LICHADI
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 4,124
- 11,113
Wakuu poleni na majukumu
Mdogo wangu wa kiume alileta taarifa za kuoa kwa mzee wetu nyumbani Marangu Mamba Lekura, mkoa wa Kilimanjaro, Binti aliyehitaji kumuoa ni Mwenyeji wa Mkoa wa Bukoba huko
So mzee alipokea swala lake kwa mikono miwili, wakaitwa wazee wengine siku ikapangwa kuelekea nyumbani kwa Binti Bukoba kwa wazazi wake ili kuweka mambo sawa, kilichotokea baada ya kufika huko mzee akawakuta ndugu wa binti upande wa mama yake lanini upande wa mwanaume hajaonekana hata mmoja
Mzee kuona hivyo ikabidi ahoji kuwa ndugu wa binti kuanzia baba yake mzazi na baba zake wadogo hadi shangazi zake wako wapi, anahitaji kuwaona na kuwafahamu, mama mtu akasema kuwa waliachana na baba wa binti mda hivyo yeye ndio kila kitu kwa Binti
Mzee kusikia hivyo akaliamsha popo kuwa hapa hamna cha ndoa wala kuchumbia , akampiga mkwara mdogo wangu kuwa pale sio pa kuowa ataowa majanga hivyo mzee wakaondoka na wazee wenzake kurudi marangu wakamuacha dogo kule kasusa kurudi na wazee
Mzee ana hoja hizi kwa nilivyomsikia mimi
* Anasema kuoa Binti ambaye alikosa malezi ya baba,kutokana na ugomvi kati ya wazazi wake huwa ni majanga
*Mzee anasema kuwa mabinti wengi walioshuhudia kuachana kwa wazazi wao hasa ukute mama ndio alikuwa na majanga basi na wao mbeleni huwa ni wasumbufu vile vile maana mama zo huwajaza sumu kuhusu wanaume
* Mzee anadai familia yoyote unayoenda kuowa baba wa mwanamke lazima awepo hata kama kashafariki basi ndugu wa baba kama baba wadogo wawepo la sivyo yakitokea matatizo huko mbeleni hutokuwa na mtu wa kumkemea huyo binti kama ana majanga, na ndoa haitokuwa na Baraka
* Mzee pia anadai kuwa masingle mother wengi huachwa na wanaume kutokana n matatizo mbali mbali hasa kutokujielewa hivyo huwalea watoto na kuwajaza sumu kuhusu wanaume hivyo binti huwa tayari kashalelewa vibaya na ashaona mama yake ameishi mwenyewe hivyo hata mkipishana kauli kukwambia achana nae aishi mwenyewe haoni tabu
* Pia anadai mabinti wengi wanaolelewa na mama zao tu wakati baba wapo hai, huwa wana matatizo hata ukioa hiyo ndoa haitodumu
Dogo kapagawa, na mzee ndio msimamo wake sijui nyie wakuu wa hapa JF manasemaje mzee yupo sawa?