Mzee Malechela ana power gani mpaka amsanue Ndugai ajiuzulu

Wrevta

JF-Expert Member
Jan 18, 2023
1,440
1,720
Kazi iendelee.!
Nimejaribu kutafakari maneno aliyoyatoa Spika wa Bunge Mstaafu Mheshimiwa Job Ndugai, kuhusiana na kile kinachotambuliwa kuwa 'kusanuliwa mapema' na Makamu wa Rais Mstaafu Mheshimiwa John Malechela.

Kisha nikatafakari kwa kujiuliza, huyu Mzee Malechela ana nguvu gani hasa?
Amekwenda nyumbani kwa Ndugai usiku wa saa tatu tena kwa ghafla. Kwa nini alikwenda usiku?

Halafu akaagiza aletewe chai ya rangi tu, kwa nini hakuagiza kitu kingine? Kwa nini chai ya rangi? Mhe. Ndugai aliongelea hili kwa mshangao pia na kustaajabishwa.

How powerful is Mzee Malechela?
Nanukuu baadhi ya maneno,
"Nimekuja kama kaka yako. Nadhani, ni vizuri kesho ukajiuzuru Uspika, na jambo hilo lisikose kufanyika".

Na kwa nini Mhe. Ndugai hakubisha na jibu lake likiwa ni 'sawa' tu?

Na kwa nini Mhe. Ndugai hakumuuliza Mzee Malechela sababu ya kumuambia yale mpaka leo hii?
 
aa.png
 
Ulitaka Ndugai aseme Kila kitu alichoambiwa?
 
Back
Top Bottom