Mzee Mwinyi alituachia PPF Tower, Mkapa katujengea National stadium, Kikwete kaacha Mwendokasi na UDOM, sasa twende na Rais Magufuli

Ila jamani kuna kitu sielewi, kwanini serikali ya Tanzania ikifanya jambo la maendeleo inapongezwa kama vile imefanya hisani na sio lazima?,
Kwani hao viongozi huchaguliwa ili wafanye nini?
Je hizo pesa wanazofanyia miradi mbali mbali zinatoka mifukoni mwao au ni kodi za wananchi?

Unakuta watu wanasifia kuwekewa umeme na maji au kujengewa hospitals na shule,
Come on guys, hizo ni kazi zao ndio maana mliwachagua na sio kama wanafanya msaada, si waliomba hiyo dhamana wakatoa na ahadi, basi ni wajibu wao kutekeleza na wasipotekeleza ndio tulipaswa kuongea na ikibidi kuwaadhibu.

Wake up guys.
 
Hatuzungumzii makaratasi mzee. Tunazungumzia utekelezaji. Kwani mbona kuna miradi ilikuwa ya nyerere. Mradi kama wa Stieglers HP ni wa nyerere, makao makuu dodoma ni wa nyerere. Tunazungumzia utekelezaji na umalizaji wa miradi.

Huyo JK mradi aliomudu ni upi? Tukianza mwendo kasi ule ulisimama. Nauli ilikuwa buku mbili mwanzo mwisho. Majaliwa wa jpm akausimamaia ukaanza kazi na nauli ikawa sh 600.
Airport ile watu walishalipwa billion 500 yote wakati hata mradi haujaanza. Matokeo yake zikaliwa mkandarasi akaacha akidai hana hela. JPM alivyoingia akamchimba biti na mradi umeisha.

Flyover mpaka jk anaondoka hakukuwa hata na nguzo moja.

Miradi mingi ya jk ilikuwa haikamiliki, ikikamilika ipo chini ya kiwango. Kisima cha milioni mbili utaambiwa kimejengwa kwa million 80.

Ijue tanzania ndugu.
Sina kumbukumbu ya mwendokasi kuchaji elfu 2000 kwa route moja ingawa nilikuwa watu wa mwanzo kuipanda. Kumbukumbu niliyonayo ni kuwa mwendokasi ilianza na kuendelea na nauli ya 650 kwa route na siyo 2000 wala 600.

Labda tuweke kumbukumbu sawa, me sipo hapa kulinganisha rais au awamu ipi imefanya nini, na kwa kiwango gani, nachoamini chochote kinachofanywa ni kwa maslai ya taifa na si mtu, iwe amefanya JPM Kikwete n.k. sisi Kama wananchi na wazalendo tunafurahi.

Unaposema hakuna mradi mkubwa ulioratibiwa na awamu ya 4 ya JK kwa 100% unanishangaza Sana, Serikali yetu ni ya kidemocrasia, raisi ana miaka mitano mpk kumi ya kukaa madarakani, ni wazi Kuna Mambo atayaanzisha rais mmj na kuja kumaliziwa na rais mwingine, ndy utaratibu ulivyo, na ndy maana unakuta miradi mingine inakuja maliziwa awamu nyingine, hv hujui kuwa hata uwanja mkubwa wa kwanza mpira wa miguu nchini ulioanza kujengwa kipindi cha Mkapa umemaliziwa kipindi cha JK, au Daraja la kigamboni ambalo lilianza kujengwa awamu ya JK limekuja kuzinduliwa kipindi Cha JPM?. Lkn kaa ukijua kila rais ana vision zake na ana namna anavyopenda Mambo yatokee ktk utawala wake, na hapa kinachoangaliwa ni wazo lilipoanzia na initiatives zilizochukuliwa.

