Mzee Sumaye azidi kuteseka. Je, atarudi CCM?

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,498
Reaction score
28,720
"Mmeamkaje? Kwangu mambo siyo mazuri. Mtakumbuka baada tu ya kuingia upinzani serikali ilitishia muda mrefu kuchukua mashamba yangu bila sababu za msingi, hata wakati wa kampeni baadhi ya viongoz wa ccm walitamka hadharani kuwa huyu dawa yake ni kumnyang'anya mashamba yake. Shamba la mabwepande ekari 33 wameagiza wiki hii halmashauri iligawe kwa wavamizi na wengineo.

Jana nimepokea barua kuwa shamba la mvomero ekari 326 limetwaliwa na rais na sitakiwa kukanyaga hapo. Shamba hilo lina majengo, mazao, mashine mbali mbali, visima virefu vya maji, umeme na mifugo mchanganyiko zaidi ya 200. Kisingizio shamba halijaendelezwa! Shamba lenye vitu vyote hivyo halijaendelezwa??

Mbaya zaidi katika kupinga dhamira hizo nilifungua kesi mahakama kuu kwa mashamba yote na mahakama zimeweka zuio la kutokuingiliwa mashamba hayo mpk mashauri ya msingi yatakapoamuliwa.

Lakini wameshaamua kwa hiyo mahakama hazina kazi. Utawala huu haufuati sheria ni udikteta mtupu! Kuna mwana ccm moja alisema "tutamfilisi mpk atakapotembelea ndala ndo atakumbuka kurudi ccm."

Hilo litawezekana kama Mungu huyu ni wa ccm. Ccm sirudi pamoja kuwa najua nitateseka na familia yangu! Kisasi hiki mimi sitakiweza namwachia Mungu ndiye atakayetufuta machozi mimi na familia yangu."

Fredrick Tluway Sumaye.
Waziri Mkuu Mstaafu
August 12, 2017

Note: Jana niligusia Kuhusu hujuma, dhuluma na madhila mbali mbali wanayopitia Viongozi na wanachama wa Upinzani. Nilieleza namna gani Viongozi wetu akiwamo Freeman Mbowe wanavyoteswa kwa namna mbali mbali kuanzia kwenye kuharibiwa au kunyang'anywa mali zao na hata kuwekwa gerezani.

Nilisema Unapoamua kuwa mpinzani Tanzania ni lazima kwanza ujikane nafsi yako kisha ujitwishe msalaba wako. Mbowe angekuwa ana roho ya ubinafsi ya kuangalia maslahi yake na familia yake leo angekuwa CCM.

Hebu leo TUJIKUMBUSHE kidogo na kutafakari DHULUMA ambazo amefanyiwa Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye tangu alipoondoka CCM na kujiunga na CHADEMA.

Jipeni moyo ulimwenguni mnayo dhiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karma inaweza kukuacha wewe ikapiga watoto wako,tujifunze kuwatendea watu yaliyo mema. Sijui alipokuwa Ccm alitenda mema au mabaya mangapi na sijui kama yanayomkuta ni haki yake ama laa!! Chamuhimu ajitetee yeye na kisha taifa maana watz unaweza kuwapigania lkn mwisho wa siku wakakutupa na kukusahau hasa unapopitia magumu. Hatujafundishwa ile hali ya kujaali pale mwenzio anapopitia hali ngumu!! Akumbuke mpaka sasa he is not a hero anyway na tunajua anatafuta upenyo wa kisiasa baada ya kuukosa tangu aondoke Mkapa. Siku za karibuni hata ubunge wamekuwa wakimbania...alitakiwa astaafu siasa abaki na chakula sasa kajiingiza upinzani kusiko na misingi thabiti nayeye siyo MTU mahiri siasani
 
"Mmeamkaje? Kwangu mambo siyo mazuri. Mtakumbuka baada tu ya kuingia upinzani serikali ilitishia muda mrefu kuchukua mashamba yangu bila sababu za msingi, hata wakati wa kampeni baadhi ya viongoz wa ccm walitamka hadharani kuwa huyu dawa yake ni kumnyang'anya mashamba yake. Shamba la mabwepande ekari 33 wameagiza wiki hii halmashauri iligawe kwa wavamizi na wengineo.

Jana nimepokea barua kuwa shamba la mvomero ekari 326 limetwaliwa na rais na sitakiwa kukanyaga hapo. Shamba hilo lina majengo, mazao, mashine mbali mbali, visima virefu vya maji, umeme na mifugo mchanganyiko zaidi ya 200. Kisingizio shamba halijaendelezwa! Shamba lenye vitu vyote hivyo halijaendelezwa??

Mbaya zaidi katika kupinga dhamira hizo nilifungua kesi mahakama kuu kwa mashamba yote na mahakama zimeweka zuio la kutokuingiliwa mashamba hayo mpk mashauri ya msingi yatakapoamuliwa.

Lakini wameshaamua kwa hiyo mahakama hazina kazi. Utawala huu haufuati sheria ni udikteta mtupu! Kuna mwana ccm moja alisema "tutamfilisi mpk atakapotembelea ndala ndo atakumbuka kurudi ccm."

Hilo litawezekana kama Mungu huyu ni wa ccm. Ccm sirudi pamoja kuwa najua nitateseka na familia yangu! Kisasi hiki mimi sitakiweza namwachia Mungu ndiye atakayetufuta machozi mimi na familia yangu."

Fredrick Tluway Sumaye.
Waziri Mkuu Mstaafu
August 12, 2017

Note: Jana niligusia Kuhusu hujuma, dhuluma na madhila mbali mbali wanayopitia Viongozi na wanachama wa Upinzani. Nilieleza namna gani Viongozi wetu akiwamo Freeman Mbowe wanavyoteswa kwa namna mbali mbali kuanzia kwenye kuharibiwa au kunyang'anywa mali zao na hata kuwekwa gerezani.

Nilisema Unapoamua kuwa mpinzani Tanzania ni lazima kwanza ujikane nafsi yako kisha ujitwishe msalaba wako. Mbowe angekuwa ana roho ya ubinafsi ya kuangalia maslahi yake na familia yake leo angekuwa CCM.

Hebu leo TUJIKUMBUSHE kidogo na kutafakari DHULUMA ambazo amefanyiwa Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye tangu alipoondoka CCM na kujiunga na CHADEMA.

Jipeni moyo ulimwenguni mnayo dhiki.

Sent using Jamii Forums mobile app

Waache watesane. Kipindi Sumaye alipokuwa kiongozi kuna watu walipata tabu sana. Hata kuwapora hayo mashamba. Mwache nae akinywee maana nae aliwatesa sana wananchi.
 
Utawala wa Kikwete ulikuwa wa Mpito tu watu wakajisahau wakadhan ile Ni Hali ya kudumu

Wakati wa Jk ilikuwa Kawaida kina Sabodo kwenda hadharan kutangaza kusaidia Chadema Na akitoka hapo Hakuna anaemuuliza wala kumpiga Buti

Akina Hans pope walijitokeza hadharan kusaidia Wapinzani na kuna Wafanyabiashara wakubwa tu wa Kihindi walijitokeza kusadia Chadema wakati wa awamu ya nne lakin Maisha yaliendelea bila usumbufu

Mbowe hakuguswa kabisa Kwenye Vitega Uchumi vyake Na wakati Mwingine alikuwa anapewa Tenda Za Serikal bila ya Shida

Mzee Hashim Rungwe anaweza kueleza vyema yaliyomkuta Kwenye Biashara zake Wakat wa Mzee Mkapa
 
Back
Top Bottom