Mzee baba, pakacha limeanza kuvuja ujue...

Tuhuma ni tuhuma tuu... Lakini kwangu tuhuma zisizothibitika wala kuthibitishwa zinabaki kuwa uzushi.... Na mimi sina kaliba na uzushi.... Sijui nini kilinipelekea kukumbuka riwaya ya Ngoswe... PENZI KITOVU CHA UZEMBE... Dah nikayakumbuka ya kudamka alfajiri na mapema kwenda kule kilimani kumuona cheupe dawa... Si adhabu hii jamani... Mateso bila chuki... Kiroho safi kabisa... Hongera mzee baba... Hongera cheupe....

Kuna wale wazee na kawimbo kao kalikokosa udhamini wa kuingia studio... Naambiwa singo yao ile haikidhi vigezo... Kale kawimbo ka MATEMBELE NI MATAMU.... Kweli Ngoswe aliona mbali... Na mtunzi wa MATEMBELE aliona karibu....

mzee baba huku kwenye chama la wana hali si shwari... Wanachonga waziwazi sasa hivi... Hawana shukrani na hawana upendo kwa wageni.. Kwao wao mgeni ni siku ya kwanza tuu... Sasa wnalalamikia uwingi wa wageni... Wenyewe wanawaita wakuja.. Wanawaita mizigo... Wanawaita wadekaji.... Hali si shwari sana pakacha limeanza kuvuja....

Mkubwa mpya wa usalama wetu Barabarani naye kaharibu... Japo ndio kutenda kwa weledi... Anapingana na dhana ya kukusanya mapato yetu ili kibubu kitune... Wanakaya wamemfurahia sana... Hakuna tena kutoza faini za kijinga... Kwahiyo hapa hakuna tena viwango elekezi vya kukusanya kwa siku wiki hata mwezi... Wanakaya wamepata mkombozi hatimaye... Mungu naye hujibu maombi kwa wakati wake....!!!!... Ila zile mbwembwe za jeshi la polisi kujivunia kuwa mwezi huu wamekusanya billion ngapi zitakoma.. Wao sio kitengo cha mamlaka ya mapato.. Faini za uonevu kwishney....

Mzee baba pakacha limeanza kuvuja... Wameanza kupambana na wewe... Mbwa anataka kula mbwa... Filamu ya half ray imedoda... Ile ya viongozi 20... Filamu ya nabii Tito imechacha.. Wanakung'ong'a.. Kikulacho ki nguoni mwako... Wasikupake mafuta kwa mgongo wa chupa..... Ni wanafique

Uliyasikia ya Benedict ? Yule mtia nia?
Uliyasikia ya Nnauye Jr?
Uliyasikia ya bwana Ole ?
Umeyasikia ya Riz moko?
Wote wametoa ya moyoni halafu wakakana lakini neno likitoka limetoka ni kama risasi haina rivasi.... Basi ndio hivyo mzee baba... Hao wote ni kiwakilishi cha wengi ndani ya chama la wana...pakacha limeanza kuvuja... Naamini halijasababishwa na Ngoswe.... Inatosha tu kusema.... MATEMBELE ni MATAMU....!!!!
Mzee baba mshana jr hapa umechemka Penzi kitovu cha Uzembe siyo riwaya ile ni thamthiliya iliyoandikwa na MAREHEM EDWIN SEMZABA
 
nimeshindwa kabisa kutafsir fasihi iyo jaman, mwenye kuielewa ebu atu dadavulie japo na sisi tusio wana fasih tupate kuelewa kidogo
 
Tuhuma ni tuhuma tuu... Lakini kwangu tuhuma zisizothibitika wala kuthibitishwa zinabaki kuwa uzushi.... Na mimi sina kaliba na uzushi.... Sijui nini kilinipelekea kukumbuka riwaya ya Ngoswe... PENZI KITOVU CHA UZEMBE... Dah nikayakumbuka ya kudamka alfajiri na mapema kwenda kule kilimani kumuona cheupe dawa... Si adhabu hii jamani... Mateso bila chuki... Kiroho safi kabisa... Hongera mzee baba... Hongera cheupe....

Kuna wale wazee na kawimbo kao kalikokosa udhamini wa kuingia studio... Naambiwa singo yao ile haikidhi vigezo... Kale kawimbo ka MATEMBELE NI MATAMU.... Kweli Ngoswe aliona mbali... Na mtunzi wa MATEMBELE aliona karibu....

mzee baba huku kwenye chama la wana hali si shwari... Wanachonga waziwazi sasa hivi... Hawana shukrani na hawana upendo kwa wageni.. Kwao wao mgeni ni siku ya kwanza tuu... Sasa wnalalamikia uwingi wa wageni... Wenyewe wanawaita wakuja.. Wanawaita mizigo... Wanawaita wadekaji.... Hali si shwari sana pakacha limeanza kuvuja....

Mkubwa mpya wa usalama wetu Barabarani naye kaharibu... Japo ndio kutenda kwa weledi... Anapingana na dhana ya kukusanya mapato yetu ili kibubu kitune... Wanakaya wamemfurahia sana... Hakuna tena kutoza faini za kijinga... Kwahiyo hapa hakuna tena viwango elekezi vya kukusanya kwa siku wiki hata mwezi... Wanakaya wamepata mkombozi hatimaye... Mungu naye hujibu maombi kwa wakati wake....!!!!... Ila zile mbwembwe za jeshi la polisi kujivunia kuwa mwezi huu wamekusanya billion ngapi zitakoma.. Wao sio kitengo cha mamlaka ya mapato.. Faini za uonevu kwishney....

Mzee baba pakacha limeanza kuvuja... Wameanza kupambana na wewe... Mbwa anataka kula mbwa... Filamu ya half ray imedoda... Ile ya viongozi 20... Filamu ya nabii Tito imechacha.. Wanakung'ong'a.. Kikulacho ki nguoni mwako... Wasikupake mafuta kwa mgongo wa chupa..... Ni wanafique

Uliyasikia ya Benedict ? Yule mtia nia?
Uliyasikia ya Nnauye Jr?
Uliyasikia ya bwana Ole ?
Umeyasikia ya Riz moko?
Wote wametoa ya moyoni halafu wakakana lakini neno likitoka limetoka ni kama risasi haina rivasi.... Basi ndio hivyo mzee baba... Hao wote ni kiwakilishi cha wengi ndani ya chama la wana...pakacha limeanza kuvuja... Naamini halijasababishwa na Ngoswe.... Inatosha tu kusema.... MATEMBELE ni MATAMU....!!!!
Naskia Da Mange kasema 26march ni Muungano day?
 
Embu tuache utani, hivi kweli yule amekubali kuwa kimada? Kwanini na inawezekanaje???? Kama ni kweli, wasiwasi wangu yule dogo atapotezwa baada ya mapumziko ya dakika 15 kabla ya kipindi cha pili kuanza. Atakuwa anajua yale yasiyohitaji kujulikana.
 
Dogo!? Dakika 15? kupotezwa?
 
.
5e8742a7b5ae590e00ac821a99af6cde.jpg
Hahahahaha sasa huyo Prof yupo upande gani?
 
Dogo!? Dakika 15? kupotezwa?

Hahaha. Dogo kasajiliwa kwenye dirisha dogo kuwa kama kiraka tu na kuhakikisha timu inapata mahitaji yote kama vile mipira ya kuchezea, soksi na pia kuhakikisha kocha na msaidizi wake wanawasiliana vizuri. Hawezi kusimamia mawe! Ila bado siamini timu yetu imefikaje hapa???
 
Nimekupata vema sasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom