Mzazi ataka maelezo ni kwa vipi mwanae kafaulu darasa la saba wakati hajui kusoma na kuandika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzazi ataka maelezo ni kwa vipi mwanae kafaulu darasa la saba wakati hajui kusoma na kuandika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Invarbrass, Jan 30, 2012.

 1. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkazi wa kijiji cha Mohoro rufiji, Saidi Makwangu, amemuuliza Mwenyekiti wa kijiji hicho nini kifanyike kufuatia mwanae kufaulu mtihani wa darasa la saba wakati hajui kusoma wala kuandika.Mwenyekiti huyo alishindwa kumjibu mzazi huyo na akaomba kwanza apate ushauri kutoka kwa Kamati ya Maendeleo ya Kata. " nilimjibu kuwa ushauri sina nakwenda kwenye kikao cha WDC nikirudi nitakuwa na majibu"alisema Mwenyekiti huyo. Mkuu wa sekondary ya Mohoro alikochaguliwa kujiunga mtoto huyo, alisema mtoto huyo ajiunge na kidato cha kwanza mara moja maaana kuna mtihani wa kidato cha pili utamchuja kama atashindwa.

  My take: majibu ya kufanya mtihani wa hesabu kwa njia ya matipo chois ndio hayo.

  Source: Mwananchi Ya leo 30/January 2012
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wizara ya elimu inaongozwa na serikali ya chichiem.

  Wanachotaka wao ni mtoto aende shuleni wao wapate pesa toka kwa mzazi
  wala hawataki kujua cha anajua kusoma wala anajua kuandika,hata hapa mtaani kwetu kuna wazazi wanalaani hii mbinu ya chichiem wanachofanya kwa watoto mijinga kama huyu tajwa hapo juu.

  Tuna hasara na uongozi mbovu uliopo ngazi ya juu.

  chichiem ni janga kwa wanainchi.
   
 3. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #3
  Jan 30, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  walimu ktk shule huona fahari kufaulisha watoto hata wasio na sifa,wanachokifanya ni shule kuandaa pesa ya rushwa kwa wasimamizi wa mitihani na hatimae wanafunzi hupewa majibu,ndio sababu si ajabu tumesikia wanafunzi wakifaulu kwa alama zinazofanana na wengine hufaulu wakati hata kuandika jina lake hawezi hii ni kwa sababu majibu wanapewa na ikibidi wanasaidiwa kujaza.
  Hii ni nchi ya kusadikika.
   
 4. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nikiwa kama mwalimu, natamani kuona kwamba tunakuwa na wazazi/walezi wengi zaidi wenye mwelekeo wa mzazi huyu wa kuhoji na kufuatilia (ingawa amechelewa sana kuanza kazi hiyo!). Inatia moyo pale amabapo kuna wazazi/walezi ambao kwao suala muhimu sio tu kufaulu na kuleta nyumbani reports zenye maksi nzuri bali wanaofuatilia mchakato mzima wa wanao kupata alama hizo.

  Hili limeniamsha hasa kwa wakati huu ambako swala muhimu si namana gani mtoto anajifunza bali ni alama nzuri kiasi gani anapata (hata kama zitapatikana ndivyo sivyo)
   
 5. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ingawa siasa ina nafasi yake kubwa tu katika kuamua mwelekeo wa elimu tunaotaka, lakini nikuhakikishie kuwa elimu ya msingi katika nchi hii ni janga kuliko hata shule za sekondari za kata! Mark my words, tatizo sio CCM tu. Tatizo lipo katika mfumo mzima -- mfumo umekwisha bakwa na hilo ni kubwa zaidi ya kuwa chini ya CCM.
   
 6. papason

  papason JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Kesi nyingi za namna hii huwa ni michezo ya kuigiza, ingawa mara chache sana huwa kweli!

  Possible huyo mwanafunzi ni wakike na huyo baba yake ana mpango wa kumuoza hivyo anatafuta mbinu ya kumuachisha shule, The only solution ni kuwauliza waalimu waliomfundisha huyo mwanafunzi primary school ndio tutapata ukweli wa mambo

  Huku usukumani 'drama' kama hizo huwa ni nyingi sanaa, mwishowe wazazi wa ma binti huaibika na kuishia lupango
   
Loading...