Mzee wangu anakaribia kustaafu, uwekezaji upi ni mzuri?

Hata sijasoma comments, ila kichwa cha uzi nimecheka tu.

Kama maisha yake yote, hajui cha kufanya hiyo pesa itapotea kwa asilimia zaidi ya 50 ndio mjipate

Mungu wetu awe na nanyi.
 
Matajiri (hata waliozeeka) wanakwenda benki kuomba mikopo ili wafanye mambo.
Maskini anaamua kuweka pesa benki.

Baba yangu alistaafu 1983. Bado yuko hai.
Alipewa kiinua mgongo sh.30,000/=(elfu thelathini).
Aliamua kupanda kahawa na miti. Ndiyo inayotuunga mkono kumtunza.

Angeiweka benki angekuwa ana nini, ukizingatia makato yao yasiyo na huruma, mfumuko wa bei, kushuka kwa thamani ya pesa nk.
Mwaka jana, Desemba; sukari ilikuwa 3,000/=. Leo ikoje?

Muwe makini sana.
 
Kuna watu wameongeza thamani ya mfumo kwa kuingiza pesa ndefu haswa bllion na kitu..

Hawa jamaa siku watatoa na thamani ya kipande itashuka kwa vile speculation upande wa kununua itakuwa chini....Sasa hapa wabongo watajua wamepigwa kumbe hawana uelewa wa soko la hisa ngoja tuone
System ya bongo haipo hivyo,
Sio kwamba mtu akitoa et itashuka to the point ya kuwa noticed, mbna wakat wananunua haikupanda ?
 
Salamu ziwafikie wana Jf wenzangu.
Ninaomba msaada katika uwekezaji wa fedha benki.

Ni hivi mimi nina mzee wangu anayetarajia kustaafu mwaka huu. Sasa kama kijana wake wa pekee na anayeniamini ameniomba nimsaidie namna ya kuwekeza fedha zake kwa ajili ya kufurahia uzee wake.

Sasa mimi cha kwanza kabla ya mengine ninachotamani ni kwamba mzee awekeze fedha zake benki ili ikiwezekana kila mwisho wa mwezi awe kama anapokea mshahara wa kati ya 500,000-700,000 za kitanzania huku ile hela yake aliyohifadhi ikibaki kuwa dhamana yake katika uwekezaji na akiitaka aichukue muda wowote ule.

Nimefatalia kwa umakini sana humu JF uwekezaji wa namna hii mfano, hisa, UTT, fixed account n.k. lakini bado sijapata kile ninachokifikiria kuwa afungue tu akaunti awekeze hela huko kisha kila mwezi awe anavuna kiasi tajwa hapo juu. Sasa maswali yangu ni haya hapa chini.

i. Je Kuna uwezekano wa kupata akaunti ya kuwekeza labda tuseme milioni 20 au 30 za kitanzania na mtu akapata mavuno ya laki 5 Kila mwezi?

ii. Kama ni ndio je ni kiasi gani kinaweza kuleta mavuno ya laki 5 kama jibu ni sio je ni akaunti gani naweza kuwekeza angalau kupata kiasi kizuri kwa mzee kwa kila mwezi?

iii. Je ni benki gani nzuri itafaa Kwa uwekezaji huo kwa ajili ya mzee?

N.B: Kumbuka sitamani uwekezaji mwingine zaidi ya huo hapo juu. naomba ushauri ujikite katika muongozo huo. Natanguliza shukrani zangu.

Soma Ushauri kwa wastaafu na wanaopata hela nyingi kwa mkupuo
Ni ngumu kukushauri bila kijia life style na investment zilizopo lakini pia preference ya baba yako
 
System ya bongo haipo hivyo,
Sio kwamba mtu akitoa et itashuka to the point ya kuwa noticed, mbna wakat wananunua haikupanda ?
Kununua ndio kunaongeza thamani ya kipande ...Binafsi nina hisa hizo tangu 2002 hazina faida ...Thamani yake inatoka na mahitaji makubwa ya watu ni hisa za zamani sana....Ninazo za umoja fund tangu miaka ya 2002.

Thamani ya mfuko ni kiwango cha pesa zilizowekezwa ...Kuna mda mtu anataka kutoa billion kadhaa ina maana kuna nyingi zitakuwa zinauzwa zikigonjea kununuliwa.
 
