N. Korea vows 'merciless' war against US

Huyu jamaa ana mikwara tu kama baba yake, sio mara ya kwanza naskia North Korea inamtishia Marekani but each time sijawahi kuona action

Mkuu USA ndio ina mikwara kuhusu nuclear ya jamaa lakini hamna kitu.
Kama watu wanadhani ni mchezo US anzishe vita 21C aone kazi ya nuclear, alipiga watu enzi zile sio hizi zama za technolojia, utandawazi na biashara huria.
 
Dogo acha kuota, jamaa wana nuke ila kibebeo ndo tatizo, namaanisha deliverance. Ila kama wanacho ni mtihani halafu hawana shida ya kupeleka america, wakipeleka kusini kwa ndugu zao tu ni tosha for reunification
 
Sidhani hizo nchi zingine, ukiondoa labda Afghanistan, licha ya kwamba na zenyewe zilikuwa au zinaendeshwa kidikteta, unaweza kuzilinganisha na Korea Kaskazini.

Hata Zimbabwe chini ya Mugabe sasa hivi ina nafuu maradufu kuliko Korea Kaskazini.

Mkuu nje ya mada kidogo
Kampuni za Samsung na LG zipo south au North Korea, hizi series tunazozifuatilia nazo niw za South au North?
 
Dogo acha kuota,

Na wewe acha kuota.

jamaa wana nuke ila kibebeo ndo tatizo,

Hata kama wanazo basi watakuwa nazo zile za kiwango cha chini kabisa na ipo siku yatawavujia na kuwaua wenyewe.

namaanisha deliverance.

Okay

Ila kama wanacho ni mtihani halafu hawana shida ya kupeleka america, wakipeleka kusini kwa ndugu zao tu ni tosha for reunification

Hata Kusini wanazo vilevile na hawatasita kuzirusha Pyongyang. Na zikirushwa sijui huyo Lil' Kim atakimbilia wapi....
 
Hapo napo kuna utata kwamba kanadanganya Ulimwengu kwamba kana kitu kizito, lakini wachunguzi wengi duniani wa mambo haya wanaamini jamaa anacho kitu kizito. Ndio sababu wanakuwa makini mno katika kukatia adabu.

mkuu BAK suala la North Korea kumiliki nukes si la kuaminika ni ukweli mtupu na hata wamarekani na washirika wao wanalifahamu hilo na wanaogopa ukizingatia sasa hivi anamiliki Taepodong 1na taepodong 2ambayo ni ICBM ambayo inauwezo wa kupiga mpaka upande wa mashariki wenye majimbo ya New York, New Jersey, North na South Carolina na mengineyo acha ule wa magharibi unaopakana nayo kwa bahari wenye LA, Frisco, nk. kwa hiyo America na South Korea wanajua nini IL sung, Jong IL na Jong un wanazungumzia.
 
Reactions: BAK
Wabongo mnajua kujudge vitu sana, but nchi yenu yenyewe inateketea, hamna maamuzi magumu
 
Ni dhambi kurithishana madaraka kwa watoto na vitukuu. Huyo jamaa hana akili kabisa....halafu kwa size na akili anafanana kabisa na prince wetu hapa...mbunge wa lile jimbo aliloliacha baba baada ya kuingia ofisi kubwa. naye anataka kuwa Rais..
 
Wa awamu ya kwanza.

Halafu kwa size na akili anafanana na prince wetu...the lawyer na mbunge. Unaonaje baba angemuachia madaraka kuendeleza maendeleo yaliyoletwa na awamu ya nne? Ya wizi mkubwa mkubwa wa mali za umma??!!
 
Wabongo mnajua kujudge vitu sana, but nchi yenu yenyewe inateketea, hamna maamuzi magumu

Mjiinga sana ni wewe "unayejua" wabongo waajjinga halafu unategemea wafanye mambo ya wenye akili. . . . . umekaa nyuma ya jogoo unasubiri atage!!!
 
Kama wabongo tuu

Wabongo mnajua kujudge vitu sana, but nchi yenu yenyewe inateketea, hamna maamuzi magumu

Bongo pamoja na mabaya yake yote, pamoja na umaskini wake wote, na pamoja na mapungufu yake yote kwangu ni bora maradufu kuliko hiyo Korea Kaskazini.

Watanzania hatufugwi kama nguruwe.
 
Ni dhambi kurithishana madaraka kwa watoto na vitukuu. Huyo jamaa hana akili kabisa....halafu kwa size na akili anafanana kabisa na prince wetu hapa...mbunge wa lile jimbo aliloliacha baba baada ya kuingia ofisi kubwa. naye anataka kuwa Rais..

Kinadharia tete, ukipewa uchaguzi wa kuzaliwa Tanzania au Korea Kaskazini utachagua uzaliwe wapi?
 
Mkuu USA ndio ina mikwara kuhusu nuclear ya jamaa lakini hamna kitu.
Kama watu wanadhani ni mchezo US anzishe vita 21C aone kazi ya nuclear, alipiga watu enzi zile sio hizi zama za technolojia, utandawazi na biashara huria.

Unapanua panua mdomo hujui hata unachoongea
 
Wabongo mnajua kujudge vitu sana, but nchi yenu yenyewe inateketea, hamna maamuzi magumu

Kila taifa lina vyombo vyake vya kufanya maamuzi liwe limestawi au linadorola, kwahiyo hatuwezi kuacha kuangalia wenzetu wanafanya nini eti kisa hicho unachokiita wewe kuteketea, unataka wote tuingie ikulu, bungeni, nk haiwezekaniiiii
 
Wanawake jeshini wanalia kwa kumtaka, hawa sio wa kuwaambia mambo kama hayo.

Duh!, wadada wako all over him na kumlilia kabsa!,...ama kweli kama kwako kipofu kwa mwenzio kengeza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…