Muhimu la kujua ni kuwa marais wote wanaitakia mema nchi yetu, ila linapokuja suala la maono au vision juu ya namna gani rais fln anataka nchi iwe hapo ndipo inapokuja tofauti. Kuna mengi mazuri Sana ambayo JPM ameyafanya ambayo hayakufanywa na na JK, lkn vilevile kuna mengi mazuri aliyoyafanya JK ambayo pengine yasingefanywa na JPM. Lkn mwisho wa siku Hawa wote ni viongozi wetu na sisi kwa wananchi tunafurahia kwa mazuri wanayoyafanya juu ya nchi yetu bila kuwabagua.
 
Tusimame tujipigepige vifua, maendeleo ni yetu, wao walikuwa wasimamizi tu, kazi tumeifanya sisi.
 
Hatuzungumzii makaratasi mzee. Tunazungumzia utekelezaji. Kwani mbona kuna miradi ilikuwa ya nyerere. Mradi kama wa Stieglers HP ni wa nyerere, makao makuu dodoma ni wa nyerere. Tunazungumzia utekelezaji na umalizaji wa miradi.

Huyo JK mradi aliomudu ni upi? Tukianza mwendo kasi ule ulisimama. Nauli ilikuwa buku mbili mwanzo mwisho. Majaliwa wa jpm akausimamaia ukaanza kazi na nauli ikawa sh 600.
Airport ile watu walishalipwa billion 500 yote wakati hata mradi haujaanza. Matokeo yake zikaliwa mkandarasi akaacha akidai hana hela. JPM alivyoingia akamchimba biti na mradi umeisha.

Flyover mpaka jk anaondoka hakukuwa hata na nguzo moja.

Miradi mingi ya jk ilikuwa haikamiliki, ikikamilika ipo chini ya kiwango. Kisima cha milioni mbili utaambiwa kimejengwa kwa million 80.

Ijue tanzania ndugu.
wewe unaishi wapi nani kakwambia mwendo kasi ulisimama, kama ulisima mabasi yangeanzaje mwaka 2015 na kuzinduliwa 2016,mtasema na Daraja la kigamboni ni Jpm kwa kua ndiye alizindua,Kikwete alikua na uwezo wa kuzindua vyote mwenyewe,alikua na uwezo wa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa TAZARA,UBUNGO INTERCHANGE,SALENDER BRIDGE kwa kua vyote vimeanzishwa na yeye lakini kwa kuzingatia kua serikali ni moja na chama ni kimoja hakuona haja ya kuforce mirandi kuzinduliwa au kuanza kwa papara .Hivyo hivyo miradi kadhaa ya mkapa imemalizika wakati wa JK na kuzinduliwa naye lakini hakukua na kelele na wala hatukuatumia nguvu nyingi kumsifia mtu mmoja bali serikali ilisimama kwa umajumui tofauti na sasa tunavyotaka kuaminidhwa kua nchi ilikua haisongi mbele.Unaweza kusifia vitu vichache na kusahau kua 2015 ilikua tayari na mtandao mkubwa wa barabara za Lami na kwa mji wetu wa Njombe toka barabara za lami za JK hatujapata hata nusu kilomita ya barabara za mitaa.
 
Tunakumbushana tu alama njema zilizowekwa na viongozi wetu wastaafu.

Kiukweli wamefanya mengi ila kwa yale ambayo yanajulikana kona zote za nchi ni hayo machache niliyoyataja hapo juu.

Kwa Dkt. Magufuli hii awamu ya kwanza tu nimeshindwa nianzie wapi maana mambo ni mengi, hapa nipo njia panda ya chuo kulia naona ubungo flyover na kushoto naziona Magufuli hostel.

Nitaendelea.........!

Maendeleo hayana vyama.

Zaidi ya miaka 50 ya uhuru, zaidi ya milioni 50 ya watanzania, hakuna vita iliyopiganiwa ndani ya nchi (Idd amini vita ndani ya Uganda). Jamani kweli ni aibu kutaja viti unavyovitaja. Kama tunashindanisha Marais toka Nyerere mpaka Jpm unaweza kuwa sawa, lakini kama unazungumzia maendeleo kwa ujumla emebugi step.

