Mzee wa kichaga

Che Kalizozele

JF-Expert Member
Jul 20, 2008
777
49
Mzee mmoja wa Kichaga ambaye alikuwa mkali
sana kwa binti yake anaamka asubuhi na kutaarifiwa
kwamba binti yake ana mimba!

Mzee wa Kichaga:
"Aisee we Manka,
nakwenda kazini,
nikirudi leo ni lazima uniambie ni nani
kafanya uchafu huu"
Anafoka na kuondoka kuelekea ofisini.

Mchana anapigiwa simu na Mama Manka na
kuambiwa kwamba yule jamaa aliyempa mimba bintiye yupo
nyumbani anamsubiri kwa mazungumzo!
Mzee anachukua panga lake na kulinoa
kabisaaa kwa ajili ya kwenda kumteketeza mwanaharamu
huyo.

Kufika nyumbani mambo yanakuwa hivi:

Kijana aliyempa mimba binti:
Mmmh!!
Mzee ni kweli mi ndiye nimempa mimba binti yako, na kusema

kweli sina mpango wa kumuoa.
Lakini akizaa mtoto wa kiume nitakupa US$ 1 million na ghorofa Kariakoo
kisha nachukua mtoto.
Akizaa mtoto wa kike nakupa US$ 1million na duka Sinza!
Lakini je mzee, ikitokea bahati mbaya mimba hii ikaharibika itakuwaje?

Mzee wa Kichaga:
Aisee babaangu itabidi tu umpe mimba nyingine, hakuna jinsi!
 
Du! Aloo hili rungu zito kweli. Bila shaka aliyelishusha ni Mpare huyu! Mtani wa jadi wa mchaga. Tuendelee hivo hivo ndiyo uzuri wa watanzania. Tunajenga mahusiano. Ungekuwa Burundi ....!
 
Du! Aloo hili rungu zito kweli. Bila shaka aliyelishusha ni Mpare huyu! Mtani wa jadi wa mchaga. Tuendelee hivo hivo ndiyo uzuri wa watanzania. Tunajenga mahusiano. Ungekuwa Burundi ....!

Hizi tamaa jamani zitatuua hizi.
Unauza mtoto (binti) kwa pesa na maduka SINZA NA KARIAKOO??????

............UUUH....... WWIIIIIII AMA KWELI PESA MWANAHARAMUUU!!!!!!!!!!!!
 
hizi tamaa jamani zitatuua hizi.
Unauza mtoto (binti) kwa pesa na maduka sinza na kariakoo??????

............uuuh....... Wwiiiiiii ama kweli pesa mwanaharamuuu!!!!!!!!!!!!

hapana pesa sio mwanaharamu bali wanadamu wenyewe ndio wanaharamu
 
hii ni kweli...wachaga ukiwa na pesa unawatawala utatengewa kitu chako special kanisani,utaitwa mzee hata kama ni kijana,utatukuzwa kama mungu mtu mji mzima....ni tofauti na wahaya wenyewe wanathamini mwenye elimu....
 
Back
Top Bottom