Mzee hataki mdogo wangu aoe binti aliyelelewa na Single Mother

Kweli mvi sio busara mzee wako anamtazamo hasi sana kuhusu haya mambo nashukuru Mungu sina mzazi wa fikra potofu kama huyu alafu wapumzisheni hawa wamama mnawazungumzia sana mbona hamuwasemi single father? acheni mfumo dume
 
tatizo la ukosefu wa malezi ya baba "Fatherlessness" ni moja ya janga kuu la dunia kwa sasa kuliko hata hiyo CORONA. Umaskini, mimba za utotoni, ushoga, kujiua, matumizi ya madawa ya kulevya, kushindwa kuendelea na shule ni baadhi ya matatizo yatokanayo na ukosefu wa baba/malezi ya baba.Hii ina maanisha kuwa mtoto aliyelelewa bila ya baba ama baba asiyejishughulisha na malezi anayo nafasi kubwa kuingia katika mojawapo ya hatari hizi.

singo mothers wengi hujitahidi sana kufanya kila kitu kuwafurahisha watoto wao, ila "hakuna kitu cha thamani kwa watoto kama malezi ya wazazi wawili". hii ya kununu kila kitu kwa mtoto, kufanya kila kitu kwa mtoto ni kujifariji kwa singo mother.

Athari za malezi ya mzazi mmoja hayaishii kwa mtoto tu, yanakwenda hata kwenye ndoa. Mwanamke anaye olewa akitoka moja kwa moja kwa wazazi/walezi wake, na mwanamke anaye olewa akiwa ameanza kujitegemea, wa kwanza ni bora kuliko wa pili.
mwanamke anaye olewa akiwa ametoka kwa baba na mama (huyu ni bora) na ambaye anatoka kwa mama pekeyake (huyu si bora) , na ndio hanzo cha ndoa nyingi kuyumba miaka yetu hii.

kwa wale ambao hawajaingia kwenye mfumo huu, fikiria mara mbili mbili. kwa walioko kwenye ndoa linda ndoa yako kama roho yako. Ukishindwa kujifunza kwa kusikia, basi utajifunza kwa maumivu.!
Wanaume mjirekebishe kuepuka majanga zaidi
 
Sijui nikwambie nini ila ngoja nikupe mfano huu:-

1. Classmate wangu alioa Mhaya, mpaka sasa ni miaka 5 wana watoto 2.
2. Kaka yangu ameoa Mhaya mpaka sasa ni miaka 10 wana watoto 3.
3. Boss wangu ofisini ameoa Mhaya na amezaa naye watoto 5.
4. Jamaa yangu wa karibu aliyetia mimba demu wangu miaka 5 iliyopita (ila waliachana)...ana mtoto 1 na mwanamke wa Kihaya wakiwa na miaka 3 kwenye ndoa hivi sasa.

Hebu niletee facts kuthibitisha wahaya wanashida kwenye ndoa.
Wahaya, Wajita na Wapare
 
Hakuna ndoa inafungwa upande wa mama wa mwanamke. Lazima baba wadogo, mashangazi upande wa baba wa mtoto wawepo. Ina maana hiyo bint hana ukoo wake?
Mara nyingine unakuta hawajui kabisa, mama alizalishwa na Jamaa mkoa wa mbali au hata karibu tu ila jamaa akadisappear kabisa au akafariki bila kutambulisha ndugu yake hata mmoja.

Haya yapo sana
 
Mzee wako ana akili sana jivunie sana kuzaliwa na baba kama huyo. Mthamini sana, mjali, muheshim na jitahidi kumfanyia kila aina ya kheri. Siku akitangulia mbele za haki utakuja jua nini alimaanisha.

