Mzee Mandela apelekwa tena hospitalini

Mzee Mandela apelekwa tena hospitalini

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,073
Reaction score
34,844
121223081806_nelson_mandela_304x171_afp_nocredit.jpg

Mandela apelekwa hospitalini tena

Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela amepelekea hospitalini kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
Taarifa kutoka kwa afisa ya Rais wa Afrika Kusini zimesema kuwa uchunguzi huu ni wa kawaida tu.
Taarifa zinazohusiana

Kwa muujibu wa tovuti ya Urais wa Afrika Kusini, Madaktari wanaomfanyia uchunguzi Mzee Mandela wamesema hakuna haja ya kuwa na tahariku.

Kwa muda mrefu sasa hali ya kiafya ya rais huyo mstaafu imekuwa ni swala la kutia wasiwasi.

Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini kwa siku 18 mwezi wa Desemba mwaka jana kutokana na kutatizwa na mapafu pamoja vijiwe ndani ya kibofu chake cha mikojo.

Taarifa iliyoandikwa kwenye mtandao wa Ofisi ya Rais Jacob Zuma zimeeleza kuwa Mzee Mandela alipelekwa katika Hospitali ya Mjini Pretoria kwa uchunguzi wa kawaida wa ki-afya


Taarifa hiyo imeendelea kusima kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutikana na matatizo yanayoambatana na Umri wake mpevu.


Mzee Mandela alifudumu kama rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 to 1999 na ndiye rais wa kwanza mweusi kuwahi kuitawala nchi hiyo.


Kutokana na juhudi zake za kupigania demokraisa na kupambana na sera za ubaguzi wa rangi nchini humo, Mzee Mandela anatambulika kama Baba wa Taifa nchini Afrika Kusini.

Tangu mwaka 2004 Mzee Nelson Mandela amekuwa hajitokeza hadharani au kushiriki katika shughuli za umma.

chanzo.
http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2013/03/130309_mandela_hospital_machi.shtml

Ahh Mzee Mandela unataka kutuacha Ugua pole Mzee wa Heshima Mungu akupe afya.


 
Maskini mzee Madiba, mmmh, mashavu yameshuka kiasi hiki! Anyway, Mola aziki kukuongeza miaka ya kuishi hapa duniani.
 
Back
Top Bottom