Uchaguzi 2020 Kampeni za Tundu Lissu zaingia rasmi kanda ya Nyasa, Mbeya Mjini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Wakuu natanguliza salamu , baada ya salamu naanza na kuomba radhi kwa usumbufu wetu wa habari zetu za kampeni zinazomiminika kama mvua za masika , hatuna jinsi ni lazima tuhakikishe nchi inakombolewa .

Taarifa ya leo inaonyesha kwamba Mgombea wa Chadema anayepewa nafasi kubwa ya kushinda Urais wa Tanzania Mh Lissu atakuwepo Viwanja vya Ruanda Nzovwe , ambapo atazindua kampeni za kanda hiyo , lakini kubwa zaidi ni kuwataja hadharani viongozi wote wanaohujumu uchaguzi huu na ahadi walizopewa na hata hela walizolipwa .

Leo tukutane Mbeya mjini _muscle_ ( 741 X 640 ).jpg


UPDATES
========

Hodi hodi kanda ya Nyasa (Mbeya, Njombe na Iringa)..!! Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni utafanyika katika viwanja vya Rwandanzovwe jijini Mbeya hii leo. Karibuni tumsikilize Mhe.@TunduALissu akinadi Ilani ya chama chetu

"Kwa vile Mama Samia Suluhu Hassan amesema kwamba askari wa serikali yao wanapiga risasi 3 tu, watuambie hao waliowaleta kwenye nyumba za serikali kuja kunipiga risasi ni kina nani.?" Tundu Lissu

"Watanzania tusikubali kuongozwa na diwani au mbunge ambaye hajapigiwa kura kwenye sanduku la kura"- Tundu Lissu

Mbeya Mbeya Mbeya....

Mwambie huyo Mama hapo atafute kazi nyingine tu, hakuna namna kwa kweli.

"Mama Samia Suluhu Hassan amesema kuna mtu anapiga kelele kwamba amepigwa risasi 16. Ndugu zangu watanzania, mama Samia alikuja hospitalini Nairobi, alikuja kunipa pole. Kama haamini kwamba nilipigwa risasi 16, aseme alikuja kufanya nini Nairobi." Tundu Lissu

"Hatutakuwa serikali ya kisasi, hatutalipa kisasi. Lakini tunataka tufanye upatanishi na maridhiano ya kitaifa. Tutaunda tume ya upatanishi ili yote yaliyofanyika vibaya yasijirudie tena. Watu tusameheane, tujenge nchi yetu" Tundu Lissu

"Magufuli hastahili kuongezewa hata siku moja baada ya October 28 mwaka huu.Tofauti na waliomtangulia, Magufuli amefanya mambo mabaya kuliko marais wote waliomtangulia"- Tundu Lissu

"Hakuna kipindi ambacho watanzania wengi wameuawa kama kipindi hiki cha miaka mitano ya Magufuli. Waliokufa Kilwa, Kibiti, Mkuranga na Rufiji ni zaidi ya 400. Takwimu halisi hazijulikani kwa sababu serikali imekataa kufanya uchunguzi wa watu waliouawa maeneo hayo"- Tundu Lissu


"Miaka mitano ya Magufuli, viongozi wa vyama vya siasa wameuawa kwa namna ambayo haikutokea katika miaka yote. Kwa mfano, viongozi wa CHADEMA, Alphonce Mawazo wa Geita, Daniel wa Hananasif , na wengine wengi wameuawa na hakuna hatua iliyochukuliwa na serikali hii" Tundu Lissu

"Katika miaka mitano hii ya Magufuli, ni nani anayeweza kubisha kwamba serikali hii ilikuwa ni serikali ya wateka nyara.?" - Tundu Lissu

"Rais Magufuli anajinasibu kwamba ni mtu wa dini, hebu atuambie, kwanini anawatesa viongozi wa kiislamu.? Kwanini mashehe wapo magerezani hapa Mbeya, kule Arusha na Dar es salaam, kwanini.?"- Tundu Lissu


