Mzunguko wa hela umekuwa shida sana mitaani

Mzunguko wa hela umekuwa shida sana mitaani

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Ndugu zangu mzunguko wa hela umekuwa shida sana kwa sasa mitaani. Kwa kweli fedha hakuna kila mtu ni kulalamika tu. Leo nimefika Benki fulani kwanza nimemkuta Meneja hana raha kabisa kisa anasema watu wanaofanya shughuli na Benki hawapo. Nimekuta watu wachache wa kuhesabu tu.

Kweli kuna tatizo. Kwa upande wa usafiri ndo usiseme. Wengi wamesimamisha mabus yao kwa sababu ya ukosefu wa abiria. Juzi nilipanda Bus kwa kawaida kampuni hiyo ya mabus ilikuwa inajaza kwelikweli.

Juzi tumesafiri kwenye Bus hilo abiriai 15 mpaka mwisho wa safari. Kuna tatizo. Tunaiomba Serikali ifanye utafiti juu ya matatizo haya na ije na jawabu ya kurekebisha matatizo haya.
 
siku hizi hatuend bank.. tunadeposit na ku draw kwa simu...

siku hizi hatupandi ma bus.. tunapanda bombadia na dreamliner...

tupo kwenye uchumi wa viwanda now
 
Mkuu wewe Binafsi ulikua unafanya shughuli gani ya kukuingizia kipato ambayo Sasa hivi unaona mambo yamebadilika?

Achana na hiyo ya kusema flani ameniambia!
 
hakuna simple Deals kila kitu ni Timing upate mchongo.
 
Tunaweka kwenye vibubu bank zenyewe zinafungwa[emoji2]

Watu waache ushabiki uchwara Hali ya mazingira ya kifedha na mzunguko wake sio rafiki kwa mtanzania hata kidogo, matumizi yamekuwa juu mno kuliko kipato na hata biashara pia mazingira, uingizi na ufanyaji biashara umekuwa mgumu nyingi Kama hazijafa Basi zinajikongoja.
Lazma watu waelewe hakuna mtu anaetaka serikali impe pesa duniani popote hamna hiyo, serikali huwa inatengeneza platform ya maisha na ufanyaji biashara kwa watu wake.
Hapa kwetu viongozi wanaokula na kuvaa na kufanyiwa kila kitu bure jibu lao Ni moja kila wakisikia wananchi wanalalamika kuhusu maisha " hao watakuwa wapiga deal".
Uongozi wa kipindi hiki hauna vision
 
Back
Top Bottom