Vitu kama hivyo nchini Angola hufanywa kwa miaka mitano tu, aibu.

Haya tuendelee kusifia, huku tukiwa nyuma hata kwa nchi za Afrika. Tuwe critical kama tunataka maendeleo......
 
Zaidi ya miaka 50 ya uhuru, zaidi ya milioni 50 ya watanzania, hakuna vita iliyopiganiwa ndani ya nchi (Idd amini vita ndani ya Uganda). Jamani kweli ni aibu kutaja viti unavyovitaja.

Vitu kama hivyo nchini Angola hufanywa kwa miaka mitano tu, aibu.

Haya tuendelee kusifia, huku tukiwa nyuma hata kwa nchi za Afrika. Tuwe critical kama tunataka maendeleo......
Hutaki acha bwashee!
 
Sina kumbukumbu ya mwendokasi kuchaji elfu 2000 kwa route moja ingawa nilikuwa watu wa mwanzo kuipanda. Kumbukumbu niliyonayo ni kuwa mwendokasi ilianza na kuendelea na nauli ya 650 kwa route na siyo 2000 wala 600.

Labda tuweke kumbukumbu sawa, me sipo hapa kulinganisha rais au awamu ipi imefanya nini, na kwa kiwango gani, nachoamini chochote kinachofanywa ni kwa maslai ya taifa na si mtu, iwe amefanya JPM Kikwete n.k. sisi Kama wananchi na wazalendo tunafurahi.

Unaposema hakuna mradi mkubwa ulioratibiwa na awamu ya 4 ya JK kwa 100% unanishangaza Sana, Serikali yetu ni ya kidemocrasia, raisi ana miaka mitano mpk kumi ya kukaa madarakani, ni wazi Kuna Mambo atayaanzisha rais mmj na kuja kumaliziwa na rais mwingine, ndy utaratibu ulivyo, na ndy maana unakuta miradi mingine inakuja maliziwa awamu nyingine, hv hujui kuwa hata uwanja mkubwa wa kwanza mpira wa miguu nchini ulioanza kujengwa kipindi cha Mkapa umemaliziwa kipindi cha JK, au Daraja la kigamboni ambalo lilianza kujengwa awamu ya JK limekuja kuzinduliwa kipindi Cha JPM?. Lkn kaa ukijua kila rais ana vision zake na ana namna anavyopenda Mambo yatokee ktk utawala wake, na hapa kinachoangaliwa ni wazo lilipoanzia na initiatives zilizochukuliwa.

Muhimu la kujua ni kuwa marais wote wanaitakia mema nchi yetu, ila linapokuja suala la maono au vision juu ya namna gani rais fln anataka nchi iwe hapo ndipo inapokuja tofauti. Kuna mengi mazuri Sana ambayo JPM ameyafanya ambayo hayakufanywa na na JK, lkn vilevile kuna mengi mazuri aliyoyafanya JK ambayo pengine yasingefanywa na JPM. Lkn mwisho wa siku Hawa wote ni viongozi wetu na sisi kwa wananchi tunafurahia kwa mazuri wanayoyafanya juu ya nchi yetu bila kuwabagua.
Ulipoanza kupanda mwendokasi ni baada ya serikali kuingilia kati hiyo bei ya 2000 iliyopendekezwa na kina robert kisena ambao ndio walikuwa wamiliki wa mradi.

Ulichosema mwanzo ndio nilichokujibu maana ulichofanya ni kubeza au kutokujua tofauti ya utekelezaji na uongeaji.

Suala la kutofautisha viongozi haliepukiki sababu wote walikuwa na cheo hiko hiko.

