetu Watanzania kwasababu wameshajua UDHAIFU wetu hivyo wanatubadilishia matukio kila leo ili tushindwe kuhoji mambo ya msingi;hakika huu ni UDHAIFU mkubwa sana.tunapenda sana kuongea,porojo na kutiana moyo mahali pasipotakiwa,ndio maana watawala hawaishi kusema ni "UPEPO TU UTAPITA",MANENO MENGI VITENDO HAKUNA.(UTOPIAN PEOPLE/NATION). HAYA NDIO MAISHA YETU WATANZANIA.
 
Back
Top Bottom