Mzee Aboud Jumbe aombwe radhi

Mzee Aboud Jumbe aombwe radhi

mzenjiboy

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Posts
907
Reaction score
387
CCM inapaswa kumuomba radhi mzee Aboud Jumbe kwa kumnyang'anya madaraka aliyokuwa nayo pamoja na cheo cha urais wa ZANZIBAR hapo 1984. Hayo yalitokea baada ya rais Aboud Jumbe kushabikia suala la serikali tatu jambo ambalo Mw/Nyerere alilipinga kwa nguvu zake zote kisha kumvua Jumbe nyadhifa zake zote. Jaji Warioba kuleta tena suala la serikali tatu katika rasimu zote mbili ya kwanza na ya pili. Hii inathibitisha ya kwamba mzee Jumbe aliona mbali sana na hakukosea kwa kile alichokuwa akikiamini. Kwa hili maCCM muombeni radhi mzee Jumbe.
 
Wacha sasa warambe matapishi yao !! Nchi hii kila mmoja ni raisi... nani anadiriki kumkosoa nani? Bado tuna safari ndefu.......
 
CCM inapaswa kumuomba radhi mzee Aboud Jumbe kwa kumnyang'anya madaraka aliyokuwa nayo pamoja na cheo cha urais wa ZANZIBAR hapo 1984. Hayo yalitokea baada ya rais Aboud Jumbe kushabikia suala la serikali tatu jambo ambalo Mw/Nyerere alilipinga kwa nguvu zake zote kisha kumvua Jumbe nyadhifa zake zote. Jaji Warioba kuleta tena suala la serikali tatu katika rasimu zote mbili ya kwanza na ya pili. Hii inathibitisha ya kwamba mzee Jumbe aliona mbali sana na hakukosea kwa kile alichokuwa akikiamini. Kwa hili maCCM muombeni radhi mzee Jumbe.
Mkuu, suala la serikali tatu sio la Jaji Warioba, ni la wananchi wengi. Hivi hata nishani kanyimwa ya miaka 50 ya Mapinduzi?
 
hatusemi well stated... tunasema well'said... hahaha !!!
 
Mpaka sasa ccm hawajaafiki serikali tatu wamwombe radhi kwa lipi?
 
CCM inapaswa kumuomba radhi mzee Aboud Jumbe kwa kumnyang'anya madaraka aliyokuwa nayo pamoja na cheo cha urais wa ZANZIBAR hapo 1984. Hayo yalitokea baada ya rais Aboud Jumbe kushabikia suala la serikali tatu jambo ambalo Mw/Nyerere alilipinga kwa nguvu zake zote kisha kumvua Jumbe nyadhifa zake zote. Jaji Warioba kuleta tena suala la serikali tatu katika rasimu zote mbili ya kwanza na ya pili. Hii inathibitisha ya kwamba mzee Jumbe aliona mbali sana na hakukosea kwa kile alichokuwa akikiamini. Kwa hili maCCM muombeni radhi mzee Jumbe.

Suala lililomtoa Jumbe madarakani halikuwa la serikali tatu bali kuiondoa Zanzibar kwenye Muungano na kujiunga na nchi fulani la kiarabu ambayo sintaitaja hapa. Huo ulikuwa ni uhaini na ashukuru huruma alizopata hadi sasa. Alistahili kufungwa jela na kutumia ndoo kwa ajili ya shughuli zake muhimu fulani fulani.

Wasiliana na Seif wa CUF atakupa mkanda mzima.
 
hakuwa anashabikia serikali tatu,yeye alihoji"setup" ya muungano,kwamba "tanganyika imevaa koti la muungano"yaani inaonekana kama tanganyika imeimeza zanzibar kwenye huu muungano. Wazee wa serikali tatu tunawajua wale wa G55 akina Njelu Kasaka na wenzake.....
 
Jamani mwacheni mzee wa watu kajikalia zake kimya Kigamboni. Kama anataka kuombwa radhi anao mdomo na kichwa chake. Vinginevyo mwache amalizie siku zake kwa amani.
 
[
QUOTE=Synthesizer;8469714]Suala lililomtoa Jumbe madarakani halikuwa la serikali tatu bali kuiondoa Zanzibar kwenye Muungano na kujiunga na nchi fulani la kiarabu ambayo sintaitaja hapa. Huo ulikuwa ni uhaini na ashukuru huruma alizopata hadi sasa..

[/QUOTE]

Mkuu! Tusihalalishe kudhalilishwa kwa Jumbe na kunyanyaswa kwake kwa habari ambazo hatuziweki wazi..... kama ni kuwatendea haki wale wote wanao sympathise naye, weka hapa hizo habari za li nchi fulani liliomponza Jumbe!
Maalim Seif hayuko tena katika nafasi ya kusema lolote lile...yeye ni VICE PRESIDENT!
 
CCM inapaswa kumuomba radhi mzee Aboud Jumbe kwa kumnyang'anya madaraka aliyokuwa nayo pamoja na cheo cha urais wa ZANZIBAR hapo 1984. Hayo yalitokea baada ya rais Aboud Jumbe kushabikia suala la serikali tatu jambo ambalo Mw/Nyerere alilipinga kwa nguvu zake zote kisha kumvua Jumbe nyadhifa zake zote. Jaji Warioba kuleta tena suala la serikali tatu katika rasimu zote mbili ya kwanza na ya pili. Hii inathibitisha ya kwamba mzee Jumbe aliona mbali sana na hakukosea kwa kile alichokuwa akikiamini. Kwa hili maCCM muombeni radhi mzee Jumbe.
CCM wamemfanya Mzee Jumbe kukosa amani ya Maisha toka Mwaka 1984
 
Back
Top Bottom