Mzee wa dodoso nahitimisha waxzo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee wa dodoso nahitimisha waxzo

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MKINDE, Sep 10, 2012.

 1. M

  MKINDE Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  KIWANGO CHA ELIMU NA AJRA KWA VIJANA NCHINI TANZANIA

  Wana jamii naombeni tena nafasi nipande jukwaani ili nitoe mada yangu ya leo…..
  Wengine hukata tamaa ya kusoma na kuendelea mbele kielimu pale wanapomwona kijana mwenzao mwenye elimu ya Degree au Masters akizunguka zunguka mtaani bila kuwa na kazi ya kueleweka kutokana na kiwango cha elimu alichonacho. Kuna wakati mwingine wazo la kutokusoma huwa linaweza kutawala ndani ya ubongo wa kijana pale anapomwona mwenzie ambaye hakusoma akimiliki nyumba ya kifahari na biashara kubwa ambayo humwendeshea maisha yake ya kila siku..Kuna vijana wengine huingia gharama ya kukodisha magari ya kifahari au nyumba za kifahari ili tu waondoe ile aibu ya kukaa nyumbani kwao huku akiwa na elimu ambayo angeweza kupata kazi na kuweza kuendeleza maisha yake pasipo msaada kutoka kwa wazazi, .Naomba nianze mada.
  Ajira kwa vijana limekuwa ni tatizo kubwa sana hapa nchini kwetu mpaka kupelekea vijana wengi kujutia kiwango cha elimu walizonazo nahii hupelekea vijana wengi kuacha kufanya kazi kutokana na fani walizo nazona kuingia katika fani ambazo hawana elimu nazo. Leo namleta kwenu kijana Julius ambaye ni muhitimu wa Degree ya kwanza katika chuo kikuu cha Dar es salaam alikuwa anasoma fani ya JIOLOJIA (GEOLOGY), Julius baada ya kuhitimu fani hiyo alijitahidi kutafuta kazi katika wizara nyingi hapa Tanzania bila mafanikio yoyote ndipo aliamua kutafuta njia mbadala na kuingia katika ujasiriamali, Julius ambaye ni kijana wa mtaani kwetu hakuna ambye atathubutu kusema yeye ni fisadi, freemason au majina mengine mengi yanayopendwa kutumiwa na vijana wengi wanapoona maendeleo ya mtu yanaposhamiri kwa kasi. Julius alianza kwa biashara ya kuuza vitenge mtaani kwetu, mwanzo alianza kwa kutembeza vitenge 12 ambavyo kila vitenge vitatu alikuwa anauza kwa sh.18,000= hadi sh.20,000/=, mwanzo tulikuwa tunamcheka na kumdharau kutokana na kazi anayofanya na elimu aliyonayo. Julius hakukata tamaa, alianzisha biashara ya kuuza vocha na baadaye aliuza line za mitandao mbalimbali mfano: Tigo, Vodacom na Airtel. Huyu ni Julius mwana JIOLOJIA aliyeangukia kwenye ujasiria mali. Baada ya kuuza vocha, line baadaye aliomba mkopo kutoka benki ya XXXXX ambao alifanikiwa kufungua ofisi yake ndogo ambayo ilikuwa inatoa huduma ya M-PESA na TIGO PESA, maisha ya Julius yanaanza kubadilika na kuanza kuwa ya kisomi zaidi. Baada ya kuanzisha M-PESA na TIGO PESA sasa ofisi inakuwa kubwa na anaamua kutoa ajira kwa kijana mwenzake ambaye alikuwa ni rafiki yake wa hapa mtaani kwetu.
  Baada ya mwaka mmoja Julius anafanikiwa kurejesha mkopo wote aliokopa kule Benki na sasa anaendelea na bishara yake . Julius sasa ni mfanyabiashara anaye fahamika sana mtaani kwetu. Biashara yake ya TIGO PESA na M-PESA inampatia mahari na kumpatia mke mwema ambaye wanaanzisha maisha yao ya ndoa. Ni funzo zuri sana tunalipata kwa kijana mwenzetu, elimu anayo tena yakutosha ila tatizo kubwa ni ajira, aliweka elimu yake na aibu yake pembeni kisha akaamua kuwa mjasiria mali hatimaye matunda yake akayaona. :Vijana wenzangu ajira za maofisini nchini kwetu limekuwa ni gonjwa ambalo limekosa dawa kwa miaka mingi, kuna siku niliomba kazi katika ofisi fulani ambayo ilikuwa inahusika na mambo ya madini nilishangaa na kustaajabu baada ya kuambiwa kilichonikosesha kazi katika ofisi ile eti ni ikwa sababu sikuandika dini yangu na kabila langu katika CV yangu(Curriculum Vitae)! Hapa ndipo nilipogundua kumbe ile dhana ya udini na ukabila katika ajira bado ipo nchini kwetu;:(Alisema Julius) Pia aliongeza: Vijana wengi huwa wanapo hitimu tu elimu zao basi hujipangia kiasi cha fedha ambacho wangependa kuanza kupokea pindi tu waanzapo kazi, hili ni kosa kubwa sana vijana wenzangu na ni vijana wenzangu wengi sana walikosa ajira na bado nawaona mtaani wakiwa hawana uelekeo mzuri wa maisha, ni vizuri ukajishusha na ukiendelea kuamini yakwamba ipo siku nawe utapandishwa cheo tena kuwapita wao, katika maisha usiogope kudharaulika kwani yule anayekudharau naye alishadharaulika kabla yako hivyo mwombe Mungu akupe ujasiri na uweze songa mbele.(Julius alimaliza).
  HAYA WANA NDUGU TUUFANYIE KAZI USHAURI WA KIJANA MWENZETU JULIUS
  ***********************MKINDE****************
  .Mzee wa kudodosa niliishia hapo kuendelea kumdodosa kijana Julius.
   
Loading...