Suala la nia njema ni nchi ni kweli kabisa hata JK alikuwa na nia njema tena sana ila alishindwa kuwasimamia watendaji wake.
 
wewe unaishi wapi nani kakwambia mwendo kasi ulisimama, kama ulisima mabasi yangeanzaje mwaka 2015 na kuzinduliwa 2016,mtasema na Daraja la kigamboni ni Jpm kwa kua ndiye alizindua,Kikwete alikua na uwezo wa kuzindua vyote mwenyewe,alikua na uwezo wa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa TAZARA,UBUNGO INTERCHANGE,SALENDER BRIDGE kwa kua vyote vimeanzishwa na yeye lakini kwa kuzingatia kua serikali ni moja na chama ni kimoja hakuona haja ya kuforce mirandi kuzinduliwa au kuanza kwa papara .Hivyo hivyo miradi kadhaa ya mkapa imemalizika wakati wa JK na kuzinduliwa naye lakini hakukua na kelele na wala hatukuatumia nguvu nyingi kumsifia mtu mmoja bali serikali ilisimama kwa umajumui tofauti na sasa tunavyotaka kuaminidhwa kua nchi ilikua haisongi mbele.Unaweza kusifia vitu vichache na kusahau kua 2015 ilikua tayari na mtandao mkubwa wa barabara za Lami na kwa mji wetu wa Njombe toka barabara za lami za JK hatujapata hata nusu kilomita ya barabara za mitaa.
Hujui kitu bwana nenda zako. Kwanza nani kakuambia daraja la kigamboni ni la serikali.

Daraja la kigamboni na chuo cha udom ni vya nssf. Ukipita pale kigamboni wanaichaji hela ni wafanyakazi wa nssf.
 
Mkuu ni nini ambacho huelewi? Una shida binafsi na JK au nini maana sielewi, kama 2000 ilipendekezwa na haijawahi kuwa nauli rasmi, unasemaje kuwa ndy abiria walikuwa wakilipa? Tangu mradi umeanza nauli rasmi ilikuwa 650 period. Sasa Kama walipropose iwe 2000, 1000, 6000 hayo yatabaki kuwa ni mapendekezo tu.
Ulipoanza kupanda mwendokasi ni baada ya serikali kuingilia kati hiyo bei ya 2000 iliyopendekezwa na kina robert kisena ambao ndio walikuwa wamiliki wa mradi.

Ulichosema mwanzo ndio nilichokujibu maana ulichofanya ni kubeza au kutokujua tofauti ya utekelezaji na uongeaji.

Suala la kutofautisha viongozi haliepukiki sababu wote walikuwa na cheo hiko hiko.

Suala la nia njema ni nchi ni kweli kabisa hata JK alikuwa na nia njema tena sana ila alishindwa kuwasimamia watendaji wake.
 
Tunakumbushana tu alama njema zilizowekwa na viongozi wetu wastaafu.

Kiukweli wamefanya mengi ila kwa yale ambayo yanajulikana kona zote za nchi ni hayo machache niliyoyataja hapo juu.

Kwa Dkt. Magufuli hii awamu ya kwanza tu nimeshindwa nianzie wapi maana mambo ni mengi, hapa nipo njia panda ya chuo kulia naona ubungo flyover na kushoto naziona Magufuli hostel.

Nitaendelea.........!

Maendeleo hayana vyama.
Ikulu, na wizara za serikali nzima, Stiglers, standard gauge, meli mpya, daraja la salander, daraja la busisi, ndege, taa za mitaani nk nk mambo ni mengi. Hii ni just awamu ya kwanza tu. Bado tunasubiri awamu ijayo

