Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,473
- 13,629
Ukimkwepa mzungu kwenye utalii utakutana nae pale ambapo unahitaji kuweka rada nne nchi nzima kimkakati.
Ukimkwepa mzungu kwenye suala la kilimo cha kisasa, utakutana nae kwenye suala zima la watalii ambao wakija kwa wingi pato la taifa linaongezeka.
Ukimkwepa kwenye utalii utakutana nae kwenye suala la wataalam mbalimbali wa afya.
Namuongelea mzungu kwa maana ya mtu mweupe na makandokando yote aliyonayo.
Ninaipenda sana hii jeuri ya awamu ya tano, ya kwamba sisi tunaweza, ni waafrika wachache sana ambao wanajengana kisaikolojia kwa kuambiana kuwa wanaweza.
Lakini aliyeiumba asili aliumba ile hali ya binadamu na viumbe vingine kushirikiana na kutegemeana.
Kwa muafrika (mtanzania) mzungu hakwepeki ni kama maji vile. Usinawa uso asubuhi mchana utayanywa kabla ya kula. Usipoyanywa utayahitaji jioni kwa ajili ya kuoga.
Matamko yanawakilisha mtazamo wa kiuongozi, lakini uhalisia ni kwamba no man is an ireland. Hayupo mwenye jeuri ya kujitegemea pasipo kupata ushirikiano wa mwingine.