MZIMU WA KINYAMKELA

KIBINDU

Senior Member
Jul 2, 2015
120
236
MZIMU WA KINYAMKELA
Huu ni mzimu wa kizaramo ambao baadhi ya wazaramo wengi wao huutumia kwa matambiko mbalimbali kama kuepukana na maradhi,kuwa na mafanikio maishani na kuimarisha umoja wa kiukoo.
Matambiko hayo hufanywa kwa njia mbalimbali kama dogoli la michi au dogoli la ngoma kupitia koba la uganga na mganga wa jadi. Pia hufanywa kupitia kibanda cha kinyamkela ambacho hujengwa kwenye mti mkubwa aina ya mvule.
Kuna wakati babu yangu alinieleza kuwa "usithubutu kukata mti wenye kibanda kwani dhahama utakayoipata maishani haielezeki"
Alinipatia mifano ya watu mbalimbali waliodiliki kuukata mti huo na majanga waliyoyapata kama kupata ukichaa.
Mzimu huu una mkoba unaoitwa koba la uganga.
Koba hili huwa linarithiwa kwa ndugu yeyote ndani ya ukoo.Hapa ndipo panapokuaga na changamoto ya baadhi ya watu kulikataa koba ambapo ni kosa kubwa sana.
Babu yangu alinisimulia kisa cha baba yangu kulikataa koba kipindi ambacho nikiwa mdogo sana.Alipatwa na dhahama kubwa ya magonjwa yasiyo na tiba ambayo yalihatarisha uhai wake takribani kwa miaka mitatu. Akaelezwa njia pekee ni kulikubali koba mwisho akakubali.
Lilipigwa dogoli hivyo akakabidhiwa koba na ukawa mwisho wa maradhi yake.
SASA BASI FATHER AMESHAFARIKI MUDA KIDOGO NA KOBA LINAHITAJI MRITHI AMBAYE KWA ASILIMIA KUBWA UKOO UMEBASHIRI NI MIMI. JE NIFANYAJE IKIWA MZIMU UNAHITAJI NIWE MIMI??
 
Back
Top Bottom