Nimekuwa nikimsikia Mh. Waziri wangu Mkuu Mzee Kayanza Peter Pinda a.k.a mtoto wa mkulima akiuliza wananchi kwamba ni Tanganyika gani wanaitaka maana anayojua yeye ni ile ya miaka 2 yaani inayoanzia kupata uhuru 1962 na kishia muungano. 1964
Mzee leo nimepata nafasi naomba nikujuze Tanganyika tunayoidai ivue koti la muungano.
Katika miaka ya 1885 – 1890 kulitokea wakoloni kiivamia Afrika ndipo Wajerumani wakafaulu kupata eneo katika Afrika mashariki. Eneo hili lilijulikana na German East Africa.
Bendera ya Ma-Governor wa German East Africa (1898-1919)
Baada ya vita ya 1 ya dunia, mwaka 1919 eneo hilo lilinyang'anywa kutoka koloni la Ujerumani, likagawanywa na kupatikana nchi mpya za Rwanda, Burundi na Tanganyika. Wakati Rwanda na Burundi zikiwa chini ya Wabelijiji (Belgians), Tanganyika iliwekwa chini ya usimamizi wa Mwingereza.
Hii ni Bendera ya Tanganyika 1919–1961
Bwana Kayanza Peter Pinda, Tanganyika tunayoizungunzia ni hii iliyoanzishwa mwaka 1919.
Ndiyo hii ambaye muasisi wetu Mwl. JK Nyerere alizaliwa mnamo mwaka 1922, miaka 3 tu baada ya Tanganyika kuwepo.
Ndiyo hii ambayo Musisi wetu Mwl. Nyerere alikulia na kusoma
Ndiyo hii ambayo Mwalimu aliipigania na kumuondoa mkoloni
Ndiyo hii ambayo kupitia chama cha Tanganyika African Association baadae Tanganyika African National Union ya mwaka 1954 vilikuwa vikiipigania kumuondoa mkoloni.
Ndiyo hii iliyopata uhuru tarehe 9 December, 1961.
Tanganyika huru 1961 (Tuitakayo)
Ndiyo hii iliyoungana na Serikali ya Mapinduzi Zanziba mwaka 1964 kuzaa Tanzania
Tanganyika ndani ya Muungano 1964 (Tuuenzi na Kuudumisha bila kuvalisha mtu koti)
Ndio hii ambayo Wananchi kupitia Rasimu ya Pili ya Katiba iliyoadaliwa na Tume ya mabadiliko ya Katiba wanataka ivue Koti la Muungano ijitokeze tuione kama tunavyoiona Zanzibar, iache kujificha, haijaiba cha mtu na haina jinai yeyote.
Mzee Pinda, wewe pamoja na Chama chako hamna haki ya kumbeza Mzee Jaji Joseph Warioba na Tume nzima ya Mabadiliko ya katiba kwakuwa wamewasilisha tulichowatuma kwa mujibu wa sheria.
Kama warundi wanavyo jivunia Urundi wao, Wanyaruanda wanajivunia Unyarwanda wao, na sisi kama wenzao waliotokana na German East Africa tunapaswa kujivunia utanganyika wetu bila haya wala kigugumizi.
Mzee Pinda hii ni historia, kama una uwezo wa kuifuta, tupe mbinu, lakini ukweili ndio huo.
Naomba toka leo baada ya kusoma uzi huu hilo swali lako la kwamba tunataka Tanganyika ipi? Ni Hii ya mwaka 1919 ambayo mpaka sasa ina umri wa miaka 95 na si ile ya miaka 2 unayosema ya 1962 - 1964. Hako ni ka kipande tu ka umri wa Tanganyika.
Napenda kukufahamisha Bwana Pinda kwamba Tanganyika iko palepale, iwe koloni au huru, iwe katika Muungano au la, Tanganyika inaendelea kuwepo. Kuvaa koti la Muungano ni jambo la muda tu, Joto likizidi koti linavuliwa Muungano utaendelea na koti lake, Tanganyika itaendelea na T-shirt yake kama ilivyo kwa Zanzibar.
Kuongelea serikali 3 si uhaini na si kuvunja muungano, nikuuimarisha!
Mungu Ibariki Tanganyika, Mungu Ibariki Zanzibar, Mungu Ibariki Tanzania.