Hongera sana Jembe JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na mengi mengi mazuri aliyoyafanya JPM haswa suala la nidhamu ktk kila taasisi ya umma na kupunguza mianya ya wizi wa rasilimali za taifa na Aina nyingine za ubabaishaji, ikiwemo pia miradi mbalimbali...Ila Kuna miradi mikubwa umeitaja ilikuwa chini ya JK , mfano fly over zote za Dar, daraja la salander, SGR, Stiegles gorge, na kama Kuna kitu Cha kumkumbuka JK basi ni upanuzi wa uwanja wa kimataifa wa JKN terminal III.
Jk hakuacha hivyo umetaja. Na asingeweza hata angepewa awamu nyingine. Ukitaka ujue kuwa hakuwa na Plan hasa ya fly over, lile daraja la mwendo kasi asingejenga. Coz limeleta shida kidogo kwenye ujenzi wa fly over pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila jamani kuna kitu sielewi, kwanini serikali ya Tanzania ikifanya jambo la maendeleo inapongezwa kama vile imefanya hisani na sio lazima?,
Kwani hao viongozi huchaguliwa ili wafanye nini?
Je hizo pesa wanazofanyia miradi mbali mbali zinatoka mifukoni mwao au ni kodi za wananchi?

Unakuta watu wanasifia kuwekewa umeme na maji au kujengewa hospitals na shule,
Come on guys, hizo ni kazi zao ndio maana mliwachagua na sio kama wanafanya msaada, si waliomba hiyo dhamana wakatoa na ahadi, basi ni wajibu wao kutekeleza na wasipotekeleza ndio tulipaswa kuongea na ikibidi kuwaadhibu.

Wake up guys.
Unaosifiwa hapa ni utekelezaji na aliyetekeleza, kama ni chaguzi tumezifanya Sana, na hiyo pesa ya Kodi tumekatwa Sana katika mishahara na.biashara zetu, madini yetu mikataba imesainiwa sana hakuna tulichokiona zaidi ya kila kukicha tunatembeza bakuli hakuna cha maana tutadanganywa na kimoja basi. Huyu Kodi zetu tunaziona kwa nini watu wasisifie? Hata kama tunapigwa anajua kila na kipofu
 
1. Stiegler's gorge HP
2. SGR
3. Uundwaji wa meli lake victoria, tanganyika na nyasa.
4. Ununuzi wa ndege na upanuzi wa viwanja vya ndege na vya kisasa kabisa.
5. Ujenzi wa miundo mbinu ya kisasa( fly overs, madaraja ya busisi across lake victoria na tanazanite bridge. Pia barabara nane ubungo - chalinze, ujenzi na upanuzi wa barabara za kisasa unaoruhusu magari kupishana hata matatu hivyo kupunguza ajali.)
6. Usambazaji wa umeme kuanzia kwenye tarafa, kata hadi vijiji.
7. Vituo vya afya bwerere. Tena vya kisasa na huduma ya oparesheni ili kupunguza vifo vya uzazi.
8. Miradi ya maji na usambazaji wa maji maeneo mengi.
9. Uboreshaji wa vyuo na sekondari zilizichoka.
10. Wanafunzi kukaa chini imebaki historia.
11. Ufufuaji na usimamizi wa mazao na kumnufaisha mkulima( pamba, mkonge, chikichiki, korosho, ufuta.) Pamoja na uondoaji wa tozo.
12. Usimamizi wa mapato ya serikali uliowezesha serikali kuwa na akaunti moja badala ya 2000.
13. Usimamizi mzuri wa vita ya corona. Hapa kila mtanzania alijua tumeisha. Jamaa alitia ujasiri wa hali ya juu sana.
14. Upigaji na upigwaji kwenye ardhi umepungua kwa asilimia 90.
Mengi sana unaweza kuandika vitabu.
MUNGU mbariki magufuli
 
Tunakumbushana tu alama njema zilizowekwa na viongozi wetu wastaafu.

Kiukweli wamefanya mengi ila kwa yale ambayo yanajulikana kona zote za nchi ni hayo machache niliyoyataja hapo juu.

Kwa Dkt. Magufuli hii awamu ya kwanza tu nimeshindwa nianzie wapi maana mambo ni mengi, hapa nipo njia panda ya chuo kulia naona ubungo flyover na kushoto naziona Magufuli hostel.

Nitaendelea.........!

Maendeleo hayana vyama.
Yaani kwa kikwete umeona mwendokasi na udom tu?
 
Back
Top Bottom