Mzee Pinda kafungua rasmi kampeni za uchaguzi?

Ina maana hayuko huru?

Mkuu hilo mbona liko wazi tu, jaribu kuangalia kama amewahi kusema au kutishia lolote dhidi ya ccm. Simply ni kuwa ameteuliwa kwenye huo ulaji na mwenyekiti wa ccm.
 
Nimemsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu ndugu Kayanza Peter Pinda wakati akitoa salamu kwenye hafla ya kupokea ndege yetu.

Amesema Kanda ya Ziwa ina idadi kubwa sana ya watu ambao ni kama asilimia 20 hivi ya watu wote wa Tanzania.

Akatoa wito wakimchagua Rais kwa wingi wao kwingineko itakuwa ni kujazia jazia tu.

Wajuzi wa mambo sijui kama kampeni zimeruhusiwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwakani.

Au Mzee Pinda kajisahau kidogo. Je sheria za nchi zinaruhusu kampeni kuanza mapema kiasi hiki?

Sent using Jamii Forums mobile app
Anaweza kuchunguzwa ubongo wake kwanza ili tujiridhishe kama yuko sawa kiakili , umri umemtupa sana .
 
Back
Top Bottom