Mzee Hassan Nassor Moyo: Kauli yake juu ya Muungano na hatma ya Uanachama wake ndani ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Hassan Nassor Moyo: Kauli yake juu ya Muungano na hatma ya Uanachama wake ndani ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mkataba, Aug 1, 2012.

 1. m

  mkataba Senior Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  moyo.png
  Mzee Moyo(ambae alikuwa waziri wa sheria ktk Serikali ya Marehemu Karume na ni miongoni waasisi wa muungano wachache waliobakia huko Zanzibar) amkana Ali Ameir asema si Muasisi wa Mapinduzi wala si
  Muasisi wa Muungano


  Asema yupo tayari kurudisha kadi ya CCM


  Awataka Vijana kuendelea na harakati za ukombozi wa nchi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

  Mzee Hassan Nassor Moyo leo amefanya mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Rumaisa Hotel Malindi Mjini Zanzibar, kujibu hoja mbalimbali zilizo zagaa nchini.

  Katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Vijana wa Umoja wa Kitaifa na wanafunzi wa Vyuo Vikuu Mzee Moyo alielezea kuwa msimamo wake anaouonesha sasa si kwa sababu kama Serikali imemtenga kama inavyovumishwa na baadhi ya watu.

  Aliwataka vijana waendelee na harakati za ukombozi wa nchi kwani wao si wa mwanzo kuendesha harakati za ukombozi wa nchi.

  ''Fujo hamkuzianza nyinyi vijana vujo tulizianza sisi toka 1970'' alisema Mzee Moyo huku akishangiriwa na vijana.

  Alisema vijana wana haki ya kuuhoji Muungano na wala yeye hawezi kuwazuwiya kwani wamewasomesha wao wenyewe ili kuleta maendeleo ya taifa hili.

  Akijibu maswali yaliokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari Mzee Moyo alisema yeye ni Mzaliwa wa Zanzibar na hajapata kuomba uraiya wa Zanzibar ila wapo wana CCM hawajazaliwa Zanzibar na wameomba uraiya wa Zanzibar mwaka 1963.

  Katika maelezo yake ya awali Moyo alisema hawezi kuyumbishwa na CCM ati kwa kudai Mamlaka kamili ya Zanzibar na kudai Muungano wa Mkataba.

  ''Hawa Wana CCM wanaodai kuwa turudishe kadi za CCM ni wana CCM uchwara hakuna mwana CCM kindakindaki aliedai sisi turudishe kadi za CCM'' alisema Mzee Moyo huku akiendelea kusema kuwa Ali Ameir si muasisi wa Mapinduzi wala si Muasisi wa Muungano na hajawahi kuwa hata Memba wa Baraza la Mapinduzi''

  Nao Vijana wa Umoja wa Kitaifa na Wanafunzi wa Vyuo Vikuu walimuhakikishia Mzee Hassan Nassor Moyo kuwa wapo wapamoja nae na kama atarudisha kadi ya CCM nao watarudisha kadi hizo na kumfata atakapo elekea.

  Tayari Vijana wa Umoja wa Kitaifa wamekwisha towa tamko lao la indhari dhidi ya wana CCM wanaowakaripia na kuwatukana Wawakilishi pamoja na Wana CCM wanaotowa mawazo ya Muungano wa Mkataba na kuonya kuwa hali hiyo itahatarisha mchako wa Katiba Mpya.
   
 2. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Huyu Mzee wetu na yeye MUAMSHO nini?
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Tunazunguka mbuyu, muungano wa mkataba! mambo gani yawe ya mkataba?
   
 4. m

  mkataba Senior Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape na huyo mpe kadi nyekundu ikiwa wewe ni kidume.
   
 5. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  MAMMAMIA hapa tulipo fikia tuiache Zanzibar iamue mstakabali wake. Wiki iliyopita niliposoma hotuba ya Alli Ameir nilitambua kwamba analalilia Muungano kwasababu zake binafsi siyo kwa maslahi ya Zanzibar.
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Huyu babu si Mngoni sasa UAMSHO umempataje?
   
