Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo maarufu 'Mzee wa Upako', jana aliwagomea waandishi wa habari kusikiliza hotuba yake ya Ibada ya Krismasi, na kutuma wasaidizi wake wawaondoe waandishi hao.
"Samahani tunaomba muondoke kwani Mchungaji amesema hataki kumuona mwandishi yeyote hapa, hivyo tunaomba muende Makanisa mengine", alisema msaidizi huyo na kuhakikisha waandishi wote wanaondoka eneo hilo majira ya saa sita kasoro mchana.
Lusekelo maarufu 'Mzee wa Upako' hivi karibuni amekuwa akirushiana maneno na baadhi ya waandishi wa habari, baada ya kuandikwa akituhumiwa kuwa mlevi na kutukana hadharani.
CHANZO: HABARI LEO, 26.12.2016.