Ubora wa elimu unapimwa kwa vitu vingi vinavyochochea taaluma.
Kwanza, ubora na idadi ya waalimu! Tangu nyakati za uhuru tuna walimu wangapi, na ubora wao ni upi! Utabaini kuwa kwa sasa idadi ya walimu inapanda kulingana na ukubwa wa namba ya wanafunzi, lakini pia ubora wa waalimu unaridhisha kutoka kuwa na waalimu wa UPE mpaka kupata waalimu wenye weledi waliopitia mafunzo kamili vyuoni.
Pili, idadi ya shule! Hapa ni mjumuiko wa vyuo vya ufundi, VETA, vyuo vya kati na vyuo vikuu! Bila shaka katika nyakati hizi za sasa idadi ya taasisi za elimu ni nyingi na zinatoa mafunzo kwa wanafunzi wengi. Hivyo elimu imepanda.
Tatu, idadi ya wahitimu. Zamani tulikuwa na wasomi wachache sana. Idadi kubwa ya watanganyika walikuwa mbumbumbu kupita kiasi. Miaka ya karibuni tumefanikiwa kuzalisha wahitimu wengi wenye ujuzi na taaluma mbalimbali kuanzia madaktari, walimu, wanasheria, mafundi, mainjinia, na wengine wengi.
Nne, Ubora wa syllabus na nyenzo za kufundishia. Zamani syllabus zilikuwa duni na mbovu maana malengo ya elimu ya kipindi hicho ilikuwa ni kupata wataalamu wa voda fasta ili kujaza nafasi wazi serikalini na taasisi mbali mbali. Syllabus za kipindi hichi cha sasa zimeboreshwa sambamba na usimikwaji wa nyenzo za kiteknolojia na za kisasa kama vile maabara bora, kompyuta, na mitaala yenye kuchochea maswala ya teknohama na tehama mashuleni.