 7. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nape anasubiri mzee ajiengue ili naye aje kusema kuwa "hivi karibuni ilikuwa tumfukuze CCM huyo mzee"
   
 8. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huu mkoa wa Zanzibar naona nao umezidi kelele, mbona wa mkoa wa Mwanza na kwingine kama Iringa, Mbeya wapo kimy tu, tunakalea kila siku lakini haka choki kudeka na kulalamika, aaaah, kama kamekua si kaende kakajitegemee bwana, kasehemu kenyewe kadogo, wilaya ya Mufindi kubwa!!!!
   
 9. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Kumbe bado wanautaka muungano............."tuwe na muungano wa mkataba" mara "Urais wa muungano wa kupokezana" n.k
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  ..huyu anapoteza muda wa watu tu.

  ..muungano wa mkataba ndiyo kitu gani?

  ..mbona Nyerere na Karume walisaini mkataba??
   
 11. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Uamsho siyo debe tupu kumbe, lina kitu ndani tena vigunge.
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hakuna tena Muungano maana Serikali ya Kikwete inaelekea kuanguka.
   
 13. M

  MTK JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  This is the folly of mankind; we can not appreciate something till it is no more!! Wazenj wataulilia muungano na kusaga meno pale utakapokuwa haupo tena!! wanaviona vinaelea wanasahau viliundwa?! jamani hata Hassan nassoro Moyo tena?! kweli mfadhili mbuzi waweza kumla nyama lakini binadamu atakuudhi.
   
 14. M

  Makupa JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  mkuu Nape kemea hili pepo
   
 15. Isalia

  Isalia JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 950
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Hicho kichwa ulichopewa kitumie inavyotakiwa uckiweke kama tikiti maji linalosubira kuliwa inawezekana wewe umetoka katika familia ya watumwa walio kuja kuuzwa z'bar ndomana unahasira nayo huwezi kuifananisha mwanza na z'bar katika historia ya z'bar wewe unajita mtanzania kutokana na z'bar na tanganyika kama una akili kwanza dai tanganyika yako na fahamu nchi haitambuliki kwa ukubwa wa eneo
   
 16. a

  adebisi Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Huyu Moyo anatumia Masaburi kuwaza...hivi nikiwauliza wazenji Tunawanyonya Kitu gani nyie?????

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Mkuu, inapofikia mahali Mzee kama huyu naye anasema tu bila kuwa na ground, lipo tatizo.

  Wznz wanataka sana muungano hawasemi tu ndiyo maana wamebaki kuzunguka mbuyu wakiimba serikali 3, mkataba, ushirikiano, mkataba wa Uswis n.k. Kelele zote za Vunja muungano sasa kimyaaa!

  Wanajaribu kutikisa kibiriti, wamuulize Salimin Amour aliyekwenda Dodoma kwa mbwembe, baada ya kikao akarudi na kukuta kila kitu 'upside down' wakiwemo walinzi wake. Kuanzia siku hiyo hadi leo Komandoo Kimyaa.

  Huyu Moyo mtoto wake si alitaka kugombea Ubunge Bara kama alivyokuwa wa Mwinyi n.k. Sasa analeta kelele mtoto wake atagombea wapi next time, maana Tanganyika inazinduka, hakuna kumuonea mtu huruma.

  ZNZ semeni, mkataba unahusu nini?
  Serikali 3 mtachangia nini kuendesha hiyo ya tatu?
  Serikali 3, hiyo ya tatu itafanya kitu gani zaidi ya zile mbili?

  LET ZNZ GO!
   
 18. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wasubr tuwape zenji yao miltary base ya kigambon ikikamilka
   
 19. terabojo

  terabojo JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Nape hana bavu wa kuto kadi ya re! Mchanga kisiuasa na si mweledi!!
   
 20. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,238
  Likes Received: 931
  Trophy Points: 280
  l like this,if Zanzibar goes I Will have my Tanganyika back.
   
Loading...