GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,543
- 108,877
Yule Mzee ' machachari ' wa Klabu ya Yanga Ibrahim Akilimali muda si mrefu akizungumza ' mubashara ' kupitia Kipindi cha Sports Headquarters cha Efm ameamua ' kufunguka ' na kutoa ' Siri ' ya Yanga SC kufanya vibaya kwa kusema kwamba Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Ndugu Clement Sanga ndiyo adui namba moja wa Yanga na anaihujumu Yanga.
Aidha Mzee Akilimali amefichua pia ' Siri ' nyingine kwamba ni kweli jana Wachezaji wa Yanga SC waligoma kutokana na ' njaa ' narudia tena ' njaa ' namalizia kwa kusisitiza ' njaa ' ambayo sasa imekomaa kama siyo kuota mizizi hapo Klabuni huku akiwaonea huruma Wachezaji kwa maisha magumu ambayo wanapitia sasa huku wengi wao wakishindia tu Mlo mmoja na wengine wakishindia tu maji.
Mwisho Mzee Akilimali alimlaumu sana Nahodha wa Yanga SC Beki Nadir Haroub ' Cannavaro wa Pemba ' kwamba na Yeye anatumika na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga SC Ndugu Clement Sanga katika ' kuihujumu ' Timu yao. Mzee Akilimali amewataka wana Yanga SC wote duniani kusahau kuwa msimu huu Yanga SC itatetea Ubingwa wake huku akiitaka TFF kama wataona inafaa waipe mapema tu Kombe Klabu ya Simba kutokana na kwamba haoni Timu ya Kuizuia katika Kuchukua Ubingwa msimu huu kwa kusema Simba SC imesajili si tu vizuri bali ' Kisayansi ' zaidi kuliko wao Yanga SC ambao wamesajili ' Kiswahili Swahili ' au ki ' hovyo hovyo '.
Jamani wana Yanga SC wenzangu wote duniani huyu Mzee Akilimali siyo kwamba labda ana ' mahaba ' na Simba SC na pengine siyo mwenzetu huyu? Hivi Katiba yetu ya Yanga SC haina ' Kipengele ' cha Kumfukuza Mwanachama ' asiyeeleweka ' kama Mzee Akilimali? Jamani wana Yanga SC wenzangu popote mlipo haraka sana tuandamane ili huyu Mzee ' afukuzwe ' Yanga SC kwani tumeshamchosha.
Nawasilisha.