Mzazi: Nairobi ya mwalimu iko wapi?

Mzazi: Nairobi ya mwalimu iko wapi?

Joined
Feb 11, 2013
Posts
76
Reaction score
7
Mtoto mmoja alitoka shule huku analia kweli kweli hadi alipofika kwao. Baba yake kuona mwanaye analia,ikabidi amuulize kulikoni;

Baba: Unalia nini mwanangu mzuri? Nini kimekusibu huko utokako?
Mtoto:Nimepigwa sana baba,nimeambiwa twende wote shule.

Baba na mwanaye wakaongozana kwenda shule pamoja. Walipofika moja kwa moja wakaingia katika ofisi ya mwalimu mkuu.

Mwalimu: Karibu sana mzazi,mwanao tumemuuliza Nairobi iko wapi,kashindwa kujibu ndio maana tukamuadhibu.
Baba akamgeukia mtoto wake na kumpiga bonge la kibao tena usoni halafu akamwambia;

Baba: Kila siku nakukataza kuchezea vitu vya watu hukomi, haya Nairobi ya mwalimu iko wapi?

RISASI:NOVEMBA 14, 2015.

==========

Kwenu waalimu, na wengineo endapo kama mngekuwa waalimu mngechukua hatua gani hapo?
 
Back
Top Bottom