"Tusije tukaruhusu tena kuongozwa au kutawaliwa na watu ambao hatujawachagua. Watanzania, msije mkaruhusu tena kuongozwa na diwani au m/kiti wa kijiji au m/kiti wa serikali ya mtaa au mbunge ambaye hajapigiwa kura kwenye sanduku la kura"-Tundu Lissu

"Taarifa ambazo ninazo ni kwamba kuna watu wanajaribu kuzuia kurusha matangazo yetu live kwenda nchi nzima na dunia nzima. Hata kama watazuia kwenda mubashara, tuna uwezo wa kubeba mkutano wote huu na baadae kuurusha tena kwa marudio dunia nzima ikaiona CHADEMA" Freeman Mbowe

"Tunataka jeshi la polisi Dodoma liwaachie huru haraka sana wagombea wetu waliowakamata Dodoma na haki ipate kutendeka. Wasitake kutuingiza katika siasa za visasi"- Freeman Mbowe

"Kwahiyo nawakaribisha TBC, nawakaribisha waandishi wa habari wa vyombo vyote waripoti matukio kama yalivyo. Waache kukatiza na waache kutuchagulia maneno ya kuzungumza " Freeman Mbowe

"Rais Magufuli anajinasibu kwamba ni mtu wa dini, hebu atuambie, kwanini anawatesa viongozi wa kiislamu.? Kwanini mashehe wapo magerezani hapa Mbeya, kule Arusha na Dar es salaam, kwanini.?"- Tundu Lissu
Leo tukutane Mbeya mjini _muscle_ ( 741 X 640 ).jpg
Muda huu Mbeya wako tayari kwa uzinduzi wa kampeni kwa kanda ya Nyasa, atakuwepo ( 561 X 750 ).jpg


Subpost 5 - Mbeya ( 424 X 640 ).jpg
Subpost 4 - Mbeya ( 424 X 640 ).jpg
Subpost 1 - Mbeya ( 425 X 640 ).jpg
Mbeya ( 640 X 640 ).jpg
Mbeya umetisha ( 480 X 640 ).jpg
IMG-20200905-WA0068.jpg
IMG-20200905-WA0061.jpg
IMG-20200905-WA0062.jpg
IMG-20200905-WA0065.jpg
IMG-20200905-WA0067.jpg
IMG-20200905-WA0056.jpg
IMG-20200905-WA0059.jpg
IMG-20200905-WA0058.jpg
IMG-20200905-WA0057.jpg
IMG-20200905-WA0055.jpg
IMG-20200905-WA0063.jpg


Video : Mapokezi yake mazito yasababisha barabara kuanza kupata nyufa , jionee mwenyewe
Video
 
Wakuu natanguliza salamu , baada ya salamu naanza na kuomba radhi kwa usumbufu wetu wa habari zetu za kampeni zinazomiminika kama mvua za masika , hatuna jinsi ni lazima tuhakikishe nchi inakombolewa .

Taarifa ya leo inaonyesha kwamba Mgombea wa Chadema anayepewa nafasi kubwa ya kushinda Urais wa Tanzania Mh Lissu atakuwepo Viwanja vya Ruanda Nzovwe , ambapo atazindua kampeni za kanda hiyo , lakini kubwa zaidi ni kuwataja hadharani viongozi wote wanaohujumu uchaguzi huu na ahadi walizopewa na hata hela walizolipwa .

View attachment 1559139
Kwanini anatengeneza misururu ya watu huyu tundulisu kwa kipindi hiki cha korona?
Inamaana chadema na nyie mumekubali kuua wanainchi wa Tanzania jamaaniii?
Chadema na tundulisu kwanini mnatengeneza misongamano ya watu huku mkijua korona ipoo??
Au mnaunangana na MAGUFULI anasema korona haipo Tanzania?
Semeni ukweli au nanyie mumeshaunga juhudi za raisi magufuli???
 
Back
Top Bottom