Narudia tena jivunie sana kuwa na Baba huyo. Huyo dogo acha alie akinyamanza mpe maji akaoge akitoka akojoe alale akiamka atajua kuwa sio kila ndoto ni yakuotwa
 
Wakuu poleni na majukumu

Mdogo wangu wa kiume alileta taarifa za kuoa kwa mzee wetu nyumbani Marangu Mamba Lekura, mkoa wa Kilimanjaro, Binti aliyehitaji kumuoa ni Mwenyeji wa Mkoa wa Bukoba huko

So mzee alipokea swala lake kwa mikono miwili, wakaitwa wazee wengine siku ikapangwa kuelekea nyumbani kwa Binti Bukoba kwa wazazi wake ili kuweka mambo sawa, kilichotokea baada ya kufika huko mzee akawakuta ndugu wa binti upande wa mama yake lanini upande wa mwanaume hajaonekana hata mmoja

Mzee kuona hivyo ikabidi ahoji kuwa ndugu wa binti kuanzia baba yake mzazi na baba zake wadogo hadi shangazi zake wako wapi, anahitaji kuwaona na kuwafahamu, mama mtu akasema kuwa waliachana na baba wa binti mda hivyo yeye ndio kila kitu kwa Binti

Mzee kusikia hivyo akaliamsha popo kuwa hapa hamna cha ndoa wala kuchumbia , akampiga mkwara mdogo wangu kuwa pale sio pa kuowa ataowa majanga hivyo mzee wakaondoka na wazee wenzake kurudi marangu wakamuacha dogo kule kasusa kurudi na wazee

Mzee ana hoja hizi kwa nilivyomsikia mimi

* Anasema kuoa Binti ambaye alikosa malezi ya baba,kutokana na ugomvi kati ya wazazi wake huwa ni majanga

*Mzee anasema kuwa mabinti wengi walioshuhudia kuachana kwa wazazi wao hasa ukute mama ndio alikuwa na majanga basi na wao mbeleni huwa ni wasumbufu vile vile maana mama zo huwajaza sumu kuhusu wanaume

* Mzee anadai familia yoyote unayoenda kuowa baba wa mwanamke lazima awepo hata kama kashafariki basi ndugu wa baba kama baba wadogo wawepo la sivyo yakitokea matatizo huko mbeleni hutokuwa na mtu wa kumkemea huyo binti kama ana majanga, na ndoa haitokuwa na Baraka

* Mzee pia anadai kuwa masingle mother wengi huachwa na wanaume kutokana n matatizo mbali mbali hasa kutokujielewa hivyo huwalea watoto na kuwajaza sumu kuhusu wanaume hivyo binti huwa tayari kashalelewa vibaya na ashaona mama yake ameishi mwenyewe hivyo hata mkipishana kauli kukwambia achana nae aishi mwenyewe haoni tabu

* Pia anadai mabinti wengi wanaolelewa na mama zao tu wakati baba wapo hai, huwa wana matatizo hata ukioa hiyo ndoa haitodumu

Dogo kapagawa, na mzee ndio msimamo wake sijui nyie wakuu wa hapa JF manasemaje mzee yupo sawa?
Shida nyingi tunasababisha sisi wanaume pia, kila kona unamwaga tu mbegu bila malengo
 
Nilishawahi kuchumbia binti toka kwenye familia ya Singo mother, Yakanikuta yakunikuta.

Naungana na hoja ya Mzee yupo sahihi kwa 100%. (Mtoto wa nyoka hawezi kuwa Mjusi)

Ndoa nyingi zinazovunjika kila kukicha, chanzo chake ni mfumo mbovu wa malezi toka kwa wazazi au walezi wetu.
 
Nilishawahi kuchumbia binti toka kwenye familia ya Singo mother, Yakanikuta yakunikuta.

Naungana na hoja ya Mzee yupo sahihi kwa 100%. (Mtoto wa nyoka hawezi kuwa Mjusi)

Ndoa nyingi zinazovunjika kila kukicha, chanzo chake ni mfumo mbovu wa malezi toka kwa wazazi au walezi wetu.
Pia Kwa mtoto wa kiume aliyelelewa na Single Mother ni taabu zaidi. Yupo jamaa (Mpare) kaoa majuzi mke kapunguzwa kazini jamaa kaanza kumnanga wewe wadada wenzako wanaendesha magari hapa mjini wewe mbona umezubaa tu. Ku-trace historia, Mama alikua anapigwa miti na vijana wa mtaani mpaka anastaafu kwenye taasisi Maarufu jijini
 
Back
Top Bottom