Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,773
Habari za leo wapendwa,
Leo shost alikuja ofisini leo kunitakia kheri ya mwaka mpya, huyu ni shost wa nursery school na tulianza primary pamoja kabla ya wazazi wake kuhamia mkoani bai tulipoteana, tulikutana ukubwani tena kwenye seminar elekezi, tangu hapo tuna mawasiliano mazuri sana. Nilishangaa shost amenitupa kumbe ananieleza walikuwa na ugeni nyumbani.
Shost kwao yeye ndiye mtoto wa kike pekee tena ni wa mwisho, ana makakak watatu. Kaka mkubwa aliondoka nyumbani mwaka 2004 kwenda ughaibuni kwa kuendelea na masomo. Kufika kule bwana kaka mkubwa alipata girlfriend wa kizungu, mapenzi yalinoga wifi aliinua mimba.
Kaka aliona ni busara kutangaza ndoa, basi alioa na familia ilibahatika kupata mtoto wa kiume mwenye afya njema. Kasheshe ilikuja sasa wifi wivu ulipitiliza, kaka alipewa dakika 30 awe amefika nyumbani baada ya masomo au kazi. Pesa yote inayopatika wifi aliipangia budge ya ndani.
Kaka akiwa ndiye mtoto mkubwa alishindwa hata kupeleka laki moja ya msaada nyumbani. Siku baba alipougua na kulazwa hospitali, kaka aliwashauri ndugu nyumbani wampeleke kaka hospitali nzuri atagharamia matibabu, wewe we wee, wifi aliposikia hayo alisema familia yako ni mimi wewe na mtoto. Kaka ilibidi akope pesa kwa marafiki na kulipa deni la hospitali, ila baada ya hapo alimwambia wifi "it's over between us".
Tangia 2010 kaka amerudi hajamuona mtoto wake, alishaweka kichwani kuwa mtoto atamtafuta akiwa mkubwa. Bidada kumbe amepata mashost wa kibongo huko aliko, anafuatilia habari za kaka kila kukicha. Tangia September alishapiga simu akisema anamleta mtoto aje Christmas na New Year bongo.
Mgeni amefika na mwanae, amefikia kwa wazazi na analala chumba kimoja na wifi yake. Kasheshe shost ananiambia ameamka anatandika kitanda cha wifi wakati mwenyewe yuko bafuni, si akute picha ya kaka yake imegandishwa hirizi kwa nyuma wifi anaweka chini ya mto akilala.
Shost ndiyo ananiambia leo hii, nimeshindwa kucheka, nilibaki kumuonea huruma mwanamke mwenzangu penzi linavyomtesa mpaka kujua ushirikina.