Mzee Chidumule na wimbo wake.....

maishapopote

JF-Expert Member
May 28, 2009
3,410
6,067
Nampenda,Kumuheshimu na kumfurahia kazi zake kila siku mzee Cosmas Chidumule,mimi kwangu sauti yake ni sauti ya dhahabu,zaidi ya TID,Q chief, Linex na wengine wengi......

Kuna nyimbo zake nyingi nimezisikiliza,na ninayoipenda mno ni, Neema, na usitumie Pesa Kama fimbo Baba..... hizi zipo kwenye simu yangu, Tablet,Laptop,kwenye flas kwenye Gari na nyumbani,it is every where in my Life....

najaribu kumfananisha na wengine kama kina marehemu Marijani Rajabu, na Hemed Manet na naona wana tofauti, kuanzia sauti had maudhui.....huyu chidumule aliacha muziki mapema na kuhamia kwenye dini ila kidunia angekua ametoa nyimbo nyingi na nzuri mno....

alikua akiibeba DDC vilivyo,inasemekana huo wa usitumie pesa kama fimbo naskia alimtungia kigogo mmoja wa serikali ambae miaka hiyo ya 81 had 83 alikua akitumia nguvu nyingi ya pesa kumtaka mwanamke wa chidumule( ni mke wake hadi sasa)

Nilikua nahisi huyo Kigogo ni Baba yake Madame,lakini kuna watu wanasema sio yeye,naomba mwenye uhakika atujuze hapa.

link ya pesa ndo hiyo hapo
 
Alishaacha ya dunia akaokoka na kumtumikia Yesu Kristo..nilitamani uweke na hizo za dini katika list yako ya favourites
 
Hizi ndizo hazina za Muziki wa Tanzania. Ni nadra kupata na kuitengeneza chemistry ya muziki kama ile iliyokuwepo Sikinde. Kila chombo kilikuwa na mtu mahiri na ndio maana mziki wake hauchoshi kuusikiliza.
 
Muziki zamani bhana. Kwanza kulikuwa na wanamuziki tofauti na sasa kuna wasanii wa muziki. Mtu unajiita mwanamuziki afu hujui kupiga ala yeyote ya muziki! Hata filimbi?

Kwa ujumla wanamuziki karibia wote waliokuwa wakipiga kwenye bendi zetu za enzi hizi kama ddc, juwata, maquis, dar international nk walikuwa ni waimbaji wazuri na watuzi pia. Kitu kama Milima ya kwetu cha super rainbow, Imakulata wa bima, Talaka ya hasira cha ddc ukivisikiliza huchoki.
 
Chidumule ni kama alilima wee ilipofika wakati wa kuvuna akasusa shamba
mziki wake ni very very unique
wimbo wa Neema kila alie urudia alishindwa kuuimba vizuri
Kila hufanya maamumuzi yake kwenye maisha mkuu...kwa namna itakavyompendeza....
 
Nyimbo ya Chidumule inayoitwa Neema nilikumbana nayo kwenye mtihani wa kiswahili ni balaa
 
Yeah na ile ya
Libarikiwe neno hiili, la uzimaa wa roho
Pembe zote za nchi na duniani kote
Likaenee injili ya uzima wa rohonii

Neno hili liponye nafsi zote zilizo bado gizani. .......
Ntapataje wimbo huu tafathali +254716788792 whatsapp
 
Back
Top Bottom