Mzungu mwingine ammwagia maji machafu polisi

Mzungu mwingine ammwagia maji machafu polisi

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2008
Posts
2,268
Reaction score
338
Mzungu mwingine ammwagia maji machafu polisi

na Ramadhani Siwayombe, Arusha
SAKATA la raia wa kigeni kuwadhalilisha Watanzania, sasa linaonekana kushika kasi, baada ya raia mwingine wa Afrika Kusini kumdhalilisha askari kwa kummwagia maji machafu.

Tukio hilo limetokea siku chache baada ya raia wa Canada ambaye pia ni ofisa ubalozi wa nchi hiyo nchini, kumtemea mate askari wa usalama barabarani na mwandishi wa habari.

Katika tukio la juzi, raia huyo wa Afrika Kusini, Gesina Susanna Hayes, alimmwagia maji machafu askari huyo aliyekuwa akilinda Benki ya Barclays iliyopo katika majengo ya TFA na kisha kumtolea matusi ya nguoni.

Baada ya tukio hilo, askari huyo PC Sengerema mwenye namba G.1757, alimdhibiti Hayes na kumfikisha katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa na kufunguliwa jalada namba AR/RB/8591/09 kabla ya kufikishwa mahakamani.

Raia huyo wa Afrika Kusini, alipofikishwa mahakamani alishindwa kujitetea, hivyo Hakimu Magesa wa Mahakama ya Mwanzo Maromboso mjini hapa kumhukumu kifungo cha miezi mitatu jela baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashitaka.

Wakati hukumu hiyo inatolewa, raia mwingine wa Canada alimdhalilisha askari wa usalama barabarani kwa kutemea mate.

Licha ya raia huyo wa Canada kumtemea mate askari huyo, pia alimtemea mate mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha TBC1, Jerry Muro, lakini kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria, Ubalozi wa Canada nchini ulitangaza kumrejesha nchini kwao kutokana na kitendo hicho.

Souerce:Mtanzania Daima
 
Bravo PC Sengerema , Kama mtu analeta upuuzi kama huu dawa ni moja tu, kamata yeye, peleka Polisi, laza rumande kisha peleka mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Hii ndio itakua fundisho kwa wengine wanaodhani wanaweza kudhalilisha watanzania.
 
What a sweeet news..Nimelipata kwa upana tukio hili hapa Arusha, na linaongelewa katika viunga vyote vya hapa!

Nadhani sasa watanzania watakuwa na courage ya kutosha kupambana na watu hawa wenye ngozi nyeupe wanaojiona wao wana haki zaidi ya ubinadamu kuliko wengine!

Bado hawa waNAOITWA WATZ WA ASILI YA aSIA AMBAO WANA MANYANYASO YA JUU SANA KWA WABONGO!
 
Kazeni buti wamakonde, msipoangalia mtachukuliwa mpaka wake zenu!!!
 
Inatakiwa siku nyingine hii mizungu ikileta za kuleta ni kuyapatia kichapo tu then yeye aende akashitaki polisi....
 
Kudos PC SENGEREMA, kweli Said Mwema sasa amewapika na mmeiva. Kwanza nakupongeza kwa uvumilivu na kufuata Sheria vinginevyo ungeitumia hiyo SMG uliyokuwa nayo, lakini umefundishwa kutumia nguvu kidogo pale inapohitajika na kweli umefanya kwa ungalifu. Huyo KABURU akitoka gerezani sasa aende akamwambie Mama yake na Baba pamoja na MAKABURU wengine kwamba Watanzania si Mchezo
 
Bravo PC Sengerema hawa wazungu sio wa kuwanyenyekea kila mtu ana haki chini ya jua, haingii akili mtu ana mwingine ajione yeye ndo yupo juu kisa yeye ni mweupe mnao nyanyaswa na hawa jamaa chukueni hatu mara moja kuwaadabisha tu.
 
Back
Top Bottom