Kama ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam.. Then gari yenye Natural Aspirated engine kwako ni sawa..
Ila kama unaishi nje ya Dar ni bora utafute gari yenye Turbo.. Ukiwa na Natural Aspirated hautoweza kupata power yote kama mtu wa Dar..!
Dar ipo +0.00m kutoka usawa wa bahari..
Mikoa mingi ipo juu ya huu usawa.. Mfano Mbeya ni 1700m kutoka usawa wa bahari.. Sasa kwenye kila 300m inayoongezeka kutoka usawa wa bahari engine yako itakuwa inapoteza nguvu kwa around 3%..!
Kwahiyo gari yenye 200hp Dar es Salaam Mbeya itakuwa na 166hp..
Hii ni kutokana na engine kushindwa kuvuta hewa vizuri same na binadamu ukipanda mlimani unavyopata shida kuvuta hewa..!
Hili tatizo kwenye Turbo halipo ndio maana gari zenye Turbo kwenye kupanda milima ndio zenyewe..
Mkonga vs Defender kwenye mlima..!
Hiyo kitu ipo mkuu...Hii research umeanzia japan kabisa au bongo tu...anyway, sawa wengine hatujui kitu ni kukanyaga wese tu
Ikifika zambia itakuwa na HP 100
Sawa mkuuHiyo kitu ipo mkuu...
Atmospheric pressure inapungua kadri unavyopanda mlima. Na inakuwa maximum kwenye usawa wa bahari.
Pressure inapokuwa ndogo hewa inaingia kwa shida kwenye engine ukilinganisha na sehemu ambapo pressure ni kubwa. Hii ni kwa Natural aspirated engines.
Kwa upande wa gari zenye turbo, Turbo inalazimisha hewa kuingia kwenye engine hivyo hakutakuwa na mabadiliko yoyote.