Unajua maswali ya namna hiyo ni kutaka kujenga hoja kuwa Karume hakukubali muungano na Nyerere alilazimishwa.Kakke, Nguruvi3, abdulahsaf, takashi, Jasusi,
..binafsi nimesikitishwa na quality ya maswali waliyokuwa wakiuliza, haswa Jussa.
..Jussa alimuuliza Mzee Moyo kama kuna wakati Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume walikuwa hawaongei. Binafsi sijui suala hilo litamsaidia vipi Mzanzibari na Mtanganyika wa kawaida.
..Kwa hapa tulipofika nadhani wanasiasa na wanasheria wangekaa pembeni. badala yake mjadala wa muungano uchukuliwe na watu wa taaluma na kada nyingine kama WACHUMI, WAFANYABIASHARA, etc etc.
Kakke, takashi, Nguruvi3, abdulahsaf,
..naona hawa waheshimiwa wanapenda sana kulalamika.
..Jussa alikuwa mbunge ktk bunge la muungano, nini kilimzuia kupeleka hoja zake kuhusu kero za muungano?
..zaidi, Jussa ni mjumbe wa baraza la wawakilishi, je, nini kimemzuia kuwasilisha hoja ya kutangaza mgogoro wa muungano?
..mimi nadhani hawa wameridhika na hii nafasi yao ya kuwa walalamishi siku zote.
Waswahili walisema mavi ya kale hayanuki!
Mh Mzee Moyo Muuasisi wa Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar
VIDEO- MUUNGANO NAUJUWA KAMA JINA LANGU ‘HASSAN NASSOR MOYO' | Mzalendo.net Part 1
VIDEO- MUUNGANO NAUJUWA KAMA JINA LANGU ‘HASSAN NASSOR MOYO' 2 | Mzalendo.net Part 2
VIDEO- MUUNGANO NAUJUWA KAMA JINA LANGU ‘HASSAN NASSOR MOYO' 3 | Mzalendo.net Part 3
www.mzalendo.net
View attachment 60472
Mzee Moyo(ambae alikuwa waziri wa sheria ktk Serikali ya Marehemu Karume na ni miongoni waasisi wa muungano wachache waliobakia huko Zanzibar) amkana Ali Ameir asema si Muasisi wa Mapinduzi wala si
Muasisi wa Muungano
Asema yupo tayari kurudisha kadi ya CCM
''Hawa Wana CCM wanaodai kuwa turudishe kadi za CCM ni wana CCM uchwara hakuna mwana CCM kindakindaki aliedai sisi turudishe kadi za CCM'' alisema Mzee Moyo huku akiendelea kusema kuwa Ali Ameir si muasisi wa Mapinduzi wala si Muasisi wa Muungano na hajawahi kuwa hata Memba wa Baraza la Mapinduzi''
Nao Vijana wa Umoja wa Kitaifa na Wanafunzi wa Vyuo Vikuu walimuhakikishia Mzee Hassan Nassor Moyo kuwa wapo wapamoja nae na kama atarudisha kadi ya CCM nao watarudisha kadi hizo na kumfata atakapo elekea.
Tayari Vijana wa Umoja wa Kitaifa wamekwisha towa tamko lao la indhari dhidi ya wana CCM wanaowakaripia na kuwatukana Wawakilishi pamoja na Wana CCM wanaotowa mawazo ya Muungano wa Mkataba na kuonya kuwa hali hiyo itahatarisha mchako wa Katiba Mpya.
Kumbe bado wanautaka muungano............."tuwe na muungano wa mkataba" mara "Urais wa muungano wa kupokezana" n.k
Mkuu JokaKuu,
Hayo malalamiko itafika wakati yatakua katika level nyengine...Masuala ya Muungano yalikua yanaogopwa kuzungumzwa hadharani ,lakini leo yana zungumzwa ...Kuna kila dalili za kua hii nchi itakumbwa na balaa la kujitakia...Wenye macho haambiwi tazama.
Kakke, Nguruvi3, abdulahsaf, takashi, Jasusi,
..binafsi nimesikitishwa na quality ya maswali waliyokuwa wakiuliza, haswa Jussa.
..Jussa alimuuliza Mzee Moyo kama kuna wakati Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume walikuwa hawaongei. Binafsi sijui suala hilo litamsaidia vipi Mzanzibari na Mtanganyika wa kawaida.
..Kwa hapa tulipofika nadhani wanasiasa na wanasheria wangekaa pembeni. badala yake mjadala wa muungano uchukuliwe na watu wa taaluma na kada nyingine kama WACHUMI, WAFANYABIASHARA, etc etc.
Joku kuu.
Nafikiri waZnz wapo huru kujadili na hata kufanya makongamano na mihadhwara kuusasambua muungano na kuweka bayana zake. Somo hili limewaweka pazuri waZnz kuelewa madhwira ya uvundo wa muungano huo na ndio maana uelewa wao ndio unaotia khofu jirani zao wa Bara.
Tgk wamekuwa hakuna forums za kuzungumza ikiwemo makongamano na semina kuilimishana kuhusu faida na khasara za muungano kwa waTgk. Kukosekana kwa ilmi hii kwa raia wa Tgk ndio maana wamekuwa wakitumika katika kupitisha katiba pendekezwa.
Kwa mtazamo mdogo tu utaona Serikali ya JMTz inakhofia Znz katika kupitisha katiba pendekezwa lakin kwa upande wa Tgk wanaona itakuwa kama kumsukuma mlevi.
Mimi ningeshauri Tgk waache uoga na kuwa wawazi katika kujadili muungano na kupeana ilmu za muungano ili kuondosha malalamiko na manung'uniko yanayoletwa na raia wake kuwa wanaumizwa na muungano lakin bado wanaung'ang'ania muungano huo.
Tuwe wawazi.
..umesema kweli.
..sisi wa-Tgk hatuna uelewa mpana kuhusu muungano kama wenzetu wa-Znz.
..huku Tgk vita vya ufisadi ndiyo hoja yenye mashiko kuliko suala la muungano.
Anaetaka kutoka atakuja na sababu nyingi tu, huo mkataba ukiisha akikataa kusaini mkataba mpya inamaana ameshatoka.Tunazunguka mbuyu, muungano wa mkataba! mambo gani yawe ya mkataba?
Ni Kheri Nyerere na Karume wange weka sahihi mkataba wa miaka 99, ikiisha hiyo watu wakae chini kuutafakari upya muungano...huyu anapoteza muda wa watu tu.
..muungano wa mkataba ndiyo kitu gani?
..mbona Nyerere na Karume walisaini mkataba??
Duh...!.Mwanasiasa mkongwe na mwasisi wa Mapinduzi Zanzibar, Hassan Nassor Moyo amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mkoani Tanga