Mzungu ombaomba Dar

Mzungu ombaomba Dar

hannibali

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
468
Reaction score
427
Habari zenu ndugu zangu poleni na majukumu.

Jana nilikuwa nimetulia kwenye moja ya hotel hapa katikati ya jiji napendaga sana kuja kujipumzisha kidogo kupata vinywaji.

Sasa bhana kuna jamaa mwenye asili ya kizungu akaja akanigusa bega kidogo akavuta kiti nayeye akakaa, Tukasalimiana vizuri akanambia huwa ananionaga nakujaga mara kwa mara pale kwani yeye yupo kitambo kidogo pale..

Basi katika stori mbili tatu nikashangaa ananiomba nimsaidie hela kwani hana hela hajatumiwa akanambia ilibidi apate hela siku mbili hizi lakini imeshindikana.

Kwa hela aliyokuwa anahitaji nikatafakari sana lakini mwisho wa siku nikamwambia ajaribu kwenda ubalozi wanaweza wakasikiliza hitaji lake.

My take:: madada zetu na wapenda mteremko sio kila mzungu mnaemwona basi ana hela wengine wapiga vitonga tu so kuweni makini.

===
Mikasa ya ufanano
Mzungu Omba Omba ndani ya Dar
 
Huyu hujamuelewa tu! Alianza na Arabs then Indians sasa Euros nasubiri Japanese, Chinese then Latinos.
Mimi ninakaa sana na Jamii tofauti na hii inatokana na mazingira ninayoishi kwaio usishangae kuja na mada za hao watu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom