Mzee Warioba kuongoza tume ya katiba!

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,285
9,922
Kwa tarifa nilizozipata leo Mzee warioba huenda akateuliwa na Rais Kuwa mwenyekiti wa tume ya kusimamia maoni ya katiba, tume hiyo itatauliwa siku chache zijazo.
 
Prof. SHIV NDO AMBAE ANGETENGENEZA CHA MAANA JAMANI WEE BABA RIZ CKIA!
 
Kila siku najiuliza hivi tz hakuna wanaharakati wasomi wa kuchukua haya majukumu, kuliko kila siku kuyafikilia mazee haya?
 
Vijana wapo tatizo ni wanafiki mkuu! Wazee kama Prof Shivji na uhindi wake anasema chochote bila hata chembe la uoga!
 
Kwa tarifa nilizozipata leo Mzee warioba huenda akateuliwa na Rais Kuwa mwenyekiti wa tume ya kusimamia maoni ya katiba, tume hiyo itatauliwa siku chache zijazo.

Warioba simuoni kama mzaledo wa kweli

Katika bodi ya TTCL amesima kwa niaba ya airtel na amekuwa kikwazo kikubwa kwa TTCL kutaka kuwekeza ktk GSM au kuunga mkono wazo la kutafuta mkopo kuboresha TTCL kisa eti inapingana na maslahi ya anaowakilisha(Airtel) . Anataka TTCL ife na isitoe upinzani kwa anaowawakilisha, aitel( zamani celtel) imjengwa jUu ya mgongo wa TTCL kama mali ya TTCL baadaye TTCL kupokwa mali yake bila malipo yoyote kwa kupitia nguvu za kifisadi za Omary issah , Salim H. Salim wakishirikiana na Warioba . Kwa ujumla ni moja kati ya wahujumu wakubwa wa TTCL mali ya watanzania
 
Shivji si mzawa mwenye asili ya hapa. Hatuwezi kuandikwa katiba na mtu anaitwa "Shivji."
 
Warioba simuoni kama mzaledo wa kweli

Katika bodi ya TTCL amesima kwa niaba ya airtel na amekuwa kikwazo kikubwa kwa TTCL kutaka kuwekeza ktk GSM au kuunga mkono wazo la kutafuta mkopo kuboresha TTCL kisa eti inapingana na maslahi ya anaowakilisha(Airtel) . Anataka TTCL ife na isitoe upinzani kwa anaowawakilisha, aitel( zamani celtel) imjengwa jUu ya mgongo wa TTCL kama mali ya TTCL baadaye TTCL kupokwa mali yake bila malipo yoyote kwa kupitia nguvu za kifisadi za Omary issah , Salim H. Salim wakishirikiana na Warioba . Kwa ujumla ni moja kati ya wahujumu wakubwa wa TTCL mali ya watanzania

mama weee!!! na huyu ndio anapewa kusimamia katiba tena? ......tumekwisha
 
Prof Warioba ni mwajiriwa wa Rais hivyo lazima atekeleze maagizo ya mwajiri wake, kuna maoni ya kweli hapo? hana tofauti na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi au msajili wa vyama. nasafi hizi zilitakiwa kufanyiwa usairi mtu anaingia kwa competence sio veting
 
Prof Shivji anafaa sana kwenye position hiyo: nina wasi wasi sana na impartiality ya Warioba kutokana na background yake.
 
TUME YA MABADILIKO YA
KATIBA
(Sheriaya Mabadiliko ya
Katiba, Sura 83,
Toleola 2012, Vifungu 5, 6
na 7) ___________________________
___
UONGOZI WA JUU
1.Mhe. Jaji Joseph Sinde
WARIOBA- Mwenyekiti
2.Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino RAMADHANI -
Makamu Mwenyekiti
WAJUMBE KUTOKA
TANZANIA - BARA
1.Prof. Mwesiga L. BAREGU
2.Nd. Riziki Shahari MNGWALI
3.Dr. Edmund Adrian
Sengodo MVUNGI
4.Nd. Richard Shadrack
LYIMO
5.Nd. John J. NKOLO 6.Alhaj Said EL- MAAMRY
7.Nd. Jesca Sydney MKUCHU
8.Prof. Palamagamba J.
KABUDI
9.Nd. Humphrey POLEPOLE
10.Nd. Yahya MSULWA 11.Nd. Esther P. MKWIZU
12.Nd. Maria Malingumu
KASHONDA
13. Mhe. Al-Shaymaa J.
KWEGYIR (Mb)
14.Nd. Mwantumu Jasmine MALALE
15.Nd. Joseph BUTIKU
WAJUMBE KUTOKA
TANZANIA- ZANZIBAR
1.Dkt. Salim Ahmed SALIM
2.Nd. Fatma Said ALI 3.Nd. Omar Sheha MUSSA
4.Mhe. Raya Suleiman
HAMAD
5.Nd. Awadh Ali SAID
6.Nd. Ussi Khamis HAJI
7.Nd. Salma MAOULIDI 8.Nd. Nassor Khamis
MOHAMMED
9.Nd. Simai Mohamed SAID
10.Nd. Muhammed Yussuf
MSHAMBA
11.Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN
12.Nd. Suleiman Omar ALI
13.Nd. Salama Kombo
AHMED
14.Nd. Abubakar
Mohammed ALI 15.Nd. Ally Abdullah Ally
SALEH
UONGOZI WA SEKRETARIETI
1.Nd. Assaa Ahmad
RASHID- Katibu
2.Nd. Casmir Sumba KYUKI- Naibu Katibu
CHANZO-Neville C. Meena,
(mabadiliko)
 
Naanza kuiona nia njema ya Mhe. Rais Kikwete. Hongera sana. HII itakufanya ukumbukwe na vizazi vijavyo.
 
Kwa jopo hili nami nakubaliana nawe Mh. Rais Kikwete umeandikwa histolia mpya. Hongera sana. Kabudi,walioba,balegu.mvungi
 
namkubali kwa kila kitu isipokuwa tu uwakilishi wa bara na zanzibar kwanin uwe sawa? Hapa ilitakiwa ratio isiwe 50% kwa sababu bara kuna wananchi wengi kuliko zenji.
 
namkubali kwa kila kitu isipokuwa tu uwakilishi wa bara na zanzibar kwanin uwe sawa? Hapa ilitakiwa ratio isiwe 50% kwa sababu bara kuna wananchi wengi kuliko zenji.

Tunapoongelea uwakilishi ulio sawa bara na visiwani, naomba na visiwani tuongelea uwakilishi ulio sawa kati ya wakristo na waislamu maana kote nchi zetu si za dini fulani!!!! Vinginevyo hapa kuna shida kwa upande wa muungano
 
Back
Top Bottom