Mzee aliyetuhumiwa kumuua bintiye auawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee aliyetuhumiwa kumuua bintiye auawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 13, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MKAZI wa Kijiji cha Kilembo wilayani Sumbawanga katika Mkoa wa Rukwa, Venance Ntogwa(65) ameuawa na mwili wake kuchomwa moto na wanakijiji wenzake wakimtuhumu kumuua binti yake kwa kumroga.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa,Isuto Mantage amemtaja marehemu kuwa ni Stella Ntogwa (15) ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kilembo.

  Kwa mujibu wa Mantage mzee Venance ni baba mdogo wa marehemu.

  Kamanda Mantage alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana kijijini humo wakati waombolezaji wakiwa kwenye maziko ya binti huyo aliyefariki dunia ghafla Mei 9 mwaka huu.

  Alisema, siku hiyo ya tukio waombolezaji hao wakiwa makaburini kwenye maziko ya marehemu kijijini humo ilianza minong'ono kuwa Venance amemroga na kumsababishia kifo marehemu.

  “Chanzo cha mauaji ya mzee Venance ni imani za kishirikina kwani baada ya kifo cha binti huyo ndipo ilianza kusikika minong'ono kuwa kifo hicho si cha kawaida kwamba amerogwa na baba yake mdogo yaani mzee Venance” alisema.

  Inadaiwa kuwa baada ya maziko ya marehemu kundi la wananchi lilimvamia mzee huyo na kuanza kumpiga.

  Kwa mujibu wa Mantage, ilimlazimu mzee Venance kukimbia na kuingia kwenye nyumba ya mwanawe aitwaye Ibrahim Akilindogo na kujifungia humo kwa usalama wake.

  Inadaiwa kuwa, baada ya kujifungia humo waombolezaji hao waliichoma moto nyumba hiyo iliyoteketea ambapo mzee huyo akafia humo na mwili wake kuteketezwa na moto.

  Kwa mujibu wa Mantage hakuna aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo lakini msako unaendelea ili wahusika waweze kukamatwa.
   
 2. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Khaaa,bora nimezaliwa kazkazini,watu kule uc hawi ndio upo lakini upuuzi wa kichomana viberiti kushnehii,wanajua shilingi kwa saaana!kwanza hao wauwaji pia ni wanga wamejuaje??? Km muuaji ni huyo dingi mdogo?loooool
   
Loading...