Mzee huyu NOMAAA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee huyu NOMAAA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 26, 2011.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,302
  Likes Received: 22,103
  Trophy Points: 280
  Mzee Huyu Balaa!
  [​IMG]
  Asubuhi huonekana mitaa ya katikati ya jiji la Dar es Salaam akijifanya mlemavu wa miguu akiomba omba, jioni huonekana kweye kumbi za starehe akipata ulabu.

  Mzee mmoja ambaye kwa muda mwingi amekuwa akiishi kwa shughuli za kuombaomba katikati ya jiji la Dar es Salaam , amekuwa gumzo jijini kwani inasadikika kuwa mzee huyo anamiliki nyumba yake huko Kigamboni na imekuwa ni desturi yake ya kuomba ambapo amekuwa akijifanya mlemavu kumbe siyo mlemavu.

  Mzee huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 50 na 60 amekuwa akikaa kwa staili ya aina yake katika makutano ya barabara ya Azikiwe na Samora mbele ya jengo la IPS.

  Ikifika tu majira ya saa nne utamkuta eneo hilo na ukaaji wake hukalia ****** huku miguu yake akiikunjia kwa ndani hivyo wasamaria wema wamekuwa wakimsaidia pesa nyingi wakidhani kuwa ni mlemavu kumbe ni danganya toto.

  Baadhi ya watu tayari wameshaanza kumgundua na kuacha kumsaidia kwani hata wenzake wenye ulemavu wa kweli wamekuwa wakinyimwa msaada kwa madai kuwa wanajifanyisha.

  Kali ya yote mzee huyo akiishajikusanyia pesa za kuombaomba jioni yake huenda kulewa katika vilabu vya starehe.

  Hivi karibuni gazeti moja la kila siku la Tanzania Daima lilichapisha picha zake zilizoonyesha akitembea kwa miguu yake bila ulemavu pia nyingine zikimuonyesha akigida bia kwa raha zake.

  Mbali ya maisha yake ya kuponda mali, mzee huyo pia inasemekana amejenga nyumba kwa kuomba kuomba katika maeneo ya Kigamboni.

  Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaojigeuza omba omba na kujifanya wana ulemavu ili mradi waweze kujikusanyia pesa kilaini.

  Kwa upande mwingine ongezeko la watoto ombaomba limezidi kushamiri nchini hasa ukipita barabara ya Bibi Titi Mohamed eneo la Taasisi ya Eimu ya Watu wazima utakuta jioni na asubuhi wamejilaza katikati ya barabara huku wakiwa wameanika nguo zao kana kwamba ni nyumbani kwao.

  "Mgambo wa jiji na Halmashauri za jiji wameshindwa kudhibiti hali hii lakini wamekuwa wakikimbilia kuwaharibia mali zao wafanyabiashara za matunda wakidai wao ndio wanachafua jiji", alisema mmoja wa wakazi wa jijini la Dar es Salaam aliyehojiwa na Nifahamishe kuhusiana na omba omba jijini
   
 2. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru kwa taarifa Bujibuji! Tutamshughulikia mapemaaaaa! kesho humkuti
   
 3. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Aibu sana, yaani jitu zima na nguvu za kufanyia kazi linazo halitaki kufanya kazi, ila linataka kuomba omba tu .
  Mijitu kama hii ndio ya kuichapa bakora hadi mjini ipaone pachungu.
  Nawakilisha KIKURYA
   
 4. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  huyu mzee ni kero ile mbaya, anajifanya ombaomba kwa gear ya ulemavu ilihali ni mzima kabisa. asubuhi utamkuta Akiba na jioni lazima akae pale IPS kuwatega wafanyakazi..Askari wa jiji mko wapi kumshughulikia mzee huyu.
   
 5. semango

  semango JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  halafu style yake ya kuita huwa noma.yani anaita mpaka mtu unajisikia vibaya usipompa msaada.ila kama ananyumba kigambona mbona huwa anapanda gari za kuelekea mwananyamala?
   
Loading...