Sasa ni mida muafaka Financial Literacy ianze kufundishwa mashuleni..Yaani babakako miaka yote hiyo alikuwa anakaa ofisini sasa kazeeka ndio mnataka muanze kufanya biashara? Wewe ni mfanya biashara au umewahi kufanya biashara yoyote ile? Ninachoweza kukushuri ni hiki, kama alishajenga nyumba na ana mahala pazuri pa kuishi nasi hako ka hela kake mwambie akatunze tu sehemu salama wakti anafikiria jambo la kufanya ambalo yeye mwenyewe analijua kwa uzuri na ufasaha ila asikurupuke kuwekeza kwenye kitu asichokijua. Kitu kingine anachoweza kufanya ni kuendelea na shughuli ile alokuwa anafanya kabla ya kustaafu ila sasa afanye mwenyewe kama mtu binafsi.
 
Salamu ziwafikie wana Jf wenzangu.
Ninaomba msaada katika uwekezaji wa fedha benki.

Ni hivi mimi nina mzee wangu anayetarajia kustaafu mwaka huu. Sasa kama kijana wake wa pekee na anayeniamini ameniomba nimsaidie namna ya kuwekeza fedha zake kwa ajili ya kufurahia uzee wake.

Sasa mimi cha kwanza kabla ya mengine ninachotamani ni kwamba mzee awekeze fedha zake benki ili ikiwezekana kila mwisho wa mwezi awe kama anapokea mshahara wa kati ya 500,000-700,000 za kitanzania huku ile hela yake aliyohifadhi ikibaki kuwa dhamana yake katika uwekezaji na akiitaka aichukue muda wowote ule.

Nimefatalia kwa umakini sana humu JF uwekezaji wa namna hii mfano, hisa, UTT, fixed account n.k. lakini bado sijapata kile ninachokifikiria kuwa afungue tu akaunti awekeze hela huko kisha kila mwezi awe anavuna kiasi tajwa hapo juu. Sasa maswali yangu ni haya hapa chini.

i. Je Kuna uwezekano wa kupata akaunti ya kuwekeza labda tuseme milioni 20 au 30 za kitanzania na mtu akapata mavuno ya laki 5 Kila mwezi?

ii. Kama ni ndio je ni kiasi gani kinaweza kuleta mavuno ya laki 5 kama jibu ni sio je ni akaunti gani naweza kuwekeza angalau kupata kiasi kizuri kwa mzee kwa kila mwezi?

iii. Je ni benki gani nzuri itafaa Kwa uwekezaji huo kwa ajili ya mzee?

N.B: Kumbuka sitamani uwekezaji mwingine zaidi ya huo hapo juu. naomba ushauri ujikite katika muongozo huo. Natanguliza shukrani zangu.

Soma Ushauri kwa wastaafu na wanaopata hela nyingi kwa mkupuo
Ajenge nyumba za kupangisha,hazina stress,wastaafu biashara hawawezi
 
Awekeze UTT hapo ndio atapata faida
 
Mwahishe utt amiss chap kwa haraka
 
Ni bora atafute hata nyumba ya kununua zile za urithi ama zile za watu waliokopa bank wakashindwa marejesho waliyokopa,kisha apangishe naona uwekezaji wa nyumba ni mzuri sana ijapokuwa faida itachukua muda mrefu kurudi ila ni uwekezaji ulio mzuri sana
 
Basi kiinua mgongo sio kazi yake kuwekeza.

Kama hukupata uwezo au muda kuwekeza ukiwa kazini basi tumia kiinua mgongo taratiiiiiibu kwa kula mdogo mdogo hadi utakapokufa
Haya ni mawazo yako. Kila mtu ana uhuru wa kutumia fedha yake kwa kadiri anavyoona inapendeza. Kila mtu ana plan ya maisha yake. Unanacho ni sawa kwako mwingine anaona umekosea.
 
Kosa limeshafanyika tayari. Uwekezaji huwa unafanywa mtu akiwa kazini, akiwa na nguvu na kujifunza, baada ya kustaafu ni ufatiliaji mdogo tu sana sana na kuongeza mtaji. Unaposema mzee wako awekeze saa hizi ni uongo.

