Mzee Shelukindo asusiwa vikao vya kutembelea jimboni.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Shelukindo asusiwa vikao vya kutembelea jimboni....

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MtazamoWangu, May 25, 2010.

 1. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni wiki ya pili sasa Mh.Shelukindo yuko jimboni Bumbuli akizungukia jimboni na kuongea na wananchi kuhusu utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi n kukagua maendeleo katika maeneo.

  Mh. amekuwa akikumbana na vikwazo vikubwa ikiwa ni pamoja na viongozi wa chama kutompa ushirikiano wa kutosha, baadhi ya maeneo aliyotembelea amejikuta akiongea na watu wachche sana na makatibu wote kutohudhuria vikao vyake pamoja nayeye kuwaomba makatibu wa kata kumuitia wajumbeili kuonana nao, wengi wamekuwa wakihusisha ziara yake na kapeni za ubunge 2010, na kwakuwa wengi hawamuungi mkono wameamua kususia vikao vyako.

  Mh shelikindo anapata upinzani mkubwa baada ya baadhi ya vijana kujitokeza kutaka kugombea nafasi hiyo na kuungwa mkono na wananchi, January Makamba ambaye amejikita sana akiwa na viongozi wanaomtangaza usiku na mchana amekubalika sana na kufikia hatua ya kugawa viongozi, wale wanaomuunga mkono Januari makamba wamekuwa wakigoma kutoa ushirikiano kwa Mh shelukindo ambaye ndiye mbunge wasasa...

  Vita ya ubunge katika jimbo la Bumbuli bado ni ngumu na imefika mahali hata wagombea wameanza kupigana vita, wakati Januari lifikisha barua ya malalamiko dhidi ya Mzee shlukindo na ikapelekea mzee shelukindo kuitwa kwenye kamati yasiasa baadhi ya malalamiko kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na baadhi ya watendaji kuhamishwa au kusimamishwa kazi, lakini barua zote za mzee shelukindo za malalamiko dhidi ya january kufanya kampeni kabla ya wakati na kuvunja kanuni hakuna iliyojibiwa....

  Katika kata ya Mgwashi mwenyekiti a ktibu walisusia kikao cha mbunge na kulaaniwa na wajumbe wengine jambo hilo limetokea Tamota, Baga na Bumbuli...
   
 2. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Nilishawahi kusema hapa JF kuwa hawa wazee wamezoea kurina asali na hawajui wakati gani wa kuacha kurina ili nyuki warejee kwenye mizinga na kuzalisha asali nyingine.
  Kwa vile hawajui au wamelewa kiasi hata timing ya kutoka hawaijui mwishowe ni kuadhirika kwa kuzomewa na wajukuu zao wenyewe na kisha kumuona kila mtu kuwa ni mbaya kumbe mbaya yeye mwenyewe.
   
Loading...