Mzee Yusuph: Maisha yangu yamekuwa magumu baada ya kuacha muziki

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Aliyekuwa Msanii nguli wa Taarab nchini Mzee Yusuph amesema kwa sasa maishayake yamekuwa magumu baada ya kuacha muziki
Baada ya kuacha muziki anadai alijaribu shughuli nyingine ikiwemo kufungua duka Kariakoo lakini duka likafeli, lakini anasema maisha yamekuwa ya amani kuliko zamani na hata mtu akimuomba hela haogopi kumwambia hana kwa sababu hana kazi
Pia alipoacha muziki alikuwa ameshachukua milioni 25 za show na alipoulizwa itakuje na show alizochukua hela alisema Allah ndio atajua

Hizi site mbili za tofali kule chanika umefunga au bado zinapiga kazi,,,mzee yusuph hakuna mtu anaeuza tofali nying kama wewe wilaya hii ya ilala,,na ghorofa unajenga pale ofisin bado unasema mambo magumu?? Pale bonden buyun umempangia sijui nani yule nyumba sh 500,000 kwa mwezi nyumba ya yule mama anaefanya kazi ikulu bado kwel mambo mabaya?? Ha ha ha haya Mkuu ila jambo ulilofanya lina thawabu kwa Allah kuliko uliloacha
 
Mbona nasikia kuwa huwa anatoa na burudani nyingine ile ya Kimombasa, Kipemba na Kilamu japo Kisirisiri sasa kwanini asijikite tu kwa hiyo kwa wakati huu anaokutana na njaa kali kama anavyotanabaisha Yeye mwenyewe? au na hiyo biashara ya Kimombasa, Kipemba na Kilamu nayo siku hizi haina tena Soko kama huku nyuma?

Shikamoo Mzee Yusuph.

Kwakuwa 'umesikia'
ndo unaona inakupa haki ya kumdhalilisha kwa sababu tu umesikia?

Vyote ambavyo watu wanasema tunasikia vingekuwa vinatumika
kama ndio facts kuwahukumu watu wewe ungebaki salama?
 
Aliyekuwa Msanii nguli wa Taarab nchini Mzee Yusuph amesema kwa sasa maishayake yamekuwa magumu baada ya kuacha muziki
Baada ya kuacha muziki anadai alijaribu shughuli nyingine ikiwemo kufungua duka Kariakoo lakini duka likafeli, lakini anasema maisha yamekuwa ya amani kuliko zamani na hata mtu akimuomba hela haogopi kumwambia hana kwa sababu hana kazi
Pia alipoacha muziki alikuwa ameshachukua milioni 25 za show na alipoulizwa itakuje na show alizochukua hela alisema Allah ndio atajua

Kwani alilazimishwa kuwacha kazi yake?asituzingue
 
Kwakuwa 'umesikia'
ndo unaona inakupa haki ya kumdhalilisha kwa sababu tu umesikia?

Vyote ambavyo watu wanasema tunasikia vingekuwa vinatumika
kama ndio facts kuwahukumu watu wewe ungebaki salama?
Ebu tufafanulie tujue huo udhalilishaji ni upi mkuu maana kufanya biashara mombasa, Pumba na lamu kama una leseni sioni kama ni tusi
 
Back
Top Bottom