Shida ya wastaafu wengi huwa wanataka akipata kiinua mgongo ndo awekeze, this is not right. Na bahati mbaya wanaowadanganya wastaafu wengi ni watoto wao, au ndugu na kimsingi ndio wanaotaka kutoka kwa kupitia hicho kiinua mgongo.

We jamaa uliyeandika hapa, tafuta kazi ya kufanya achana na hela za huyo mzee. Huyo mzee anahitaji counseling tu ili hizo hela zake azile Pole Pole hadi atakapokufa. Mwacheni huyo mzee na hela zake tafuteni zenu. Mtu kapambana kajifanyia kazi zake miaka 30+ anastaafu mnaibuka mnataka kuanza kumshauri namna ya kuishi na namna ya kutumia hela zake.

Hela ya kustaafu ni hela ya kujikimu sio ya uwekezaji. Inaaminika mtu anapostaafu ameshamaliza kusomesha, ameshamaliza kujenga pa kuishi so hela yake ni ya kula tu.
Aisee huu ujumbe wako ni mzuri sana uwekewe lamination
 
Sasa ni mida muafaka Financial Literacy ianze kufundishwa mashuleni..Yaani babakako miaka yote hiyo alikuwa anakaa ofisini sasa kazeeka ndio mnataka muanze kufanya biashara? Wewe ni mfanya biashara au umewahi kufanya biashara yoyote ile? Ninachoweza kukushuri ni hiki, kama alishajenga nyumba na ana mahala pazuri pa kuishi nasi hako ka hela kake mwambie akatunze tu sehemu salama wakti anafikiria jambo la kufanya ambalo yeye mwenyewe analijua kwa uzuri na ufasaha ila asikurupuke kuwekeza kwenye kitu asichokijua. Kitu kingine anachoweza kufanya ni kuendelea na shughuli ile alokuwa anafanya kabla ya kustaafu ila sasa afanye mwenyewe kama mtu binafsi.
Kiongozi nashukuru sana Kwa mawazo tukuka. Moja, mimi ni mfanyabiashara mdogo ninayejitafuta na bado sijajipata vizuri kwa namna ya ndoto yangu ninayotaka. Hivyo bado napigania ndoto yangu katika ulimwengu huu wa biashara.

Pili, mzee wangu mbali ya kuwa ni mtumishi anayejiandaa kustaafu, katika maisha yake amekuwa ni mtu aliyejihusisha sana na kilimo hasa kilimo cha mahindi na maharage Kwa asimilia kubwa. Katika hili ana uzoefu wa kutosha.

Sasa Kwa kuwa Mimi pia najihusisha na biashara hii ya mazao na Nina uzoefu kidogo nilitaka mzee atumie kiasi kidogo tu Cha mafao yake tuseme labda million 5 kuwekeza kwenye biashara hii. Ni suala la kumfundisha jinsi ya kutoka kufanya kilimo cha chakula kwenda kilimo cha biashara kitu ambacho atakiweza sana. Mfano mdogo ni kumwambia achukue mil. 1 anunue mazao kisha nimuoneshe soko lilipo akauze Kwa bei nzuri apate faida yake

Sasa mimi Kwa kutambua changamoto zilizoko katika biashara na kwa kuangalia umri wa mzee nilifikiria achukue kiasi pia cha fedha hata kama ni milioni 30 au 40 ahifadhi benki awe kama anaendelea kupokea mshahara kila mwezi kwa muda wote wa uzee wake huku sasa akifanya pia hii biashara yake ya mazao ambayo ana uzoefu nao kupitia kilimo.

Hofu yangu ni asichukue hela zote na kuweka kwenye kapu moja bali afanye mgawanyo katika mafungu kadhaa. Kwa sasa nimekuwa na mawazo mawili. Moja awe na akiba benki, na pili abadilishe kilimo chake cha chakula kuwa kilimo cha biashara ambapo Nina uhakika ataweza. Ndio maana nikajitokeza kwenu wakuu kuomba huu ushauri. Asante sana
 
UTT hii mbeleni naona kuna watu watatoa machozi

Sababu hisa zinaweza shuka...vilevile ongezeko na migogoro duniani na hizi pandemic desease
Kunaweza kuleta mtikisiko wa uchumi kidunia
Huo ndo ukweli ambao wengi hawaambiwi
 
Back
Top Bottom