Mzazi ahoji ni kwa vipi mtoto wake alifaulu la saba

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
MKAZI wa Kijiji cha Mohoro amepeleka malalamiko kwa mwenyekiti wa kijiji hicho akiomba apewe ushauri wa nini cha kufanya baada ya mwanawe wa kiume kufaulu mtihani wa darasa la saba wakati hajui kusoma na kuandika.Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Chumbi kilichofanyika juzi katika Kijiji cha Kiwanga, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mohoro, Saidi Makwangu alisema kuwa mkazi huyo alifika ofisi kwake akiomba apewe ushauri wa nini cha kufanya baada ya mwanawe ambaye hajui kusoma na kuandika amefaulu.
Makwangu alisema kwa kuwa kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata kina wataalamu wengi katika fani mbalimbali alitaka apate majibu ya kwenda kumjibu mzee huyo ambaye amekuwa akimfuata kila wakati kupata ushauri.
“Nilimjibu kuwa ushauri sina nakwenda kwenye kikao cha WDC nikirudi nitakuwa na majibu,” alisema mwenyekiti huyo.
Akijibu swali hilo Mkuu wa Shule ya Sekondari Mohoro ambako mtoto huyo amechaguliwa kwenda Masyanga Mwita alisema kuwa mwanafunzi huyo anatakiwa kuanza masomo yake haraka iwezekanavyo na kama atakuwa hana uwezo mtihani wa kidato cha pili utamuengua.
Mwita alisema kuwa akiwa kidato cha pili atafanya mtihani kwa mara ya kwanza na akifeli atapewa nafasi nyingine ya kurudia na akishindwa atarudishwa nyumbani.
Kumekuwa na madai kuwa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wamekuwa wakipewa majibu na wasimamizi wa mitihani hali inayosababisha baadhi ya wanafunzi kufaulu wakiwa hawana uwezo kitaaluma
 
hayo ni maelekezo ya wanasiasa ya kufaulisha kwa asilimia 100 we ulitaka walimu wafanyeje zaidi ya kuonesha mitihani ili nao wendelee kwenda chooni(ashakumu si matusi wadau)
 
hayo ni maelekezo ya wanasiasa ya kufaulisha kwa asilimia 100 we ulitaka walimu wafanyeje zaidi ya kuonesha mitihani ili nao wendelee kwenda chooni(ashakumu si matusi wadau)

kama hajui kusoma wala kuandika,hata kama alionyeshwa mtihani bado asingefaulu
 
Huyu mwalimu mkuu hana akili. anataka kumuadmit mtu asiyejua kusoma wala kuandika. kwanini nafasi hii asipewe mtu mwingine kuliko kupeleka mbumbumbu.
HUYU mbumbumbu ata tumia resources ambazo zingetumika mahali pengine more productively
 
baada ya kuonekana hata form 4 wanamaliza wakiwa hawajaelimika, serikali ikawapaisha kwa division five...

majanga!!
 
Nina mashaka na ukweli wa habari hii.Mtoto kama hajui kusoma na kuandika atakariri vipi? Labda waseme ni dhaifu lakini kusema hajui kusoma na kuandika ni exaggeration.
 
Back
Top Bottom